Na Mwandishi wetu Jovina Massano Musoma Mwitikio mzuri wa wazazi na walezi kwa kushiriki na kuhakikisha watoto wanapata chanjo ya Polio yapaisha lengo watoto 222,076 Wilaya ya Musoma mkoani Mara wafikiwa. Wilaya mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amewapongeza wazazi na walezi kwa kushiriki kikamilifu katika zoezi la utoaji Chanjo kwa watoto. Amesema katika halmashauri ya Manispaa ya Musoma idadi tarajiwa ilikuwa ni Walengwa 66,176 kutokana na mwitikio mkubwa imepelekea waliopata chanjo hiyo kufikia 77,104 sawa na 120% huku halmashauri ya Musoma Vijijini walengwa walikuwa ni 118,760 na kufikia waliochanjwa 144,972 sawa na 157%. Nae Mratibu wa Halmashauri ya Musoma DC Joseph Chacha amesema zoezi hilo limefanyika vizuri kutokana na elimu na hamasa iliyotolewa kwa wakati kwa jamii kupitia wenyeviti wa mitaa,vitongoji na vijiji na makundi mbalimbali ya kijamii. "Ushirikiano katika ngazi zote umeleta matokeo na mwitikio mkubwa kwa jamii na kupata Idadi kubwa ya watoto kupata...
Marato tv - Sauti ya Jamii