Skip to main content

Posts

Showing posts from July 19, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kampuni ya CRCEG inatekeleza kwa ubora na kasi ujenzi uwanja wa AFCON Arusha-Serikali

Na Prosper Makene, Arusha NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Hamis Mwinjuma ameipongeza Kampuni ya CRCEG ya kutoka nchini China ambayo inajenga uwanja wa mpira wa miguu jijini Arusha utakaotumika kwa michuano ya AFCON 2027 kwa kuweza kujenga uwanja huo kwa kasi na viwango vya hali ya juu. Akizungunza mwishoni mwa wiki wakati wa halfa ya kumalizika kwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa zege na kuanza ramsi kufunga paa la uwanja huo, Naibu Waziri amesema kuwa ni mara ya kwanza nchini kuona mkandarasi anamaliza kazi aliyopewa kabla ya muda kwani amemaliza awamu ya kwanza siku 20 kabla ya  muda uliopangwa kwenye mkataba. Mwinjuma alimaalufu kama Mwana Fa amesema: "Mkataba huu wa ujenzi wa uwanja mkubwa wa michezi jijini Arusha, ulitiwa saini tarehe 19, mwezi wa 3, mwaka jana (2024), lakini natambua kazi rasmi zilianza tarehe 25, mwezi wa 7, mwaka huo huo, baada ya utaratibu wa kukabidhiana site pamoja na shughuli zingine za awali kukamilika. Mkandarasi amepewa jukumu la kufanya u...

Muhimbili na Vodacom kutoa matibabu bila malipo.

  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania Foundation itafanya kambi maalum ya huduma za  uchunguzi na matibabu ya ubingwa bobezi bila malipo kwa wakazi wa mikoa ya Tanga na Kilimanjaro kuanzia Julai 21 hadi 27, 2025. Kwa wakazi wa mkoa wa Tanga kambi hiyo itafanyika Chuo cha Ualimu Korogwe Julai  21 hadi 23 na Kilimanjaro itafanyika soko la Memorial lililopo  Manispaa ya Moshi,   Julai 25 hadi 27, 2025.  Huduma zitakazotolewa katika kambi hiyo ni pamoja na uchunguzi na matibabu ya   macho, afya ya kinywa na meno,  magonjwa ya akina mama na afya ya uzazi, magonjwa ya ngozi, magonjwa ya afya ya akili,  sukari na homoni pamoja na saratani ikiwemo tezi dume. Aidha, kambi hiyo itatumika kama jukwaa la kutoa elimu kwa wakazi wa mikoa hiyo na maeneo ya jirani namna ya kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza ambayo yamekuwa tishio na kugharimu fedha nyingi kwa wananchi walio wengi. Hospitali ya Taifa Muhimbili Up...