Skip to main content

Posts

Showing posts from August 13, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA ZABUNI ZILIZOTANGAZWA NA CAF KUELEKEA AFCON 2027

 DAR ES SALAAM, AGOSTI 14, 2026 Watanzania, kampuni, taasisi na watoa huduma wenye uwezo na sifa stahiki wamehimizwa kuchangamkia fursa mbalimbali za zabuni zilizotangazwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuelekea maandalizi na uendeshaji wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON2027). Akitoa taarifa hiyo leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa Kamati ya Ndani (LOC), Neema Msitha, amesema CAF imetangaza fursa mbalimbali za zabuni zinazohusiana na maandalizi na uendeshaji wa mashindano yake, ikiwamo AFCON 2027, ambayo Tanzania itaandaa kwa kushirikiana na Kenya na Uganda. “LOC inawahimiza Watanzania wenye uwezo, sifa na nia ya kushiriki fursa hizi kufuatilia matangazo rasmi ya zabuni hizo kupitia tovuti ya CAF ambayo ni https://www.cafonline.com/inside-caf/about-us/tenders/tenders-tab/ ili kusoma masharti ya kila zabuni na kuwasilisha maombi yao kufuatana na taratibu na muda uliowekwa na shirikisho hilo” amesisitiza Msitha. Amesema fursa hizo zinahusisha maeneo mbal...

MHE. BALOZI OMAR: AIMWAGIA SIFA TRA UKUSANYAJI WA MAPATO YA NDA

Na. Benny Mwaipaja, Kizimkazi, ZANZIBAR Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameimwagia sifa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA kwa utendaji uliotukuka uliowezesha Mamlaka hiyo kuendelea kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato kila mwezi na kueleza imani yake kwamba kwa kushirikiana na alipakodi, wataweza kuvuka lengo walilopangiwa la kukusanya zaidi ya shilingi trilioni 42 katika Mwaka wa Fedha 2026/2027. Mhe. Balozi Omar, ametoa pongezi hizo wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya TRA, Kizimkazi, Zanzibar, litakalokuwa na ghorofa moja, ambapo hadi kukamilika kwake linatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 3.6. Sifa hizo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, zinafuatia maelezo ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA Bw. Yusuph Mwenda ambapo alisema katika mwezi Julai mwaka huu, Mamlaka yake imevuka malengo kwa kukusanya shilingi trilioni 3.2 ikilinganishwa na malengo waliyopangiwa ya kukusanya shilingi trilioni 2. Alisema kuwa mafa...

MKUU WA JESHI LA MAGEREZA AKUTANA NA BALOZI WA CHINA 'WATETA' KUHUSU USHIRIKIANO

Na INSP. Nurdini Nanyanga - DSM Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP Jeremiah Yoram Katungu, leo Agosti 13, 2026, amefanya ziara katika Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China, jijini Dar Es Salaam na kukutana na Balozi wa nchi hiyo hapa Tanzania Mhe. Chen Mingjian. Katika ziara hiyo, CGP Katungu amesema lengo ni kuimarisha ushirikiano kati ya Jeshi la Magereza na China, hususan katika maeneo ya teknolojia na kilimo, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Jeshi la Magereza kuongeza uzalishaji na kujitosheleza kwa chakula. Amesema Jeshi la Magereza liko tayari kushirikiana na kampuni na wadau mbalimbali katika uwekezaji, kwa kuzingatia sheria, taratibu na maslahi ya pande zote. Kwa upande wake, Mhe. Chen Mingjian, amesema Tanzania na China zimekuwa na ushirikiano mzuri, huku kampuni nyingi za China zikionyesha nia ya kuwekeza nchini. Ameahidi kuyapa kipaumbele mazungumzo yao na kuendelea kubadilishana taarifa na Jeshi la Magereza ili kutafuta fursa za ushirikiano katika teknolojia na sekta ya kilimo.

