Skip to main content

Posts

Showing posts from February 11, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tanzania Yahakikisha Usalama Wa Chakula Comoro

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Visiwa  vya Comoro Mheshimiwa Saidi Yakubu,februari 11 Mwaka huu amekutana na kufanya Mazungumzo na Ujumbe maalumu kutoka Serikali ya Comoro unaoshughulikia azma ya nchi hiyo kuimarisha biashara ya bidhaa za chakula.  Ujumbe huo uliongozwa na Bw. Snehal SONEJI, Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa nchini Comoro.  Washiriki wengine kwenye Mazungumzo hayo ni Dkt. Hamza A. Azali, Mamlaka ya Utafiti wa Kilimo, Mazingira na Uvuvi (INRAPE), na Bw. Abdillahi M'Saidie, Rais wa Jumuiya ya Wafugaji, Wakulima, Wavuvi na Sanaa nchini Comoro. Ujumbe kutoka Serikali ya Comoro ulijulisha kuwa ulitembelea Tanzania wiki ya kwanza ya mwezi Februari, 2025 ambapo walibahatika kukutana na kufanya mazungumzo na watendaji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kukutana na Ushirika wa Uzalishaji katika Chuo cha Kilimo cha SOKOINE, pamoja na kutembelea miradi ya kilimo.  Kufuatia mazungumzo yao, Taasisi za Tanzania zimeon...

Tra Mkoa Wa Kagera Yaadhimisha Wiki Ya Mlipa Kodi Kwa Kutoa Misaada Kwa Watoto Yatima

 Na Angela Sebastian ;Bukoba MAMLAKA ya mapato Tanzania( TRA) mkoani Kagera imeadhimisha wiki ya shukrani kwa mlipa kodi kwa kutoa misaada ya vitu  mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni tano kwa watoto yatima na wasiojiweza katika kituo cha watoto Yatima cha Uyacho kilichopo Manispaa ya Bukoba mkoani humo. Meneja wa TRA mkoani Kagera Castor John amesema wametoa vitu hivyo kwa watoto hao vyenye thamani ya shilingi  ikiwa ni kurudisha shukrani kwa mlipa kodi wakiamini kuwa watoto hao ni wadau pia wanamchango mkubwa katika ulipaji wa kodi kupitia huduma wanazopatiwa ikiwemo za manunuzi ya vitu mbalimbali. Maadhimisho hayo kwa kufanya matembezi  yaliyoanzia katika ofisi za TRA mkoa huo na kupita mitaa mbalimbali ya Manispaa ya Bukoba kwa kujumuisha wadau wa mamlaka hiyo waliobeba mabango yenye ujumbe wa   kuhamasisha ulipaji kodi kwa hiari na shukrani kwa mlipa kodi. Misaada iliyotolewa ni pamoja na mchele, sukari, unga, maharage, mafuta ya kula, unga w...

Wenye Viwanda wakaa na Waziri kutatua kero ya tozo ya Sh 150,000 kupakia kontena

Na Mwandishi Wetu  WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Seleman Jafo amesema ndani ya siku 60 Wizara yake itakuwa imepata ufumbuzi wa malalamiko ya wawekezaju kuhusu tozo ya shilingi 150,000 wanayotozwa kwaajili ya kushusha na kupakia kontena. Alitoa ahadi hiyo jana mara baada ya mkutano baina yake na wanachama wa Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI), ambao wamekuwa wakilalamikia kutozwa shilingi 150,000 kwa kontena linaloshushwa na kupakiwa kwenye halmashauri hizo kutoka bandarini. Alisema ni kweli wizara yake imepata malalamiko hayo ya tozo za kontena na wawekezaji wengi nd ndiyo sababu waliamua kukutana nao kuwasikiliza. “Kwenye hili suala kuna sekta mbalimbali zinahusika kwa hiyo serikali itaratibu tukae pamoja tuangelie nini kifanyike tuwasaidie wafanyabiashara hawa na tumekubaliana kwamba ndani ya siku 60 tutakuwa tumepata jawabu la malalamiko haya,” alisema Waziri Jafo Alisema malengo ya Rais Samia ni kuona viwanda vinafanya vizuri mwaka hadi mwaka na uwekezaji unaendelea kukua hivyo...

Afrika Tunapaswa Kutumia Rasilimali Tulizonazo Kuzalisha Umeme Wa Kutosha- Dkt.Biteko

📌 *Asema pamoja na dunia kuhamia kwenye nishati jadidifu, makaa ya mawe yatasaidia Afrika kuwa na umeme wa kutosha* 📌 *Aeleza mafanikio sekta ya nishati Tanzania katika Jukwaa la Mawaziri Wiki ya Nishati India* 📌 *Tanzania yapongezwa kwa miradi ya kikanda ya umeme* *Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa pamoja na dunia sasa kuweka mkazo ikiwemo ya kifedha kwenye uzalishaji umeme kwa kutumia nishati jadidifu kama vile jua, maji na upepo,  nchi za Afrika zinapaswa kutumia vyanzo ilivyonavyo kama vile makaa ya mawe ili kuweza kuwa na umeme wa kutosha. Dkt. Biteko amesema hayo  leo Februari 11, 2025, New Delhi, India wakati akishiriki katika mjadala wa Mawaziri wa Sekta ya Nishati kutoka India, Qatar, Uingereza na Tanzania wenye  mada iliyosema Mpango Mpya wa Dunia wa Biashara ya Nishati ikiwa ni sehemu ya Mkutano wa Wiki ya Nishati India. Dkt.Biteko ametolea mfano kuwa Tanzania ina ma...