Skip to main content

Posts

Showing posts from May 7, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Takukuru Mwanza Yaokoa zaidi ya Millioni Mia Saba, Mikopo ya Asilimia kumi.

 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini(TAKUKURU) imefanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi Millioni Mia Saba kwenye utoaji wa Mikopo ya Asilimia kumi ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa mwaka wa fedha 2024/2025. Taasisi hiyo imeokoa shilingi Millioni 706.2 kutokana na Uhakiki na Udhibiti uliofanyiia kwenye utoaji wa Mikopo ya Vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu inayotokana na asilimia kumi ya mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo.  Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza Protas Henry amesema kuwa katika Uhakiki huo,Vikundi 41 ambavyo Mikopo yake ilikuwa na Thamani ya Millioni Mia Saba havikukidhi vigezo.  Vikundi hivyo vilibainika kuwa na Makosa mbalimbali ikiwemo Kuomba mkopo hewa,kuwasilisha kwa kamati vielelezo vya kughushi mfano Profoma invoice na kuwasilisha Mikataba ya uongo ya maeneo ya kufanyia biashara,kuwasilisha bei za Juu za vifaa kuliko bei ya soko,kutokuwa na maeneo ya kufanyia biashara pamoja na Kuomba mkopo kwa ajili ya...

Walioula mikopo ngazi ya Diploma hadharani

Na: Mwandishi Wetu, Dar Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa majina ya wanufaika wa mikopo ya elimu kwa ngazi ya Stashahada (Diploma) walioomba kwenye dirisha la mwezi Machi, 2025. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dk. Bill Kiwia, kupitia Taarifa yake kwa Umma, Mei 05, 2025, ameeleza kuwa fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 1.94 zimetengwa ili ziwanufaishe wanafunzi 873.. Sambamba na hilo, taarifa hiyo imeeleza kuwa Shilingi Bilioni 1.51 zimetengwa kwa ajili ya chakula na malazi, Milioni 408 kwa ajili ya ada ya mafunzo huku vitabu na viandikwa vikigharimu shilingi 16,700,000. Aidha, ili kuona majina ya waliopata mikopo hiyo, waombaji wameelekezwa kuangalia taarifa zao kupitia akaunti walizoombea mikopo (SIPA). Huu ni mwendelezo wa utekelezaji wa maamuzi yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Dk. Samia Suluhu Hassan ya kuongeza wigo wa wanufaika wa mikopo kwa ngazi ya Stashahada, ambapo hadi sasa idadi ya wanufaika wa mikopo hiyo imeon...

kikwete na Nmb Wajadiliana Kiundani Maeneo ya Uwezeshaji Vijana na Jamii

Leo Jumatano ofisini kwake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete ametembelewa na ugeni wa Watendaji wa Benki ya NMB wakiongozwa na Bi. Vicky Bishubo, Meneja mahusiano Benki na Serikali waliofika kujitambulisha na kutambulisha Wizarani bidhaa mbalimbali zinazotolewa na Benki hiyo.  Katika kikao hicho wamejadiliana kiundani baadhi ya maeneo ambayo Benki hiyo inaweza shirikiana na Serikali katika kufanikisha uwezeshaji Vijana na Jamii. #KaziInaendelea #UwezeshajiVijana

Dkt. Biteko Awataka Maafisa Maendeleo Jamii Wasikubali Kuachwa Nyuma

📌 Awataka wafurukute  kuonesha umuhimu wa kadsa yao kwa Taifa 📌 Asema Wizara ya Nishati itashirikiana maafisa hao kusambaza umeme na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia  📌 Rais Samia apongezwa kwa kuongeza ajira za maafisa maendeleo ya jamii   Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati   Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza maafisa maendeo ya jamii nchini kushirikiana na kuhakikisha wanashirikishwa katika mipango ya nchi kuanzia ngazi za halmashauri na kuwezesha jamii kujiletea maendeleo endelevu na jumuishi kwa maslahi mapana ya Taifa. Dkt. Biteko amesema hayo leo Mei 7, 2025 jijini Dodoma wakati aliposhiriki kwenye Kongamano na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Tanzania. “Mahali popote ulipo ni muhimu kila mtu ajue upo usisubiri uambiwe upo, ama litokee tatizo ndio waseme nani anaweza, wapeni ulazima wakuu wenu kuwatafuta  kupitia chama chenu furukuteni kwenye halmashauri zenu na...

