Na Mwandishi wetu Jovina Massano Musoma. Mwenyekiti wa mtaa wa Pwani Kata ya Mwisenge Manispaa ya Musoma mkoani Mara Abdallah Edward Kitundu amesema Mfuko wa hifadhi ya Jamii (NSSF) ni muhimu kwa Maendeleo na ustawi wa jamii. Ameyasema hayo Septemba 8,2026 mara baada ya maafisa matekelezo wa hifadhi skimu kutoka NSSF kutoa elimu kwa wakazi wa mitaa ya VETA na Pwani katika kata hiyo. Abdallah ameeleza kuwa mpango huu wa NSSF una manufaa makubwa kwa jamii kwani ni mojawapo ya njia ya kijiinua kiuchumi na kujiletea maendeleo. " Uwekaji akiba NSSF ni mzuri na muhimu kwa jamii kwani inasaidia kupunguza utegemezi na ghalama za maisha hapo baadae kwa kuwa mwanachama anapata huduma za matibabu ya bima kupitia michango take anayojiwekea yeye na familia yake". Ameipongeza NSSF kufika na kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kujiwekea akiba ya baadae na manufaa yake ambayo yanapelekea kupata maendeleo sambamba na unafuu wa ghalama mbalimbali na kupunguza utegemezi usio wa lazima kwa baad...
Marato tv - Sauti ya Jamii