Skip to main content

Posts

Showing posts from May 27, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

WAZIRI MAKONDA ASEMA MUDA WA ONYO UMEISHA, SHERIA KUCHUKUA HATUA MITANDAONI

  Kufuatia kuongezeka kwa baadhi ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii kupakia maudhui yanayokiuka maadili ya Kitanzania, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  amesema Serikali ipo katika hatua za mwisho kuja na mwarobaini wa kudhibiti tabia hiyo inayozidi kuathiri jamii hususan vijana. Akizungumza kuhusu mwenendo wa maudhui kwenye majukwaa ya kidijitali, Waziri Makonda amesema umefika wakati sheria zichukue nafasi yake badala ya kuendelea kutoa onyo kwa maneno pekee.  Aidha, Serikali imewataka watumiaji wa mitandao ya kijamii pamoja na wanaojiita content creators kuhakikisha wanazingatia maadili, sheria na utu wa jamii wanayoiwakilisha mtandaoni huku hatua kali zikitarajiwa kuchukuliwa kwa watakaobainika kukiuka taratibu zilizowekwa.

WANAUME MSIKWEPE MAJUKUMU", TAWLA.

  Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga  Jamii mkoani Tanga imetakiwa kutojiingiza katika mahusiano yatakayo kuja kuvunja haki za wengine. Hayo yamesemwa na mratibu chama Cha wanasheria wanawake Tanzania (TAWLA) mkoa wa Tanga ambae pia ni mwanasheria Mwanaidi Kombo kutokana na ongezeko kubwa na wanaume wanaotelekeza familia hasa watoto. Huku akisema kwasasa hiyo imekuwa changamoto kubwa na wamekuwa wakipokea kesi nyingi kuhusu wanaume kutohudumia watoto. Mwanaidi aliongeza kuwa kwa mujibu wa Sheria ya watoto,Sheria namba 21 ya mwaka 2009 katika kifungu Cha 9(1),kimeeleza wajibu wa mtoto kuishi na wazazi wake lakini pia wajibu wa wazazi kumhudumia mtoto yale mahitaji muhimu ya kibinaadamu kiwemo,chakula,malazi,mavazi na elimu pamoja na huduma za matibabu. Pia katika 9(2)wameelekeza kuwa mzazi ama mlezi atakae kuwa na mtoto katika malezi atawajibika kumpatia mtoto hayo mahitaji,na katika kifungu Cha 33-41 kimeelekeza wajibu wa mzazi ama mlezi,afisa maendeleo ya jamii,kuhakikisha mtoto an...

TANZANIA KUJIIMARISHA KUWA KITOVU CHA UTAFITI KATIKA KUKABILIANA NA MAJANGA

Na Mwandishi Wetu - Msumbiji SERIKALI imesema inaendelea kujipanga kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha utafiti katika kukabiliana na majanga katika ukanda wa Kusini mwa Afrika (SADC) na Afrika Mashariki, hatua itakayosaidia kuimarisha mifumo ya tahadhari na uokoaji. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Dkt. Jim Yonazi, wakati wa ziara ya kubadilishana uzoefu kati ya Tanzania na Msumbiji kuhusu hatua za mapema kabla ya majanga. Ziara hiyo ya siku tano inayofanyika jijini Maputo nchini Msumbiji kuanzia Mei 25 hadi 29, 2026, inalenga kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu matumizi ya teknolojia za kisasa, tafiti na mifumo ya utoaji wa taarifa za tahadhari mapema ili kupunguza athari za majanga. Akizungumza katika mkutano huo, Dkt. Yonazi alisema Tanzania imeendelea kujenga uwezo wake katika kukabiliana na majanga kupitia uwekezaji katika tafiti na matumizi ya teknolojia za kisasa ikiwemo mifumo ya kidijitali na aki...

