Skip to main content

Posts

Showing posts from July 21, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

RAIS DKT. MWINYI: SMZ ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA UN WOMEN KUWAWEZESHA WANAWAKE ZANZIBAR

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na UN Women katika kukuza usawa wa kijinsia, kuwawezesha wanawake kiuchumi na kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na wasichana. Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 22 Julai 2026, Ikulu Zanzibar, alipokutana na Mwakilishi mpya wa UN Women nchini Tanzania, Bi. Julia Broussard, aliyefika kujitambulisha rasmi baada ya kuanza majukumu yake. Katika mazungumzo hayo, Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza kuimarishwa kwa ushirikiano katika maendeleo ya sekta ya mwani, matumizi ya takwimu za kijinsia, bajeti zinazozingatia usawa wa kijinsia na kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi. Kwa upande wake, Bi. Julia Broussard ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa hatua zinazochukua katika kukuza usawa wa kijinsia na kuahidi kuwa UN Women itaendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali katika kuwawezesha wanawake na kuboresha u...

RAIS SAMIA AWASILI GHANA KUSHIRIKI MKUTANO MAALUM WA UMOJA WA AFRIKA KUHUSU AFYA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Accra nchini Ghana leo Julai 21, 2026 kwa ajili ya kushiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) kuhusu Afya. Mara baada ya kuwasili, Rais Samia alipokea heshima ya wimbo wa Taifa wa Tanzania kabla ya kukagua gwaride rasmi la heshima lililoandaliwa kumkaribisha, ikiwa ni sehemu ya mapokezi ya viongozi wa nchi na serikali wanaoshiriki mkutano huo muhimu unaolenga kujadili masuala ya afya barani Afrika na kuimarisha ushirikiano wa nchi wanachama katika sekta hiyo.

TANZANIA NA OACPS WAKUBALIANA KUINUA SEKTA YA UVUVI NA UCHUMI WA BULUU KWA MANUFAA YA WANANCHI WA NCHI WANACHAMA

 Tanzania na Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS) wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika kuendeleza sekta ya uvuvi na uchumi wa buluu ili kuongeza mchango wake katika ukuaji wa uchumi, usalama wa chakula, ajira na ustawi wa wananchi wa nchi wanachama. Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa kikao kati ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (Mb.), na Katibu Mkuu wa OACPS, Mhe. Moussa Saleh Batraki, kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, jijini Dar es Salaam, tarehe 21 Julai 2026. Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Kakurwa amesema Tanzania inathamini juhudi za OACPS za kuendelea kuitambua sekta ya uvuvi na uchumi wa buluu kama eneo la kimkakati la maendeleo. Akiipongeza Jumuiya hiyo kwa mipango mbalimbali inayolenga kuimarisha sekta hiyo, ikiwemo programu ya FISH4ACP ambayo imechangia kuendeleza mnyororo wa thamani wa uvuvi nchini.  Aidha, Waziri Kakurwa amesema kuna umuhimu w...

WIZARA YA MALIASILI NA TAASISI ZAKE ZAJIPANGA UJIO WA MAONESHO YA NANENANE

 ðŸ“ŒKamati ya kitaifa yakutana kwa ajili ya maandalizi na kutoa mwelekeo wa ushirikiano wa Wizara 📌Maliasili yajipanga kuleta wanyama hai na kutangaza vivutio vya Utalii Dodoma  📌Taasisi zajipanga kutoa huduma bora kwa wananchi Na Neema Chalila Mbuja, Dodoma KAMATI ya kitaifa ya Kuratibu maandalizi ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) kwa Wizara ya Maliasili na Utalii na taasisi zake imekutana leo Julai 21,2026 Jijini Dodoma na kuazimia kutoa huduma bora kwa wananchi ili watambue kazi na majukumu ya Wizara na taasisi zake. Akizungumza na kutoa maelekezo ya namna ya kuboresha ushiriki wa Wizara ya Maliasili na Utalii na taasisi zake kwenye maonesho ya nanenane, Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Utalii, Richard Wandwi amesema, ushiriki wa Wizara kwa mwaka huu unapaswa kuwa wa kiubunifu na kutangaza maeneo ya vivutio vya utalii kwa Mkoa wa Dodoma kama ilivyoainishwa kwenye mkakati wa uendelezaji utalii kwa mkoa wa Dodoma uliozinduliwa na Waziri Mkuu, Mhe Dkt Mwigulu Nchemba. ‘’ Naomb...

RAIS SAMIA AONDOKA NCHINI KUELEKEA NCHINI GHANA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiondoka nchini kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam tarehe 21 Julai, 2026 kuelekea Accra, Ghana ambapo atashiriki katika Mkutano Mkuu Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) kuhusu afya, utakaofanyika tarehe 22 Julai, 2026 jijini Accra.

MAPINDUZI YA UMWAGILIAJI: SERIKALI YASAMBAZA PAMPU 2,000, YACHIMBA VISIMA 390 KUINUA KILIMO

Njedengwa, Dodoma Serikali imeongeza kasi ya mapinduzi ya sekta ya kilimo kwa kuanza kusambaza pampu za umwagiliaji na kuchimba visima 390 katika mikoa 15, hatua inayolenga kuwawezesha wakulima kulima mwaka mzima, kuongeza uzalishaji wa mazao na kuimarisha usalama wa chakula nchini. Mpango huo unatarajiwa kunufaisha wakulima 15,022 waliounganishwa katika vikundi 769, huku ekari 13,518.75 zikiingizwa kwenye kilimo cha umwagiliaji ili kupunguza utegemezi wa mvua. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Raymond Mndolwa, alisema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuwainua wakulima wadogo, hususan wanawake na vijana, kwa kuwapatia uhakika wa maji kwa ajili ya uzalishaji. Alisema pamoja na kuendelea na ujenzi wa miradi mikubwa na ya kimkakati ya umwagiliaji, Serikali imeamua kuwekeza pia katika uchimbaji wa visima na usambazaji wa pampu kwa vikundi vya wakulima ili kuongeza tija mashambani. "Tumeelekezwa kutaf...