KENYA: MAKAMANDA WA POLISI WATAWAJIBIKA BINAFSI KWA UHALIFU MAENEO YAO

INSPEKTA Jenerali wa Polisi Nchini Kenya, Douglas Kanja ametoa onyo kali kwa maafisa wa polisi na makamanda wao kwamba, watawajibishwa binafsi kwa uhalifu unaotokea katika maeneo yao iwapo uzembe wao au usimamizi hafifu utachangia matukio hayo. Akihutubia makamanda wakuu wa polisi kutoka sehemu mbalimbali za nchi katika Chuo cha Kitaifa cha Uongozi wa Polisi, Ngong,Kanja alisema viongozi wa polisi hawawezi tena kujitenga na vitendo vya uhalifu vinavyofanyika chini ya usimamizi wao. Alisema makamanda lazima wahakikishe wanatoa uongozi na usimamizi madhubuti kwa maafisa walio chini yao, akionya kuwa wale watakaoshindwa kuchukua hatua dhidi ya wahalifu wako hatarini kupoteza nyadhifa zao. “Kamanda yeyote katika ngazi yoyote atakayepatikana akivumilia uhuni au kushindwa kuchukua hatua madhubuti dhidi ya wahalifu atawajibishwa kwa kutotekeleza majukumu yake,” alisema Bw Kanja. Onyo hilo linajiri huku Huduma ya Kitaifa ya Polisi ikiendelea kujiandaa kwa kipindi cha shughuli za uchaguzi. Insp...

WAZAMBIA WAPIGA KURA, MAGEUZI YA KIUCHUMI YA RAIS HICHILEMA YAPIMWA

LUSAKA, Zambia.  Wazambia wamejitokeza kupiga kura leo, Alhamisi Agosti 13, 2026, katika uchaguzi mkuu unaoonekana kuwa mtihani mkubwa kwa Rais Hakainde Hichilema na mageuzi yake ya kiuchumi tangu alipoingia madarakani mwaka 2021.  Takribani wapiga kura milioni nane waliojiandikisha wameshiriki katika uchaguzi wa rais, wabunge na viongozi wa serikali za mitaa. Hichilema, ambaye anawania muhula wa pili, anaingia kwenye uchaguzi huo akijivunia hatua zilizochukuliwa kuimarisha uchumi, ikiwemo mchakato wa kurekebisha mzigo mkubwa wa deni la taifa na kuvutia uwekezaji, hususan katika sekta ya madini.  Hata hivyo, pamoja na baadhi ya viashiria vya uchumi kuimarika, gharama kubwa za maisha, ukosefu wa ajira na hali ya kipato cha wananchi bado ni miongoni mwa masuala yanayowasumbua wapiga kura. Zambia iliingia katika mzozo mkubwa wa madeni na kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kushindwa kulipa deni lake la nje katika kipindi cha janga la COVID-19. Serikali ya Hichilema imekuwa iki...

MKUU WA MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA RWANDA MBARONI

 KIGALI.  Taasisi ya Upelelezi nchini Rwanda (Rwanda Investigation Bureau (RIB) imemkamata Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini humo (FDA), Profesa Emile Bienvenu, pamoja na watuhumiwa wengine 17, wakiwemo maofisa 10 wa FDA. Watu hao wanakabiliwa na tuhuma zinazohusiana na uzalishaji, usambazaji na udhibiti wa vinywaji vya kilevi visivyokidhi viwango na vinavyodaiwa kuuzwa kinyume cha sheria. Hatua hiyo inakuja baada ya Rwanda kuendesha kampeni kubwa dhidi ya wazalishaji wa vileo wanaokiuka kanuni za usalama na afya ya umma. Katika operesheni hiyo, zaidi ya kampuni 140 zimefungiwa, huku mamia ya bidhaa za vileo zikiondolewa sokoni na baadhi ya bidhaa kutoka nje zikizuiwa au kuwekwa chini ya masharti maalumu. Miongoni mwa bidhaa zilizoingia kwenye hatua hizo ni baadhi ya bidhaa za vileo kutoka Uganda, zikiwemo Uganda Waragi, Bond 7, Gilbeys na V&A Sherry. Kwa mujibu wa wachunguzi, baadhi ya maofisa wanatuhumiwa kutumia vibaya madaraka yao kwa manufaa binafsi, huku weng...

