Skip to main content

Posts

Showing posts from October 2, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

TADB YATWAA TUZO YA KIMATAIFA KWA UFADHILI WA KILIMO

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imetunukiwa tuzo ya Ubora katika Suluhisho za Ufadhili wa Kilimo Tanzania katika tuzo za Global Brand Awards, zilizofanyika Dubai, jana Tuzo hiyo inatambua juhudi za TADB katika kuendeleza suluhisho bunifu za kifedha kwa sekta ya kilimo, ikiwemo ufadhili wa kijani, unaolenga kukuza uwekezaji endelevu na kuimarisha uwezo wa sekta ya kilimo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Frank Nyabundege, alisema tuzo hiyo itaendelea kuhamasisha benki kubuni na kutoa suluhisho za kifedha endelevu zinazochochea mageuzi ya kilimo na kuchangia utekelezaji wa malengo ya Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050. Tuzo hiyo ilipokelewa kwa niaba ya TADB na Frank Nyabundege, Mkurugenzi Mtendaji; Mkani Waziri, Mkurugenzi wa Mipango, Ushauri na Mahusiano ya Taasisi; na Irene John, Meneja wa Masoko, Huduma kwa Wateja na Mahusiano ya Taasisi.

GF YAPATA SOKO LA MAGARI GEITA, YAUZA ZAIDI YA 10 KUPITIA MAONESHO

 Na. Wellu Mtaki, Geita KAMPUNI ya GF Truck Equipment Smart imesema Maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita yamefungua fursa kubwa ya biashara, baada ya kupata wateja wapya na kuuza zaidi ya magari 10 kwa wachimbaji na wadau mbalimbali wa sekta ya madini. Kampuni hiyo imesema maonesho hayo yamekuwa na tija kwa biashara yake, huku baadhi ya wachimbaji wakifanya manunuzi ya magari na wengine kuonyesha nia ya kununua bidhaa na vifaa vinavyotolewa na kampuni hiyo. Akizungumza katika maonesho hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa GF Truck Equipment Smart, Deus, amesema kampuni hiyo imepata mwitikio mkubwa kutoka kwa wachimbaji, hali iliyochochea ongezeko la mauzo. Amesema hadi sasa kampuni hiyo imekabidhi gari moja kwa mteja, huku ikiwa katika hatua za mwisho za kukabidhi mteja mwingine aliyenunua zaidi ya magari 10 kupitia maonesho hayo. “Tunamshukuru Mungu kwa siku hii kwa sababu tumeweza kumkabidhi mteja wetu gari moja. Kupitia maonesho haya tumepata mzigo mkubwa wa mauzo,...

DKT. JUDITH MHINA: SEKTA BINAFSI NI UFUNGUO WA KUENDELEZA KANDA ZA USAFIRISHAJI NA MAENDELEO ENDELEVU YA VIWANDA AFRIKA

 Na Mwandishi Wetu El Alamein, Misri - Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za PMM Group na Mwenyekiti wa EACCIA wa Kamati ya Kiufundi ya AfBC ya Kanda za Usafirishaji, Muunganiko na Maeneo Maalum ya Kiuchumi, Dkt. Judith Mhina, amesisitiza kuwa sekta binafsi ina nafasi muhimu katika kuendeleza kanda za usafirishaji, biashara, uwekezaji na maendeleo endelevu ya viwanda barani Afrika. Dkt. Mhina aliyasema hayo tarehe 1, Oktoba wakati akiwasilisha mada katika Jukwaa la Ngazi ya Juu la Sekta Binafsi la Baraza la Biashara Afrika (AfBC) lililofanyika katika Hoteli ya Rhatus, El Alamein nchini Misri Jukwaa hilo limeanza Leo tarehe 1 hadi 3 Oktoba 2026. Jukwaa hilo limefanyika pembeni mwa Mkutano wa Nusu Mwaka wa Umoja wa Afrika. Jukwaa hilo limewakutanisha viongozi wa sekta binafsi, watunga sera na wadau wa maendeleo kujadili fursa za kuimarisha biashara, uwekezaji na ushirikiano wa kikanda. Alieleza kuwa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo ya Afrika Mashariki (EACCIA) ilianzishwa Septemba 2...

