Aliyewahi kuwa Katibu wa Rais wa Awamu ya Tano,Hayati Dkt.John Pombe Magufuli ameingia kwenye kinyang’anyiro cha ubunge wa Jimbo la Sengerema Mkoani Mwanza. Ngusa Samike amechukua fomu ya kuwania uteuzi wa kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi(CCM) kwenye nafasi ubunge wa Jimbo la Sengerema katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Uamuzi wa Samike wa kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho kumeleta kumezua msisimko Mkubwa kwenye Jimbo hilo,huku baadhi ya wakazi wa sengerema wakimpa nafasi ya kuwa miongoni mwa watia wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda. Ngusa Samike anabebwa zaidi na rekodi yake ya kuwa karibu na Utendaji wa Hayati Magufuli pamoja na Uzoefu alioupata akiwa Wizara ya ujenzi pamoja Ikulu. Wengi wa wananchi pamoja na Makada wa CCM wanaamini kwa Samike atalitumikia Jimbo la Sengerema Weledi na kwa kasi inayotarajiwa. Uungwaji Mkono wa Samike Unazidi Kuongezeka kutokana na Mvuto wake wa kisiasa pamoja na Maono aliyoanza kuyawasilisha kwa wananchi wa Jimbo la Sengerema. Baadhi...
Marato tv - Sauti ya Jamii