MBUNGE MARY SURATI AKABIDHI MILIONI 10 UJENZI WA OFISI ZA CCM SERENGETI

MBUNGE wa Jimbo la Serengeti, Mhe. Mary Daniel Surati, amekabidhi shilingi milioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Serengeti, zinazojengwa Mugumu. Mhe. Surati amekabidhi fedha hizo leo, Alhamisi, Agosti 13, 2026, akieleza kuwa ujenzi wa ofisi bora utasaidia kuimarisha utendaji, uratibu na shughuli mbalimbali za Chama katika Wilaya ya Serengeti. Amesema hatua hiyo ni sehemu ya dhamira yake ya kuendelea kushirikiana na viongozi, wanachama pamoja na wadau mbalimbali katika kusukuma mbele juhudi za maendeleo ya Serengeti. Katika makabidhiano hayo, imeelezwa kuwa Maendeleo Magereza Mugumu watasimamia na kutekeleza ujenzi wa mradi huo hadi kukamilika. Mhe. Surati ametoa wito kwa viongozi, wanachama na wadau wa CCM kuendelea kushirikiana na kuunga mkono juhudi zinazolenga kuhakikisha ujenzi wa ofisi hizo unakamilika kwa wakati. “Ninaendelea kusimamia kwa vitendo dhamira yangu ya kushirikiana na wananchi na taasisi mbalimbali katika kuleta maendeleo ya Se...

PROF. MKENDA: VETA ITOE UJUZI UNAOKIDHI MAHITAJI YA SOKO LA AJIRA

 WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amezitaka Kamati za Ushauri wa Stadi (Training Advisory Committees–TACs) za Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kuwa chachu ya kuhakikisha mafunzo yanayotolewa yanaendana na mahitaji halisi ya soko la ajira na uzalishaji nchini. Prof. Mkenda amesema kamati hizo zinapaswa kuwa kiungo madhubuti kati ya VETA, Serikali, waajiri na sekta binafsi, ili kuhakikisha vijana wanaohitimu wanakuwa na ujuzi, umahiri, ubunifu na uwezo wa kutumia teknolojia unaohitajika katika maeneo ya kazi. Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda Ameyasema hayo leo, Agosti 13, 2026, jijini Dodoma, wakati akizindua rasmi Kamati za Ushauri wa Stadi za VETA, ambapo amesisitiza kuwa mfumo wa mafunzo ya ufundi stadi haupaswi kuishia katika kutoa vyeti pekee, bali unapaswa kuwaandaa wahitimu kwa ajira, kujiajiri na kuanzisha shughuli za uzalishaji. “Hatupaswi kuwa na mfumo wa mafunzo unaoishia katika kutoa vyeti pekee. Tunataka...

MBUNGE SURATI AAMBATANA NA WAZIRI BASHIRU KUFUATILIA MAENDELEO JIMBO LA SERENGETI

 MBUNGE wa Jimbo la Serengeti, Mhe. Mary Daniel Surati ameambatana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, katika ziara ya kikazi wilayani Serengeti, iliyolenga kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kusikiliza changamoto za wananchi na kuweka mikakati ya kuboresha huduma muhimu katika jimbo hilo. Katika ziara hiyo, Waziri Dkt. Bashiru amekutana na kufanya kikao na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Serengeti, ambapo masuala mbalimbali ya maendeleo na changamoto zinazowakabili wananchi yalijadiliwa. Ziara hiyo pia ilimfikisha Waziri katika Kata ya Matare, ambako alizindua vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Igina, hatua inayotarajiwa kuimarisha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa wanafunzi wa shule hiyo. Mbunge Mary amesema kushiriki kwake katika ziara hiyo ni sehemu ya kuendelea kusimamia kwa karibu masuala ya maendeleo ya wananchi wa Serengeti, akieleza kuwa uwepo wa viongozi katika maeneo ya wananchi unasaidia kupata ...

