Skip to main content

Posts

Showing posts from August 12, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

DKT. DOTO BITEKO ANOGESHA MASHINDANO YA NGALAWA TAMASHA LA KIZIMKAZI

 Naibu Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Mheshimiwa Dkt. Doto Mashaka Biteko amesema kuwa mashindano ya ngalawa race ni miongoni mwa matukio makubwa ya kiburudani yanayoipamba Kizimkazi Festival 2026. Mashindano hayo yamefanyika Kizimkazi, Kusini Unguja Agosti 12, 2026 yaliyokuwa na ushindani mkubwa ambapo Nassor Pandu wa Mkunguni ameibuka mshindi wa mashindano ya ngalawa ikiwa ni sehemu ya shughuli mbalimbali zinazoendelea katika Tamasha la Kizimkazi. “ Ni dhahiri kwamba mashindano haya yamekuwa muhimu kwa vijana na jamii kwa ujumla. Tukio hili limewaleta pamoja wadau mbalimbali na kuchangia kwa kiasi kikubwa juhudi za kuboresha mazingira ya michezo na burudani,” amesema Dkt. Biteko. Dkt. Biteko ameongeza kuwa mashindano ya Ngalawa race Kizimkazi Festival yameendelea kutoa fursa za kiuchumi kwa vijana mbalimbali katika kushindana hadi kupata timu mbili bora za Mchangamle na Mkunguni ambapo kila timu imehusisha manahodha 10.

TRA TANGA YATOA MAFUNZO MABADILIKO SHERIA ZA KODI KWA WAFANYABIASHARA

 NA: MWANDISHI WETU, TANGA Katika kuhakikisha wafanyabiashara wanakuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka 2026/2027, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Tanga, imetoa mafunzo kwa wafanyabiashara mkoani humo. Mafunzo hayo yametolewa Agosti 12, 2026, katika Ukumbi wa YDCP Jijini Tanga. Katika mafunzo hayo, wafanyabiashara wamejengewa uwezo juu ya mabadiliko mbalimbali ya sheria za kodi yaliyofanyika ili kuiwezesha TRA kutekeleza majukumu waliyopangiwa na serikali kuu. Akifungua mafunzo hayo, Meneja wa TRA mkoa wa Tanga, CPA. Castro John, amesema sheria zaidi ya 15 za kodi zimefanyiwa mabadiliko, hivyo wanalo jukumu la kutoa elimu kwa wafanyabiashara. "Niwashukuru wafanyabiashara wa Tanga kwa kujitokeza kupata elimu hii muhimu kwani wafanyabiashara wanapokuwa na uelewa wa mabadiliko haya, basi utekelezaji wa ulipaji kodi utakuwa mwepesi," amesema CPA John. Maofisa mbalimbali kutoka TRA Makao Makuu waliwaelimisha wafanyabiashara hao maba...

AMBASSADOR CHEN: YOUTH ARE THE BRIDGE OF CHINA-TANZANIA FRIENDSHIP

 By Prosper Makene  Ambassador of the People’s Republic of China to Tanzania, H.E. CHEN Mingjian said that young people carry the future of China-Tanzania relations and must be placed at the centre of cooperation between the two countries. Her remarks were made during the "China-Tanzania Dialogue on Youth Development and Exchange" held in Dar es Salaam on Wednesday. The Dialogue brought together more than 100 representatives from the governments of China and Tanzania, universities, infrastructure companies, media, and students. It is being held in a landmark year as 2026 marks the 70th anniversary of China-Africa diplomatic relations and has been declared the "China-Africa Year of People-to-People Exchanges." Speaking at the opening, Ambassador Chen reflected on the historic ties between the two countries. "Over the past seven decades, China and Tanzania have written a remarkable chapter of solidarity and cooperation. Our friendship has been tested by time and ...

KUTOKA MFANYAKAZI WA KAWAIDA HADI KUWA MHANDISI: MAFANIKIO YA MHANDISI LUKUWI WA CRJE

Na Prosper Makene ;Dar es Salaam *"Nilipopata kazi yangu ya kwanza niliogopa kusema 'sijui'. Lakini CRJE ilitupatia mazingira mazuri. Wahandisi wakubwa walitufundisha kazini."* Hayo ni maneno ya Mhandisi Titus Lukuwi wa kampuni ya CRJE, kijana ambaye alianza kama mfanyakazi wa kawaida mwaka 2022 na leo ni miongoni mwa wafanyakazi muhimu wa kiufundi katika miradi mikubwa ya ujenzi nchini. Hadithi ya Lukuwi ilikuwa moja ya vivutio vikubwa katika "Mjadala wa China-Tanzania kuhusu Maendeleo na Ubadilishanaji wa Vijana" uliofanyika Dar es Salaam leo.  "Nilianza kazi nikiwa sijui chochote. Kupitia mafunzo ya CRJE mwaka 2023 na 2025, hatua kwa hatua nilijifunza ujuzi wa uhandisi, mawasiliano, utekelezaji wa miradi na viwango vya ubora," amesema Lukuwi.  "Leo niko katika timu inayotengeneza miundombinu ya ubora kwa Tanzania. Matumaini yetu ni kwamba katika miaka michache ijayo wahandisi wa Kitanzania watakuwa na uwezo wa kuongoza miradi kwa ajili ya k...