PRIVATE SECTOR KEY TO ADVANCING AFRICA'S CORRIDORS, TRADE AND INDUSTRIAL DEVELOPMENT - DR. JUDITH MHINA

 By Prosper Makene  El Alamein, Egypt- Executive Chairperson of PMM Group of Companies and EACCIA Chairperson of the AfBC Technical Committee on Corridors, Connectivity & Special Economic Zones, Dr. Judith I. Mhina, has underscored the critical role of private sector leadership in advancing Africa's corridors, trade, investment and sustainable industrial development. Dr. Mhina made the presentation at the Africa Business Council (AfBC) High-Level Private Sector Forum held at Rhatus Hotel, El Alamein, Egypt from 1st to 3rd October 2026, on the margins of the African Union Mid-Year Coordination Summit. The forum brings together African private sector leaders, policymakers and development partners to reflect on opportunities for strengthening trade, investment and regional integration. She explained that the East African Chamber of Commerce, Industry and Agriculture (EACCIA) has existed since September 2005 in Nairobi and was formally launched in Arusha in February 2006, to l...

𝙈𝘼𝙆𝘼𝙈𝙐 𝙒𝘼 𝙍𝘼𝙄𝙎 𝘼𝙎𝙃𝙐𝙃𝙐𝘿𝙄𝘼 𝙐𝙏𝙄𝘼𝙅𝙄 𝙎𝘼𝙄𝙉𝙄, 𝙈𝙋𝘼𝙉𝙂𝙊 𝙒𝘼 𝙐𝙎𝙃𝙄𝙍𝙄𝙆𝙄𝘼𝙉𝙊 𝙒𝘼 𝙏𝘼𝙉𝙀𝙎𝘾𝙊 𝙉𝘼 𝘾𝙍𝘿𝘽 𝙆𝙐𝙒𝘼𝙒𝙀𝙕𝙀𝙎𝙃𝘼 𝙒𝘼𝙉𝘼𝙉𝘾𝙃𝙄 𝙆𝙐𝙋𝘼𝙏𝘼 𝙐𝙈𝙀𝙈𝙀.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ametoa wito kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kushirikiana na wadau husika wa sekta binafsi kuandaa mpango utakaowawezesha wananchi kununua umeme kwa mkopo kama ilivyo mikopo katika mitandao ya simu ili kuwasaidia wananchi wanapokuwa na uhitaji wa umeme lakini hawana fedha. Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati wa hafla ya utiaji Saini Mkataba wa Uzinduzi wa Mpango wa Ufadhili wa Uunganishaji Umeme kwa Wananchi, kati ya Benki ya CRDB na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. Amesema hatua hiyo itaweza kusaidia wananchi kuendelea kutumia huduma ya umeme na kufanya uzalishaji mali au mahitaji ya nyumbani hata pale wanapokuwa na changamoto ya fedha ya kununua umeme huo. Aidha, Makamu wa Rais ameitaka Wizara ya Nishati kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuendeleza mradi ulioanzishwa chini ya Ra...

KIWANDA CHA KIBAHA CHAKUZA FURSA ZA MAGARI KATIKA SEKTA YA MADINI

GF Trucks yakabidhi magari Geita, Amotech yaeleza mahitaji ya usafiri na vifaa katika shughuli za migodi GEITA: Uhitaji wa magari na vifaa vya kusaidia shughuli za uchimbaji madini umejitokeza kuwa fursa ya kibiashara kwa kampuni zinazojihusisha na sekta ya magari nchini, huku GF Trucks & Equipment ikitumia Maonesho ya Tisa ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini kutangaza bidhaa zake na kukabidhi magari kwa wateja. Meneja Biashara na Masoko wa GF Trucks & Equipment, Smart Deus, amesema hayo Oktoba 2, 2026, katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Geita, akieleza kuwa maonesho hayo yameiwezesha kampuni kukutana na wateja na kuonesha magari yanayoweza kutumika katika shughuli mbalimbali za kiuchumi, ikiwemo zinazohusiana na uchimbaji madini. Smart Deus amesema kampuni hiyo pia ina kiwanda cha kuunganisha magari cha GF Vehicle Assemblers kilichopo Kibaha, mkoani Pwani, ambacho ni sehemu ya shughuli zake katika sekta ya magari. Amesema ushiriki wao katika maonesho hayo unatoa...