ZIARA YA RAIS SAMIA URUSI YAZIDI KUZAA MATUNDA, WANAFUNZI 10 WAPATA UFADHILI WA KUSOMA MOSCOW

 Ziara Rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, nchini Urusi imeendelea kuzaa matunda katika sekta ya elimu, baada ya wanafunzi 10 waliofanya vizuri katika masomo ya sayansi kupata ufadhili wa masomo katika Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi (RUDN University) kilichopo jijini Moscow. Wanafunzi hao waliomaliza kidato cha sita na kufanya vizuri katika tahasusi za PCM, PGM na PMC, wamepata fursa hiyo kupitia mpango wa Samia Scholarship Extended, ikiwa ni sehemu ya matokeo ya ziara ya Rais Samia nchini Urusi iliyofanyika mwezi Juni 2026. Rais Samia alifanya ziara hiyo nchini Urusi na kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) na RUDN University, moja ya vyuo vikuu vinavyotambulika nchini humo. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo, Agosti 13, 2026, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, amesema wanafunzi hao wamechaguliwa kutokana na kufanya vizuri kitaaluma, wakifuata kundi ...

PROF. MKENDA: VETA ITOE UJUZI UNAOKIDHI MAHITAJI YA SOKO LA AJIRA

 WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amezitaka Kamati za Ushauri wa Stadi (Training Advisory Committees–TACs) za Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kuwa chachu ya kuhakikisha mafunzo yanayotolewa yanaendana na mahitaji halisi ya soko la ajira na uzalishaji nchini. Prof. Mkenda amesema kamati hizo zinapaswa kuwa kiungo madhubuti kati ya VETA, Serikali, waajiri na sekta binafsi, ili kuhakikisha vijana wanaohitimu wanakuwa na ujuzi, umahiri, ubunifu na uwezo wa kutumia teknolojia unaohitajika katika maeneo ya kazi. Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda Ameyasema hayo leo, Agosti 13, 2026, jijini Dodoma, wakati akizindua rasmi Kamati za Ushauri wa Stadi za VETA, ambapo amesisitiza kuwa mfumo wa mafunzo ya ufundi stadi haupaswi kuishia katika kutoa vyeti pekee, bali unapaswa kuwaandaa wahitimu kwa ajira, kujiajiri na kuanzisha shughuli za uzalishaji. “Hatupaswi kuwa na mfumo wa mafunzo unaoishia katika kutoa vyeti pekee. Tunataka...

UGANDA KUHAMISHA WIZARA NA TAASISI ZA SERIKALI KUTOKA KAMPALA

  KAMPALA, Uganda   Serikali ya Uganda imepanga kuanza kuhamisha kwa awamu wizara, idara na taasisi zake kutoka Kampala kwenda Nakasongola , katika mpango wa muda mrefu ambao unaweza kuendelea hadi mwaka 2040 . Mpango huo umetangazwa na Waziri wa Nchi wa Maendeleo ya Miji, Margaret Muhanga , mbele ya Kamati ya Ardhi na Nyumba ya Bunge la Uganda. Muhanga amesema Rais Yoweri Museveni anaunga mkono mpango huo, ambao Serikali inautazama kama sehemu ya utekelezaji wa maono ya maendeleo ya Uganda kuelekea mwaka 2040. KAMPALA YAWA CHANGAMOTO Serikali imesema msongamano mkubwa wa magari na changamoto za upangaji wa mji zimefanya Kampala kuwa na mazingira magumu kwa watu kuishi na kufanya kazi. Muhanga amesema Uganda inapoteza takribani dola bilioni 1.6 kwa mwaka kutokana na foleni za magari, huku baadhi ya wakazi wakilazimika kuamka saa 10 alfajiri (4:00 asubuhi) ili waweze kufika kazini saa 2 asubuhi (8:00) . “Kampala haiwezi kuishiwa, haiwezi kubadilishwa, haiwezi kuendelez...

