Skip to main content

Posts

Showing posts from May 29, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

TANZANIA YAUNGA MKONO UBUNIFU MPYA KIFEDHA KWA AJILI YA MITADI YA USAFIRI NA AFYA

Na Benny Mwaipaja, Congo Brazzaville Tanzania imeelezea msimamo wake wa kuunga mkono mbinu za fedha za mseto (blended finance) zitakazosaidia kuimarisha sekta za usafiri wa anga na afya barani Afrika, akieleza kwamba hakuna chanzo kimoja kitakachoweza kuziba mapungufu ya miundombinu ya bara hilo. Akizungumza kama Gavana Mbadala wa Tanzania kwenye mkutano ulioandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuhusu “Platform solutions to Africa’s Transformation: De‑risking Aviation and Health systems through Innovative Financing”, jijini Congo Brazzaville, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba alisema suluhisho linalopendekezwa ni la vitendo, nafuu na linaendana na vipaumbele vya kitaifa vya Tanzania. “Tunasisitiza matumizi ya rasilimali za umma na binafsi pamoja na dhamana na msaada kutoka kwa washirika. Hatuwezi kutegemea chanzo kimoja pekee,” alisema Dkt. Mwamba, akiongeza kuwa ni muhimu kuzingatia udhibiti wa deni linalozidi kukua katika n...

UWEPO WA MADUKA YA NYARA HAPA NCHINI UTAIMARISHA USIMAMIZI MADHUBUTI

Na Mwandishi wetu Jovina Massano. Uimarishaji uhifadhi unazidi kuboreshwa na Serikali ya awamu ya sita kwa kuweza kuanzisha maduka maalum ya kuuza nyara na kuweka historia mpya  tangu Uhuru. Uanzishwaji huo umechukuliwa mara baada ya Machifu kutoka makabila mbalimbali nchini kuiomba Serikali kuwezesha upatikanaji wa nyara kwa makundi yanayohitaji kuzitumia katika mila na desturi. Maombi hayo yaliwasilishwa kwa Mh.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan jijini Mwanza wakati wa tamasha la Bulabo ambalo hufanyika kila Mwaka linalokutanisha Viongozi wa mila na desturi kwa maana ya machifu kutoka mikoa mbalimbali. Katika tamasha hilo waliweza kumsimika Mh.Rais wa awamu ya sita kuwa   Chifu mkuu  na mmiliki wa mila na desturi zilizo njema huku wakimpa jina la Chifu Hangaya. Chifu Hangaya hakusita kuchukua hatua madhubuti kwa kuanzisha maduka hayo  kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) katika mikoa ya Mwanza na Arusha. Umuhimu wa maduka haya yatawezesha usi...

KUIMARISHWA KWA MIFUMO YA USIMAMIZI WA MAAFA TANZANIA KWATOA SOMO MAPAI MSUMBIJI

Na, Mwandishi wetu, Mapai - Msumbiji TANZANIA imeendelea kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha udhibiti wa maafa unaanzia ngazi ya chini ya jamii, hatua inayolenga kuongeza ufanisi katika tahadhari, maandalizi na mwitikio wa haraka pindi majanga yanapotokea. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Brigedia Jenerali Hosea Ndagala, walipotembelea Wilaya ya Mapai iliyoko mkoa wa Gaza Nchini Msumbiji ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kubadilishana uzoefu kati ya Tanzania na Msumbiji kuhusu hatua za mapema za kukabiliana na majanga. Amesema moja ya mambo makubwa yakujivunia ni namna mifumo ya usimamizi wa maafa ilivyoimarika kuanzia ngazi ya chini jambo linalosaidia kuongeza ufanisi na mwitikio wa haraka pindi majanga yanapotokea. Aidha, akieleza faida ya ziara hiyo Wilayani Mapai ni kuchukua uzoefu wa namna ya kuongeza tija katika eneo la kurejesha hali na kukabiliana na maafa kwa kuwa na miradi ya k...

RAIS SAMIA APONGEZWA KWA KUKUZA MICHEZO NCHINI

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Esther Bulaya, ameungwa mkono bungeni kutokana na hoja nzito aliyowasilisha huku wabunge wakitoa pongezi kwa timu ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 17  (Serengeti Boys) kwa historia waliyoandika usiku wa kuamkia leo Kwa kufuzu Fainali za AFCON 2026 na kukata Tiketi ya kushiriki Mashindano ya Kombe la Dunia la Vijana chini ya umri wa Miaka 17 Mwaka 2026. Azimio hilo liliwasilishwa na Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Mhe. Esther Bulaya wakati wa Kikao cha 39 cha Mkutano wa 3 wa Bunge la 13, leo Mei 29, 2026 Jijini, Dodoma. Akitoa pongezi kwa kumpongeza  Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake binafsi katika kukuza michezo nchini na kuendeleza vipaji vya watoto wa Kitanzania, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda amesema hatua hizo zimeifanya Tanzania kuendelea kutambulika kimataifa kupitia mafanikio ya michezo. Amesema uwekezaji mkubwa unaofanywa na Rais Samia katika sekta ya michezo ni matokeo ya maono na mapenzi ...

JK AKUTANA NA BI. CATHERINE P. CONRAD MINJA

  NI MSICHANA ALIYEFANYIWA UPASUAJI WA MOYO KWA MAFANIKIO KATIKA TAASISI YA MIFUPA YA MUHIMBILI (MOI) MIAKA 18 ILIYOPITA  Asubuhi ya Ijumaa, Novemba 14, 2008 Rais wa Awamu ya Nne wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, alisimama kwa muda kando ya kitanda cha binti mdogo Catherine P. Conrdad Minja mwenye umri wa miaka minne katika Taasisi ya Mifupa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MOI), akimsabahi na kumtakia nafuu ya haraka baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo mapema wiki hiyo, akiwa mmoja wa wagonjwa wa mwanzo kufanyiwa upasuaji huo katika Taasisi hiyo. Jioni ya Ijumaa Mei 29, 2026  - yaani leo - Rais huyo mstaafu wa Awamu ya Nne wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekutana kwa mara nyingine na Catherine P. Conrad Minja ambaye Julai 19 mwaka huu atatimiza umri wa miaka 22 , ikiwa ni miaka 18 toka walipoonana katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo mapema wiki hiyo. Catherine hivi sasa ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanz...

UNODC REAFFIRMS COMMITMENT TO STRENGTHENING TANZANIA MARITIME SECURITY

  From: Mwanza Police Information Desk The ongoing partnership between the United Nations Office on Drugs and Crime (UNODC) and the Tanzania Marine Police is yielding significant success in the fight against maritime crimes, a top official has said. ​Andres Reyes, a UNODC instructor from Colombia, made the remarks on May 29, 2026, in Mwanza City during the closing ceremony of a rigorous four-week training program on "Maritime Boarding, Search, and Seizure Operations" for marine police officers. ​Reyes noted that the month-long training was specifically designed to sharpen the officers' skills and boost their capacity to tackle various maritime threats, including smuggling, illegal fishing, illicit arms trafficking, and other transnational crimes across the country's waters. ​Throughout the training, participants engaged in both theoretical and practical sessions designed to enhance their professionalism and ensure the robust security of the nation's water borders....

PROF. KABUDI:TANI 29.52 ZA DAWA MPYA YA KULEVYA AINA YA KRATOM ILIKAMATWA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Profesa Palamagamba Kabudi, amesema Serikali imeendelea kupata mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kupitia operesheni maalumu za ufuatiliaji na udhibiti nchini. Akiwasilisha taarifa kuhusu hali ya dawa za kulevya kwa waandishi wa habari leoei 29,2026 jijini Dodoma, Profesa Kabudi amesema mwaka 2025 jumla ya tani 26.36 za mirungi zilikamatwa, ikiwa ni ongezeko la asilimia 42.88 ikilinganishwa na mwaka 2024. Amesema ongezeko hilo linaonyesha kuimarika kwa ufanisi wa operesheni za ufuatiliaji na udhibiti, hususan katika maeneo ya mipaka na njia zinazotumika kusafirisha dawa hizo nchini. Kwa upande wa dawa za kulevya za viwandani, Profesa Kabudi amesema Serikali ilikamata kilogramu 907.18 za methamphetamine, kilogramu 672.23 za heroin, kilogramu 4.89 za cocaine, pamoja na gramu 178 za MDMA na gramu 7.82 za MDA. Aidha, amebainisha kuwa kwa mara ya kwanza mwaka 2025, Serikali ...

SERIKALI YAZIDISHA MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA, YATIBU ZAIDI YA WATU 85,000

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Profesa Palamagamba Kabudi, amesema Serikali imeendelea kuimarisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini kwa kuhakikisha waathirika wanapata huduma za tiba na marekebisho ya tabia. Profesa Kabudi ameyasema hayo leo Mei 29,2026 Bungeni jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa ya hali ya dawa za kulevya kwa mwaka 2025. Amesema katika mwaka huo, jumla ya watu 85,425 wenye uraibu wa dawa za kulevya walipatiwa huduma za tiba kupitia vitengo vya afya ya akili vilivyopo katika hospitali za rufaa za mikoa na kanda, kliniki za MAT pamoja na nyumba za upataji nafuu nchini. Ameeleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa Serikali kuhakikisha waathirika wanapata huduma stahiki zinazowasaidia kurejea katika maisha ya kawaida na kuwa sehemu ya kuchangia maendeleo ya taifa. Aidha, Profesa Kabudi amesema Serikali pia imeendelea kuimarisha elimu kwa umma kuhusu madhara ya dawa...

SERIKALI YASISITIZA KUHARAKISHWA UJENZI WA OFISI ZA MIKOA ILI KUONGEZA NGUVU ZA UDHIBITI DAWA ZA KULEVYA

 SERIKALI imesisitiza kuharakishwa kwa ujenzi na uanzishwaji wa ofisi za Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya katika mikoa yote inayotajwa kuwa njia kuu za mapito ya dawa za kulevya, ili kuongeza kasi ya udhibiti na kuimarisha mapambano dhidi ya biashara hiyo haramu. Akizungumza leo Mei 29,2026 Jijini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa kuhusu hali ya dawa za kulevya nchini, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Palamagamba Kabudi amesema ni muhimu kuharakisha ujenzi na uanzishwaji wa ofisi katika mikoa yote inayotumika kama njia za mapito ya dawa za kulevya ili kuongeza ufanisi wa udhibiti na operesheni. Amesema kuwa ujenzi wa ofisi hizo lazima uendane na kuimarishwa kwa uwezo wa kiutendaji wa mamlaka hiyo. “Tumeamua pia kuimarisha uwezo wa kiutendaji ikiwemo kununua magari 17 yatakayosaidia kuongeza nguvu za operesheni za udhibiti, ufuatiliaji na ukamataji wa mitandao ya dawa za kulevya,” amesema. Prof. Kabudi ...

MAKAMU WA RAIS AONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA MAREHEMU BI SUZANA MAGUFULI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mazishi ya Marehemu Bi. Suzana Ngolo Magufuli, ambaye ni Mama wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, yaliyofanyika Kilimani, Chato mkoani Geita. Akitoa salamu za rambirambi mara baada ya kumalizika kwa Ibada ya kumuombea Marehemu Bi. Suzana Ngolo Magufuli, Makamu wa Rais amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameguswa na msiba huo na anatoa salamu za pole kwa familia, ndugu jamaa na marafiki na wote walioguswa na msiba huo. Makamu wa Rais amewasihi Watanzania kumtumia marehemu Bi. Suzana Ngolo Magufuli kama kielelezo cha malezi ya watoto, malezi ya maadili na uzalendo kwa kuwafanya watoto kutanguliza maslahi ya Taifa mbele na kuwa tayari kutumikia Taifa kwa nafasi yeyote wanayopewa. Ameongeza kwamba namna bora ya kumuenzi marehemu Bi. Suzana Ngolo Mag...