NA: MWANDISHI WETU Rai imetolewa kwa wadau mbalimbali kujitoa kwa hali na mali kuchangia fedha kwa ajili ya mfuko unaohudumia wagonjwa wa figo na upandikizaji uloto kwa watoto wenye selimundu (sickle cell) wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma. Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti Taifa wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda, Julai 13, 2026, jijini Dodoma. Chatanda amesema, kutokana na gharama kubwa za matibabu ya magonjwa hayo, viongozi, taasisi binafsi, asasi za kiraia na wananchi kwa ujumla hawana budi kuunganisha nguvu ya pamoja, kuwezesha upatikanaji wa shilingi bilioni saba, ili wagonjwa wasio na uwezo, waweze kunufaika na mfuko huo na hatimaye kuokoa maisha yao. "Wenzetu Hospitali ya Benjamin Mkapa, wamekuja na mpango kabambe wa kukusanya shilingi bilioni saba za kugharamia wagonjwa wa figo na selimundu, na UWT tuliposhirikishwa tuliona ni jambo jema kwani linagusa uhai wa watu, hivyo basi, niwaombe wadau na wananchi kwa uju...
Marato tv - Sauti ya Jamii