MBUNGE NSEKELA AHAIDI KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI KIMULI

   Na Angela Sebastian ;Kyerwa Mbunge wa Kyerwa, Khalid Nsekela, ameahidi kushirikiana na Halmashauri pamoja na wadau wa elimu kutatua changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama katika Shule ya Sekondari Kimuli, ili kuwawezesha wanafunzi kutumia muda mwingi kujisomea badala ya kutembea hadi saa nne kufuata maji. Ahadi hiyo imekuja wakati wa afla ya utoaji tuzo kwa walimu na shule zilizofanya vizuri katika mitihani ya Taifa ya kidato cha sita 2026, licha ya shule hiyo kufanya vizuri kitaaluma, ambapo katika matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2026 ilishika nafasi ya kwanza wilayani,ya kwanza kwa shule za Serikali kimkoa na ya pili kimkoa kwa shule zote. Kimuli inakabiliwa pia na changamoto ya ukosefu wa ofisi za walimu na mabweni, hali inayowalazimu baadhi ya wanafunzi kulala katika vyumba vya madarasa visivyo na madirisha lakini wanafanya vizuri katika masomo yao. Kwa niaba ya Mbunge, Nekmia Nguma Katibu wa Mbunge-Kitengo cha Mahusiano, amesema Nsekela amewapongeza wanafunzi na...

MBUNGE NSEKELA AHAIDI KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI KIMULI

 Na Angela Sebastian ;Kyerwa Mbunge wa Kyerwa, Khalid Nsekela, ameahidi kushirikiana na Halmashauri pamoja na wadau wa elimu kutatua changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama katika Shule ya Sekondari Kimuli, ili kuwawezesha wanafunzi kutumia muda mwingi kujisomea badala ya kutembea hadi saa nne kufuata maji. Ahadi hiyo imekuja wakati wa afla ya utoaji tuzo kwa walimu na shule zilizofanya vizuri katika mitihani ya Taifa ya kidato cha sita 2026, licha ya shule hiyo kufanya vizuri kitaaluma, ambapo katika matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2026 ilishika nafasi ya kwanza wilayani,ya kwanza kwa shule za Serikali kimkoa na ya pili kimkoa kwa shule zote. Kimuli inakabiliwa pia na changamoto ya ukosefu wa ofisi za walimu na mabweni, hali inayowalazimu baadhi ya wanafunzi kulala katika vyumba vya madarasa visivyo na madirisha lakini wanafanya vizuri katika masomo yao. Kwa niaba ya Mbunge, Nekmia Nguma Katibu wa Mbunge-Kitengo cha Mahusiano, amesema Nsekela amewapongeza wanafun...

NAIBU WAZIRI MAKAMBA AITAKA PBPA KUENDELEA KUTOA ELIMU KWA UMMA

 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba (Mb.), ameitaka Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) kuendelea kuimarisha utoaji wa elimu kwa umma ili wananchi wawe na uelewa mpana kuhusu majukumu ya Wakala na mchango wake katika kuhakikisha upatikanaji wa mafuta nchini. Mhe. Makamba ametoa wito huo alipotembelea banda la PBPA katika maonesho yanayofanyika Viwanja vya Dimbani, Kizimkazi, Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya Tamasha la Kizimkazi 2026. Amesema ni muhimu wananchi wakaendelea kuelimishwa kuhusu Mfumo wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja na namna PBPA inavyotekeleza majukumu yake katika kusimamia uagizaji wa bidhaa za mafuta kwa lengo la kuhakikisha nchi inakuwa na uhakika wa upatikanaji wa bidhaa hiyo muhimu. Aidha, Mhe. Makamba ameipongeza PBPA kwa utendaji wake katika kutekeleza majukumu yake na kuhakikisha upatikanaji wa mafuta nchini. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkaguzi wa Mafuta wa PBPA, Bw. Issa Mwitazy, amemweleza Naibu Waziri kuwa Wakala unaendelea kutekeleza majuk...