Skip to main content

Posts

Showing posts from July 30, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

TARI YAADHIMISHA MIAKA 10 KWA MARATHON NA MAONESHO YA TEKNOLOJIA ZA KILIMO

 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kushiriki Marathon ya TARI itakayofanyika Agosti 2, 2026, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI). Mhe. Senyamule ameyasema hayo mara baada ya kutembelea banda la TARI na kukabidhiwa jezi za marathon hiyo, ambapo alieleza kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo. Amesema marathon hiyo inalenga kuhamasisha afya, kuunganisha wadau wa sekta ya kilimo na kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu mchango wa TARI katika utafiti na maendeleo ya kilimo nchini. Amesema hadi sasa zaidi ya washiriki 1,000 wamekwishajisajili, huku akiwahimiza wananchi wengine kuendelea kujisajili ili kushiriki mbio hizo zitakazoanzia eneo la Nzuguni saa 2:00 asubuhi. Marathon hiyo itakuwa na mbio za kilomita 5, 10 na 21, ili kutoa nafasi kwa makundi mbalimbali ya washiriki. K...

RAIS SAMIA AKITETA NA MAMA MARIA NYERERE WAKIWA SAFARINI KWENDA NCHINI ANGOLA

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mama Maria Nyerere muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kuelekea Luanda, Angola ambapo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa Hospitali iliyopewa jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, tarehe 31 Julai, 2026.

RC MALIMA: MAANDALIZI YA NANENANE KANDA YA MASHARIKI YAFIKIA ASILIMIA 99, AWATAKA WAKULIMA KUZALISHA MAZAO KWA KUZINGATIA MAHITAJI YA SOKO

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Kighoma Malima, leo Julai 30, 2026 ameongoza kikao cha tatu cha Kamati Kuu ya Maandalizi ya Maonesho ya Wakulima (Nanenane) Kanda ya Mashariki 2026, kilichofanyika katika Ukumbi wa JKT Nanenane, Manispaa ya Morogoro. Mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Mhe. Malima alizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua za maandalizi ya maonesho hayo yanayotarajiwa kuzinduliwa rasmi Agosti 1, 2026. Akizungumza na waandishi wa habari, Mhe. Malima aliwahimiza wakulima kuzalisha mazao yanayokidhi mahitaji ya soko la ndani na la kimataifa ili kuongeza tija, ushindani na mchango wa sekta ya kilimo katika ukuaji wa uchumi. Aidha, amesema maandalizi ya maonesho hayo yamefikia asilimia 99, huku maboresho makubwa ya miundombinu na mazingira ya maonesho yakikamilishwa kwa lengo la kuwawezesha wafanyabiashara wadogo na wakubwa kuonesha bidhaa zao katika mazingira bora na kuwapa fursa ya kutambulika zaidi pamoja na kupanua masoko ya bidhaa zao. Maonesho ya Nanenane...

SERENGETI VS MAASAI MARA: VITA MPYA YA MIUNDOMBINU YA KUVUTIA WATALII

 Na Waandishi Wetu Vita mpya imeanza katika ukanda wa Afrika Mashariki. Sio vita vya bunduki wala migogoro ya mipaka. Ni vita vya miundombinu, viwanja vya ndege, barabara na masoko baina ya nchi za Tanzania na Kenya katika kuvutia watalii. Kwa upande wake Serikali ya Kenya ipo katika ujenzi wa uwanja wa ndege wa KSh Bilioni 1.4 unaojengwa pembezoni mwa Maasai Mara.  Wakati huo huo, Serikali ya Tanzania bado ikijipanga kuanza mchakato wa ujenzi wa uwanja wake wa kimataifa wa Serengeti. Ushindi wa vita hii utaamua wapi fedha za watalii zitakapotiririka kwa wingi, hususani katika muongo ujao. Na kwa kuwa Serengeti na Mara zinashiriki mfumo mmoja wa ikolojia, mshindi atapata zaidi ya watalii. Atapata hadithi, ajira na uchumi. Kwa wiki moja timu ya waandishi ilifanya uchunguzi wa kina nchini Kenya. Tulitoka Nairobi hadi Narok town, kisha hadi Talek, na tukafika ndani ya kilomita 30 za milango ya Sekenani na Oloololo. Kila mtu tuliyemzungumza, kuanzia maafisa wa kaunti, wahandisi, m...

INSIDE KENYA’S KSH 1.4 BILLION NAROK AIRPORT PLAN: HOW TANZANIA MUST SPEED UP TO SECURE THE SERENGETI

 By Staff Writers Kenya is executing what tourism experts are calling the most aggressive infrastructure play in East Africa in the last decade. At the center of it is a KSh 1.4 billion international airport rising on the edge of Maasai Mara in Narok County. Following a one-week investigation in Kenya by this publication, it is clear this project is not about convenience alone. It is about controlling the flow of tourists, dollars, and influence in the shared 25,000 square kilometer Serengeti-Mara ecosystem.  For seven days in Kenya, our team moved from Nairobi to Narok town, to Talek, and within 30km of the Sekenani and Oloololo gates. The investigative reporters spoke with county officials, Kenya Airports Authority engineers, tour company owners, lodge managers, and drivers. The message was consistent.  “We are not just building an airport,” a senior engineer with the Kenya Airports Authority told us at the construction site. “We are building the front door to the Migra...

RAIS SAMIA AIPA TADB NGUVU,MTAJI WAPAA HADI BILLIONI 452.16

 Jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuimarisha sekta ya kilimo zimeendelea kuzaa matunda baada ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuongeza mtaji wake kutoka Shilingi bilioni 60 hadi kufikia Shilingi bilioni 452.16, hatua inayoongeza uwezo wa benki hiyo kufadhili kilimo, mifugo na uvuvi kwa kiwango kikubwa zaidi. Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 30, 2026, katika ukumbi wa Idara ya Habari  MAELEZO jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania TADB, Frank Nyabundege, amesema mafanikio hayo yametokana na uwekezaji mkubwa wa Serikali pamoja na ushirikiano na taasisi mbalimbali za maendeleo. Amesema kabla ya Serikali ya Awamu ya Sita, mtaji wa TADB ulikuwa Shilingi bilioni 60 pekee, lakini sasa umefikia Shilingi bilioni 452.16, jambo linaloifanya benki hiyo kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuwafikia wakulima, wafugaji na wavuvi nchini. "Kabla ya Serikali ya Awamu ya Sita, mtaj...

MKURUGENZI MKUU WA REA AZUNGUMZA NA WADAU KATIKA KUWEKA MIKAKATI YA USAMBAZAJI WA NISHATI YA UMEME VIJIJINI

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy leo Julai 30, 2026 amezungumza na Wajumbe wa Rural Energy Working Group, ambalo ni Jukwaa lililoundwa na REA likishirikisha Taasisi mbalimbali za Serikali ambao ni Wadau muhimu katika kusambaza Nishati Bora Vijijini. Mhandisi Saidy amesema kuwa Jukwaa hilo ni muhimu sana katika kuratibu, kubadilishana taarifa na kuwa na mipango ya pamoja katika kusaidia utekelezaji wa miradi ya Wakala na kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya nishati bora vijijini kwa wakati.  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Utafiti wa REA, Mhandisi Jensen Mahavile amesema kuwa kundi hilo pia ni jukwaa muhimu kwa sababu linatoa ushauri pamoja na kutoa ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazotokea wakati wa utekelezaji wa miradi ya kusambaza nishati bora vijijini.

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA NA MKURUGENZI MTENDAJI MUHIMBILI WAWEKA MIKAKATI MADHUBUTI KUBORESHA MFUMO WA MALIPO YA HUDUMA ZA AFYA

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Grace Magembe, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Dellilah Kimambo, kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma za afya na kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha mfumo wa malipo ya huduma ili kuwawezesha wananchi kupata huduma kwa urahisi, haraka, kwa ufanisi na kuondoa malalamiko ya wananchi. Katika kikao hicho, Dkt. Magembe amesisitiza umuhimu wa matumizi ya teknolojia katika kuboresha huduma za afya, akimtaka Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisha mifumo ya TEHAMA ya hospitali inaendelea kuimarishwa ili kurahisisha mchakato wa malipo ya huduma, kuongeza uwazi kwa wananchi, kupunguza usumbufu na muda wa kusubiri kwa wagonjwa, pamoja na kuondoa udanganyifu. “Mwananchi apate taarifa za malipo anayotakiwa kufanya kiganjani mwake kupitia simu ili kabla ya kulipa ajihakikishie kama malipo hayo ni sahihi au hapana”, amesema Dr Grace.  Amemwelekeza Mkurugenzi wa Muhimbili kuimarisha usimamizi wa hu...

CHATANDA SASA MLEZI WA CCM MKOA WA MARA

 NA: MWANDISHI WETU Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Taifa, na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu (MCC), Mary Chatanda, amebadilishwa mkoa wa ulezi wa kichama na sasa ni mlezi wa CCM mkoa wa Mara. Mabadiliko hayo yamefanyika Julai 29, 2026, Zanzibar, kufuatia vikao vya Chama vinavyoendelea. Kabla ya mabadiliko hayo, Chatanda alikuwa mlezi wa mikoa ya Mjini na Magharibi, Zanzibar. Akizungumzia mabadiliko hayo, Chatanda amekishukuru Chama chake kwa kuendelea kumuamini kutekeleza majukumu mbalimbali ya kichama. "Nimepokea taarifa hii ya mabadiliko ya ulezi wa Chama mkoa kwa moyo wa unyeyekevu. Nakishukuru Chama changu kwa kuniamini. Niwaombe wanachama wenzangu na wananchi kwa ujumla tushirikiane kuhakikisha tunasukuma mbele gurudumu la maendeleo na Chama chetu". Ameongeza kuwa "Serikali ya CCM chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imepeleka fedha nyingi za miradi ya maendeleo mkoani Mara, ni wajibu wetu kuhakikisha fedha hizo zina...

VISIMA 67,000: NGUVU MPYA YA KUONGEZA CHAKULA NA KIPATO CHA MKULIMA

 Arusha.  Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) imeanza utekelezaji wa mpango wa kuchimba visima 67,000 kwa wakulima wadogo nchini, hatua inayolenga kuongeza uzalishaji wa mazao, kuimarisha usalama wa chakula na kufungua maelfu ya ajira kwa vijana. Akizungumza katika Kongamano la 10 la Ununuzi wa Umma mwaka 2026 jijini Arusha, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raymond Mndolwa, amesema mpango huo unatekeleza maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati wa uzinduzi wa mradi wa uchimbaji wa visima kwa wakulima wadogo katika Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Mbeya mwaka 2023. «"Lengo letu ni kumkomboa mkulima mdogo kutokana na utegemezi wa mvua kwa kuhakikisha anapata maji ya uhakika kwa ajili ya uzalishaji wa mwaka mzima. Hii itachochea uzalishaji, kuongeza kipato cha wakulima na kuimarisha usalama wa chakula nchini," amesema Mndolwa.» Amesema mpango huo pia unalenga kufikisha huduma za umwagiliaji kwa wakulima walio nje ya skimu ra...