ESAP MINING SERVICES YAIBUKA KINARA MAONESHO YA 9 YA TEKNOLOJIA YA MADINI GEITA, YATWAA TUZO TATU KWA MPIGO

KAMPUNI ya Esap Mining Services Limited imetwaa tuzo tatu katika Maonyesho ya Tisa ya Teknolojia ya Madini yaliyofanyika mkoani Geita, hatua inayotajwa kuwa chachu ya kuongeza ubunifu, matumizi ya teknolojia za kisasa na ufanisi katika shughuli za uchimbaji madini nchini. Katika ushindi huo mkubwa, kampuni hiyo imejinyakulia tuzo za Mthamini Mkuu wa Maonyesho, Kampuni Bora ya Uchorongaji Miamba (Drilling) na mshindi wa pili katika kipengele cha Kampuni Bora ya Uchimbaji Madini. Akizungumza baada ya kupokea tuzo hizo Leo Oktoba 2,2026 wakati wa Maonesho ya Tisa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea Katika Viwanja vya Dkt.Samia Suluhu Hassan Mkoani Geita, Afisa Utawala na Mawasiliano wa Esap Mining Services Limited,ShabaniMitenenko Sadiki, alisema mafanikio hayo ni hamasa kwa kampuni kuendelea kuboresha huduma zake na kuongeza juhudi katika utekelezaji wa shughuli zake za uchimbaji madini. Alisema kutambuliwa katika vipengele hivyo kunawapa ari ya kuendelea kutumia teknolojia za kisasa n...

ESAP YAZIDI KUWEKEZA TEKNOLOJIA, YALENGA KUIMARISHA HUDUMA ZA ULIPUAJI MIGODINI

 Na. Wellu Mtaki, Geita KAMPUNI ya kizawa ya Tanzania inayojihusisha na usambazaji wa vilipuzi na huduma za ulipuaji katika sekta ya madini, ESAP, imeendelea kuwekeza katika teknolojia na mitambo ya kisasa kwa lengo la kuongeza uwezo wa kutoa huduma kwa migodi mikubwa, ya kati na wachimbaji wadogo nchini. Uwekezaji huo umeifanya kampuni hiyo kuongeza ushiriki wake katika mnyororo wa thamani wa sekta ya madini, huku ikipanua huduma zake katika maeneo mbalimbali yanayojihusisha na shughuli za uchimbaji nchini. Akizungumza mkoani Geita wakati wa Maonesho ya Teknolojia ya Madini, Mkurugenzi wa ESAP, Yahya Puyaga, alisema uwekezaji katika teknolojia ya kisasa umeiwezesha kampuni hiyo kukidhi mahitaji yanayoongezeka katika sekta ya madini. “Local content imetuwezesha sisi kufika na kutoa huduma katika sehemu mbalimbali. Tumewekeza katika teknolojia ya kisasa na mitambo inayotuwezesha kutoa huduma kulingana na mahitaji ya sekta ya madini,” alisema Puyaga. Alisema tofauti na baadhi ya kamp...

SERIKALI YATOA SHILLINGI BILLION 5 KUKUZA WABUNIFU WA TEHAMA,KAMPUNI CHANGA KUNUFAIKA

SERIKALI imefungua fursa ya Sh5 bilioni kwa ajili ya kuwawezesha vijana na wabunifu wenye kampuni changa za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), ikilenga kugeuza mawazo na bunifu zao kuwa biashara zinazokua, ajira na masoko mapya. Fursa hiyo imetolewa kupitia Programu ya Uwezeshaji wa Mikopo kwa Kampuni Changa za TEHAMA iliyozinduliwa jijini Dodoma, ambapo Serikali imesema fedha hizo zitatolewa kwa kampuni zitakazokidhi vigezo na masharti yaliyowekwa. Akizindua programu hiyo, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Kairuki, amesema Serikali inalenga kuona mikopo hiyo ikileta matokeo yanayoonekana katika ukuaji wa kampuni, ongezeko la ajira, mauzo na mapato pamoja na upanuzi wa masoko ndani na nje ya Tanzania. “Swali letu si tu tumetoa mikopo kiasi gani? Swali muhimu zaidi ni fedha hizo zimeleta mabadiliko gani?” amesema. Amesema mikopo hiyo itatolewa katika madaraja matatu, kuanzia Sh1 milioni hadi Sh25 milioni, zaidi ya Sh25 milioni hadi Sh50 milioni na zaidi ...