MTWARA YATANUA FURSA ZA MADINI, MAPATO YA SERIKALI YAPANDA MARA NNE

📍Mtwara Mkoa wa Mtwara umeendelea kujidhihirisha kama kitovu muhimu cha uwekezaji wa madini nchini kutokana na uwepo wa rasilimali nyingi za madini ya viwandani, vito na madini mkakati, huku mapato ya Serikali kupitia sekta hiyo yakiongezeka kwa kasi katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mtwara, Winnifrida Mrema, amesema mkoa huo unafahamika zaidi kwa uwepo wa madini ya chokaa yanayotumika kuzalisha saruji katika Kiwanda cha Saruji cha Dangote, jambo linalochangia kukuza uchumi wa mkoa na kuimarisha shughuli za viwanda nchini. Amesema Mkoa wa Mtwara pia una utajiri wa madini mengine ya viwandani yakiwemo chuma, shaba, kinywe, ulanga pamoja na madini ya mchanga mzito (heavy mineral sands), ambayo ni miongoni mwa madini mkakati yanayohitajika kwa kiwango kikubwa duniani katika utengenezaji wa teknolojia mbalimbali ikiwemo magari ya umeme. Aidha, amesema Bandari ya Mtwara imeendelea kuwa kiungo muhimu cha biashara na usafirishaji wa madini na bidhaa za ...

MWANAFA ASHIRIKI SWALAH YA EID JITEGEMEE, AENDA MLINGANO KUCHINJA NG'OMBE

 *EID AL-ADHA MUHEZA:* Na Mwandishi Wetu, Muheza  MBUNGE wa Muheza, Mhe. Hamis Mwinjuma (MwanaFA), ameshiriki Swalah ya Eid Al-Adha iliyofanyika katika uwanja wa Jitegemee wilayani hapa, na kuwataka waumini wa Kiislamu kudumisha amani. Swalah hiyo kubwa ya iliongozwa na Sheikh Khatibu, ambaye kabla ya kuanza ibada, aliwasihi Waislamu kufuata kikamilifu mafundisho ya Mtume Muhammad (SAW) na kuacha kupoteza muda mwingi kwenye mambo yasiyo na msingi.  Sheikh Khatibu aliwakumbusha waumini hao umuhimu wa kufanya ibada za funga zilizowekwa kisheria katika siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Dhul-Hijjah ili kujisogeza karibu na Mwenyezi Mungu. Akisalimia maelfu ya waumini waliofurika uwanjani hapo, Mhe. Mwinjuma aliwatakia heri ya sikukuu ya Eid na kuwasisitiza kuendelea kuwaombea viongozi wakuu wa nchi kila wanapofanya ibada zao. "Tunapoendelea kufurahia sikukuu hii ya kuchinja, nawaomba sana ndugu zangu tusiache kuwaombea viongozi wetu wa kitaifa, hususan Rais wa Jamhuri ya Muunga...

SAGINI ACHINJA NG'OMBE 400 NA KONDOO 1000 EID AL ADHA

Mbunge wa zamani wa Jimbo la Butiama Mhe. Jumanne Abdallah Sagini Kwa kushirikiana Taasisi ya ITTIFAK International kutoka nchini Uturuki amechinja Ng'ombe 400 na Kondoo 1000 na kugawanywa kwenye vitongoji 370 na taasisi zote za umma na binafsi zilizopo katika Wilaya ya Butiama ikiwemo baadhi ya misikiti Wilaya ya Musoma mkoani Mara kwa ajili ya kitoweo kwa wananchi kipindi hiki cha kusherehekea Sikukuu ya Eid Al-Adha. Zoezi hilo la Sadaka limefanyika leo Mei 27, 2026  nyumbani kwake Kijiji cha Kiabakari, Kata ya Kukirango katika Wilaya ya Butiama kama sehemu ya kuimarika kiimani na ukarimu na mshikamano na upendo. Kwa upande wake Sheikh wa Kata ya Mugango Musoma Vijijini Mwabadi Yusuph Chogero ameeleza kuwa kwa kipindi hiki Sagini amepanua wigo zaidi kwani Sadaka hiyo imewafikia hadi Misikiti Saba iliyopo Musoma Vijijini, huku Sheikh wa Kata ya Kukirango Juma Maharage amesema imekuwa ni desturi ya Sagini kuwaalika wananchi mbalimbali katika kushiriki kitoweo kwa pamoja. Baadhi ya ...