GEREZA KWAMNGUMI LAKABIDHI ALIYEKUWA MFUNGWA VIFAA VYA UJENZI

 Na Ssgt Mawazo Mtondo  Mkuu wa Gereza la Kwamngumi mkoani Tanga, Mrakibu wa Magereza (SP) Francis Makelemo, Agosti 11, 2026, aliongoza zoezi la kumkabidhi aliyekuwa mfungwa, Ndugu Tumaini Mahuji, vifaa mbalimbali vya ujenzi baada ya kumaliza kutumikia kifungo chake katika Gereza hilo. SP Makelemo amesema Jeshi la Magereza limeendelea kuwa chuo cha mafunzo kwa kuwapatia wafungwa fursa ya kupata elimu, ujuzi na maarifa ya ufundi stadi, pamoja na vitendea kazi vinavyowawezesha kujitegemea na kuendesha maisha yao wanaporejea katika jamii. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Bw. Ally Mkwavinga, alisema juhudi zinazofanywa na Jeshi la Magereza katika kuwajengea wafungwa uwezo na kuwapatia ujuzi ni muhimu katika kuwaandaa kurejea katika jamii wakiwa na uwezo wa kujitegemea. Katika hafla hiyo, Ndugu Tumaini Mahuji alitoa shukrani kwa serikali na uongozi wa Jeshi la Magereza kwa kukabidhiwa cheti kutoka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), pamo...

KITUO KIPYA CHA MIKUTANO ARUSHA KUHUDUMIA WATU 5000 KWA WAKATI MMOJA-WAZIRI KOMBO

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), amesema kuwa, ujenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mlima Kilimanjaro (MK-ICC) jijini Arusha, utaongeza uwezo wa Tanzania katika kuandaa mikutano ya kitaifa, kikanda na kimataifa kwa kuondoa changamoto ya muda mrefu ya nchi ya kutokuwa na kumbi za kubeba watu wengi kwa wakati mmoja. Waziri Kombo ametoa kauli hiyo wakati wa kikao kati ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) chini ya mwenyekiti wake, Mhe. Najma Murtaza Giga (Mb) na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kilichofanyika kwenye ukumbi wa Bunge jijini Dodoma Agosti 12, 2026. Balozi Kombo alieleza kuwa ujenzi huo ni utekelezaji wa vitendo wa Diplomasia ya Uchumi kupitia utalii wa mikutano; kuvutia uwekezaji wa ndani na nje; kuongeza ajira; kuvutia utalii; kuongeza mapato ya Serikali; kuongeza mapato ya fedha za kigeni na kuchochea maendeleo ya sekta za utal...

BALOZI KHAMIS OMAR: MBEYA TUMIENI FURSA ZENU KUINUA UCHUMI WA TAIFA

 MWaziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amesema Mkoa wa Mbeya na kwa ujumla Nyanda za Juu Kusini una uwezo mkubwa wa kuongeza mchango wake katika uchumi wa Tanzania, akisisitiza umuhimu wa kuongeza uzalishaji, kuchakata mazao na kuimarisha uwekezaji katika viwanda. Mhe. Balozi Omar ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja mkoani Mbeya, ambapo alitembelea Ofisi za Mkoa za Chama cha Mapinduzi (CCM), jijini Mbeya. Amesema Nyanda za Juu Kusini zinachukua takribani asilimia 20 ya eneo lote la Tanzania, lakini mchango wake katika Pato la Taifa bado haujaakisi kikamilifu ukubwa wa eneo hilo na utajiri wa fursa zilizopo. Amesema hali hiyo inatoa nafasi kwa Serikali, sekta binafsi na wadau wengine kuongeza uwekezaji katika kilimo, madini, viwanda na sekta nyingine za uzalishaji ili kuongeza tija na mapato ya wananchi pamoja na Taifa kwa ujumla. “Bado tuna fursa kubwa sana ya kuimarisha mchango wetu katika pato la Taifa uendane na eneo tulilonalo, na si kwa s...

KATIBU MKUU CCM AFUNGUA TAWI LA CHAMA KIBUTENI

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Asha-Rose Migiro, amefungua rasmi Tawi la CCM Kibuteni, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja, leo tarehe 12 Agosti 2026. Tawi hili lina historia kubwa tangu nyakati za ASP na TANU, na ni jambo la kujivunia kuona sasa lina sura mpya inayokwenda sambamba na mahitaji na hadhi ya Chama. Dkt. Migiro amewahimiza viongozi na wanachama kuhakikisha Tawi hilo linakuwa kituo cha uhai wa Chama, mshikamano, mafunzo, vikao na utekelezaji wa shughuli za Chama. Pia, Katibu Mkuu amewashukuru wana-CCM wa Kibuteni kwa mapokezi mazuri, upendo na zawadi.

RAIS DKT. MWINYI: TAMASHA LA KIZIMKAZI NI JUKWAA LA UTAMADUNI, UTALII NA FURSA ZA UWEKEZAJI

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Tamasha la Kizimkazi limeendelea kuwa jukwaa muhimu la kutangaza utamaduni, utalii, biashara na fursa za uwekezaji zilizopo Zanzibar, sambamba na kuchochea maendeleo ya wananchi. Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 12 Agosti 2026, alipokuwa akizindua rasmi Tamasha la Kizimkazi 2026 lenye kaulimbiu “KIZIMKAZI Kumenoga!” katika Mkoa wa Kusini Unguja. Amepongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa maono ya kuasisi Tamasha hilo, ambalo limekuwa likichangia kuhifadhi mila na utamaduni, kukuza utalii na kufungua fursa za kiuchumi kwa wananchi. Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza umuhimu wa kutumia Tamasha hilo kutangaza fursa za uwekezaji katika utalii, uvuvi, mwani na Uchumi wa Buluu, huku Serikali ikiendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji na miundombinu ya uzalishaji. Amesema Tamasha la Kizimkazi linaunga mkono dhamira ya Serikali ya kuongeza ...