Ccm Yamlilia Mzee Cleopa David Msuya

 

MISA Tanzania Yaipongeza Wizara ya Habari kwa Kuwasilisha Bajeti ya 2025/2026

Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika – Tawi la Tanzania (MISA Tan) imepongeza uwasilishaji wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2025/2026, iliyowasilishwa leo bungeni na Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Paramagamba Kabudi, pamoja na Katibu Mkuu Bw. Gerson Msingwa. Mwenyekiti wa MISA Tan, Bw. Edwin Soko, amesema kuwa kuongezeka kwa bajeti hiyo ni ishara njema kwa maendeleo ya shughuli za wizara, hususan katika sekta za habari, utamaduni na sanaa, ambazo ni muhimu kwa kukuza demokrasia na utamaduni wa taifa. Bw. Soko pia ametoa wito kwa Mheshimiwa Rais kutafakari uwezekano wa kuifanya sekta ya habari kusimama kama wizara huru, badala ya kuwa chini ya wizara pana kama ilivyo sasa, ili kutoa nafasi ya kujadili kwa kina masuala ya taaluma ya habari bila kuingiliwa na sekta nyingine.

Serikali Mkoani Mara yakabidhi hati mbili za Mashamba ya Umwagiliaji

Serikali mkoani Mara imekabidhi hati mbili za shamba la umwagiliaji la Bugwema lililopo katika halmashauri ya Musoma vijijini kwa Tume ya Taifa ya  Umwagiliaji.  Mashamba hayo ni maalumu kwa ajili ya kuanza ujenzi wa miundombinu ya shamba hilo ili liweze kutumika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji. Shamba hilo ni  miongoni mwa mashamba matano ya mfano yanayotarajiwa kuanzishwa na Tume hiyo hapa  nchini kwa ajili ya kuboresha na kuimarisha kilimo cha umwagiliaji. Akikabidhi hati hizo leo Jumatano Mei 7,2025, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Gerald Kusaya ameiomba Tume hiyo kuhakiksha shamba hilo linaanza  uzalishaji haraka ili kuwanufaisha wakazi wa eneo hilo na mkoa kwa ujumla. Alisema Shamba hilo lenye ukubwa wa hekta 3,000 limekaa kwa muda mrefu bila kufanyakazi.  "Tayari tumekamilisha suala la umiliki wake tunaomba Tume ihakikishe uzalishaji unaanza mapema ili kuwanufaisha wananchi wa maenoe yale na watanzania kwa ujumla," amesisitiza.  Mkurugenzi Mk...

Serikali Yakabidhi Hati Mbili za Mashamba ya Umwagiliaji

Serikali mkoani Mara imekabidhi hati mbili za shamba la umwagiliaji la Bugwema lililopo katika halmashauri ya Musoma vijijini kwa Tume ya Taifa ya  Umwagilaiji.  Mashamba hayo ni maalumu kwa ajili ya kuanza ujenzi wa miundombinu ya shamba hilo ili liweze kutumika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji. Shamba hilo ni  miongoni mwa mashamba matano ya mfano yanayotarajiwa kuanzishwa na Tume hiyo hapa  nchini kwa ajili ya kuboresha na kuimarisha kilimo cha umwagiliaji. Akikabidhi hati hizo leo Jumatano Mei 7,2025, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Gerald Kusaya ameiomba Tume hiyo kuhakiksha shamba hilo linaanza  uzalishaji haraka ili kuwanufaisha wakazi wa eneo hilo na mkoa kwa ujumla. Alisema Shamba hilo lenye ukubwa wa hekta 3,000 limekaa kwa muda mrefu bila kufanyakazi.  "Tayari tumekamilisha suala la umiliki wake tunaomba Tume ihakikishe uzalishaji unaanza mapema ili kuwanufaisha wananchi wa maenoe yale na watanzania kwa ujumla," amesisitiza.  Mkurugenzi Mk...

Rais Samia Atangaza Kifo Cha David Cleopa Msuya

  Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha aliyewahi kuwa Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu,Cleopa David  Msuya kilichotokea majira ya saa tatu za asubuhi ya leo Jumatano,Mei saba Mwaka 2025 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar-es-salaam. Akitangaza Msiba huo kwa Taifa,Rais Samia amesema Mzee Msuya ameugua tatizo la moyo kwa kipindi kirefu na kupata matibabu ndani ya nchi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete,Mzena  pamoja na nchini Uingereza. “Natoa pole kwa familia,ndugu,jamaa na marafiki kwa msiba huu mkubwa kwa Taifa na natangaza siku saba za maombolezo kuanzia Julai saba hadi 13,2025 ambapo Bendera zitapepea nusu mlingoti”amesema Rais Samia Kwa mujibu wa Rais Samia,Taarifa zaidi kuhusu msiba huo zitaendelea kutolewa na serikali. Mzee Msuya amefikwa na Umauti akiwa na umri wa miaka 94.Alizaliwa Januari nne,1931 katika kijiji cha Chomvu Usangi,wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro