Skip to main content

Posts

Showing posts from September 5, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt Nchimbi "Utafiti Maeneo ya Madini Kuongezeka Kwa 50%"

Mgombea mwenza wa kiti cha Urais kupitia Chama Cha Mapindizi (CCM).  Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi amesema Serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan, endapo kama Itaingia Madarakani kwa mara nyingine itahakikisha inatenga maeneo mengine ya kutosha kwa ajili ya Wachimbaji Wadogo, ikiwa ni pamoja na kuongeza kiwango cha Utafiti kwenye maeneo ya Madini kutoka asilimia 16 hadi asilimia 50. Dkt Nchimbi ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Septemba 05, 2025 akiwa mkoani Geita katika Wilaya za Mbogwe na Nyang'hwale, ikiwa ni muendelezo wa Mikutano ya Kampeni za Urais Kupitia CCM kuelekea Uchaguzi mkuu wa Oktoba 29. "Ninachotaka kusema hapa ni kwamba Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya 2025/2030 imedhamiria kuongeza tija kwenye Sekta ya Madini, kwa kutenga maeneo ya Wachimbaji madini wadogo, vile vile Serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan inakusudia pia kuongeza kiwango cha Utafiti wa Madini kutoka asilimia 16 hadi kufikia asilimia 50" amesema Dkt Nchimbi. Dkt Emmanuel John Nchi...

Tanzania Imejengwa Kwa Misingi Imara ya Amani na Uzalendo-Majaliwa

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Tanzania imejengwa kwa misingi imara ya amani, uzalendo na maadili mema ambayo yameasisiwa na viongozi wa Taifa hilo. Amesema kuwa wakati wote viongozi wa dini wamekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Serikali kuhamasisha amani, kukemea uovu na utovu wa nidhamu katika jamii ili kujenga kizazi chenye heshima, mshikamano na uzalendo kwa Taifa. Amesema hayo leo Ijumaa (Septemba 05, 2025) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika baraza la Maulid Kitaifa lililofanyika Wilayani Korogwe mkoani mkoani Tanga Amesema kuwa Maulid ni tukio lililobeba mwongozo wa kiroho kwa wanadamu wote. “Maisha ya Mtume yanaonesha mfano na yanatufundisha kuwa waadilifu, kuishi kwa maadili, na kumtegemea Mwenyezi Mungu. katika kila jambo”. Amesema Waziri Mkuu. Kwa upande wake Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir bin Ali ametoa wito kwa Masheikh nchini kuendelea kuhubiri amani katika maeneo yao kwa kuwa amani si jambo la hiari hivy...

Dkt.Samia Aendelea Kuomba Kura Mkoani Mbeya

 Mgombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi na wanachama wa CCM wa Marali mkoani Mbeya katika muendelezo wa kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama hicho tarehe 05 Septemba 2025.

Nchimbi Atinga Geita,Apokewa Kwa Kishindo Mbogwe

Mgombea Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi  akiwahutubia Wananchi wa kata ya Masumbwe,katika Viwanja vya Shule ya Msingi  Masumbwe, leo Ijumaa Septemba 5,2025 Wilayani Mbogwe, Mkoa wa Geita . Dkt Nchimbi ameingia mkoani Geita leo kuendelea na Mikutano yake ya Kampeni ya kusaka kura za ushindi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),akitokea mkoani Shinyanga. Pamoja na mambo mengine Dkt Nchimbi pia aliwanadi wagombea Ubunge,akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbongwe,Fagasoni Aron Nkingwa pamoja na Madiwani. Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi anaendelea na mikutano yake ya Kampeni Mkoani Geita ya kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030, ambayo inalenga kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM, Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.