MADINI SI UCHAWI, NI SAYANSI — FEMATA YATAJA MABADILIKO SEKTA YA MADINI

Na Wellu Mtaki, Geita SHIRIKISHO la Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA) limesema moja ya mafanikio makubwa katika sekta ya madini ni kubadilika kwa mtazamo wa Watanzania kuhusu shughuli za uchimbaji, kutoka kwenye dhana za kishirikina na kuanza kuiona sekta hiyo kama shughuli inayohitaji sayansi, teknolojia na utaalamu. Katibu wa Kamati ya Mahusiano wa FEMATA, Mathew Chengule, amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea mabanda mbalimbali katika Maonesho ya Tisa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita. Chengule amesema elimu inayotolewa kwa wananchi kuhusu sekta ya madini imekuwa na mchango mkubwa katika kuvunja dhana zilizokuwepo kwamba upatikanaji wa madini unahusishwa na uchawi au imani za kishirikina. Amesema kwa sasa uelewa wa wananchi umeongezeka na wengi wameanza kutambua kuwa shughuli za madini zinahitaji matumizi ya teknolojia, taarifa sahihi na mbinu za kisayansi ili kuongeza ufanisi na kupunguza hasara.  “Hatua tuliyopiga ni k...

ESAP YAWEKEZA KIWANDA CHA VILIPUZI BUKOMBE

 Kampuni ya Kizalendo ESAP Yawekeza Kiwanda cha Vilipuzi Bukombe Kuhudumia Migodi Mikubwa na Wachimbaji Wadogo Mafanikio ya Sera ya Maudhui ya Ndani (Local Content) katika sekta ya madini yameanza kuonekana wazi baada ya kampuni ya kizalendo ya ESAP Mining Services kuwekeza kiwanda cha kisasa cha uzalishaji wa vimiminika vya vilipuzi Wilayani Bukombe. Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Mhandisi Yahya Ruyaga, akizungumza Oktoba 2, 2026 katika Maonesho ya 9 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Geita, amesema uwekezaji huo unalenga kupunguza utegemezi wa kuagiza vilipuzi kutoka nje na kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kwa urahisi nchini. "Kupitia kiwanda chetu cha Bukombe tunazalisha vimiminika maalumu vinavyotumika kwenye mifumo ya vilipuzi na tunatumia magari maalumu yenye teknolojia ya kuchanganya vilipuzi moja kwa moja eneo la kazi. Hii inaongeza usalama na ufanisi," amesema Ruyaga. Ruyaga amesema licha ya kuhudumia m...

USALAMA WA CHAKULA NI USALAMA WA TAIFA – KAMATI YA BUNGE

 <Yasisitiza uwezeshaji Miradi ya Umwagilia NA MWANDISHI WETU ;TABORA📍 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imesema usalama wa nchi unaanza na usalama wa chakula, hivyo wananchi hawapaswi kushangazwa na mabadiliko makubwa yanayofanywa na Serikali katika kuwezesha miradi ya Umwagiliaji. Kamati hiyo imeeleza kuwa jitihada za Serikali katika kuwekeza kwenye miradi ya Umwagiliaji zinalenga kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa salama na kujidhatiti katika kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula, hali inayoiwezesha pia kuihakikishia dunia kuhusu uwezo wake wa uzalishaji. Akizungumza katika muendelezo wa ziara ya kukagua miradi ya umwagiliaji inayosimamiwa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Njombe Mjini, Mhe. Deodatus Philip Mwanyika, amesema Tanzania ni salama na msingi wake ni uhakika wa chakula. Mwanyika amesema nchi imekuwa na uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula kwa matumizi ya ndani na hata nje ya nchi,...

SERIKALI KUKAGUA UMILIKI WA KAMPUNI ZA HUDUMA MIGODINI

 Waziri Mavunde awataka Watanzania kuchangamkia fursa za huduma na bidhaa kwenye migodi_ 📍GEITA Serikali kupitia Tume ya Madini inatarajia kuanza kuhakiki umiliki halali wa kampuni zinazotoa huduma kwenye migodi ya madini nchini, ili kuhakikisha fursa za ajira, huduma na biashara zinawanufaisha Watanzania wenye sifa na uwezo unaohitajika. Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, amesema hatua hiyo inalenga kudhibiti utaratibu unaodaiwa kuwepo wa kampuni za kigeni kuingia ubia na Watanzania wasio na sifa stahiki kwa ajili ya kutimiza matakwa ya ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini. Waziri Mavunde ametoa kauli hiyo mapema leo Oktoba 2, 2026, wakati akifungua Siku ya Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini, ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya Kitaifa ya Tisa ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bomba Mbili, Geita. Amesema katika utekelezaji wa Kanuni za Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sek...