Skip to main content

Posts

Showing posts from September 2, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

SHIRIKA LA NYUMBA KUJIPANGA KUKABILIANA NA ONGEZEKO LA WATU TANGA.

   Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga. Shirika la Nyumba Nchini (NHC) limejipanga kuendelea kutoa huduma ya makazi bora kwa wananchi  sambamba na kukabiliana na ongezeko la watu kutokana na kasi ya maendeleo na uhitaji uliopo Kwa sasa. Hayo yamesemwa na meneja wa  Shirika la Nyumba 'NHC' mkoa wa Tanga Mhandisi Mussa Kamendu alipokuwa akizungumza na waandshi wa habari ofisini kwake ambapo amesema kuwa  kutokana na kasi ya maendeleo inayochangiwa na uwepo wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ikiwepo Maboresho ya Bandari pamoja na ujenzi wa Bomba la mafuta ghafi.  "Kazi yetu ni kujenga nyumba na kukarabati nyumba ambazo tunazo tayari,kwahiyo tumejinga vizuri kukabiliana na ongezeko la watu na ndio maana kuna miradi mingine ya nyumba inaendelea na pia tunashirikiana na sekta binafsi kwani shirika pekee yet hatuwezi kumaliza changamoto hii ya makazi ", alisema Mhandis. Kamendu  Aidha Mhandisi Kamendu amesema mpaka sasa kuna mradi wa nyumba 20 za makazi...

SHIRIKA LA NYUMBA KUJIPANGA KUKABILIANA NA ONGEZEKO LA WATU TANGA.

 Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga. Shirika la Nyumba Nchini (NHC) limejipanga kuendelea kutoa huduma ya makazi bora kwa wananchi  sambamba na kukabiliana na ongezeko la watu kutokana na kasi ya maendeleo na uhitaji uliopo Kwa sasa. Hayo yamesemwa na meneja wa  Shirika la Nyumba 'NHC' mkoa wa Tanga Mhandisi Mussa Kamendu alipokuwa akizungumza na waandshi wa habari ofisini kwake ambapo amesema kuwa  kutokana na kasi ya maendeleo inayochangiwa na uwepo wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ikiwepo Maboresho ya Bandari pamoja na ujenzi wa Bomba la mafuta ghafi.  "Kazi yetu ni kujenga nyumba na kukarabati nyumba ambazo tunazo tayari,kwahiyo tumejinga vizuri kukabiliana na ongezeko la watu na ndio maana kuna miradi mingine ya nyumba inaendelea na pia tunashirikiana na sekta binafsi kwani shirika pekee yet hatuwezi kumaliza changamoto hii ya makazi ", alisema Mhandis. Kamendu  Aidha Mhandisi Kamendu amesema mpaka sasa kuna mradi wa nyumba 20 za makazi unaoen...

WAZEE WA KIMILA WAPAMBA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU MISSENYI

Wazee wa kimila maarufu kama Abenkorogo katika Wilaya ya Missenyi, mkoani Kagera, wamepamba mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kwa kujitokeza kwa wingi huku wakiwa wamevalia mavazi yao ya asili.  Wazee hao walionekana wakiwa wamevaa kanzu nyeupe, koti,fimbo na kofia huku baadhi yao wakibeba vibuyu mikononi walishiriki katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru yaliyofanyika katika Kijiji cha Gera, wakati wa makabidhiano ya mwenge huo kati ya Mkuu wa Wilaya ya Missenyi, Kanali Mstaafu Hamis Maiga, na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Erasto Siima.  Katika tukio hilo, wazee hao pia walipewa fursa ya kuubeba Mwenge wa Uhuru ambapo kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wazo Mwang’onda, amesema amefurahishwa na namna wazee hao wa kimila walivyoshiriki katika tukio hilo muhimu lenye Tunu ya Taifa, akiwataka kuendelea kuwa mabalozi wa amani, mshikamano na maadili mema kwa vijana wao. Mwang’onda amewataka wazee hao kuendelea kudumisha mila na tamaduni zao, pamoja na kuhakikisha zinahifadhiwa na ...

WAZIRI MKENDA ATAJA MIKAKATI YA SERIKALI KATIKA UBORESHAJI SEKTA YA ELIMU NCHINI

 Serikali imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha sekta ya elimu kwa kuongeza miaka ya elimu ya lazima, kupanua fursa za elimu ya sekondari na kuimarisha mafunzo ya ufundi ili kuwapa vijana uwezo wa kushiriki kikamilifu katika soko la ajira.   Akizungumza Septemba 02, 2026 jijini Dodoma na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema maandalizi ya utekelezaji wa miaka 10 ya elimu ya lazima kuanzia mwaka 2028 yanaendelea, hatua itakayohitaji miundombinu, walimu na nafasi za kutosha katika shule za sekondari.   Prof. Mkenda amebainisha kuwa mpango huo utasababisha ongezeko kubwa la wanafunzi watakaoingia sekondari, hivyo Serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha wanafunzi wote wanaostahili wanapata nafasi ya kuendelea na masomo.   Aidha, ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuimarisha mfumo wa elimu wenye mikondo ya elimu ya jumla na elimu ya amali, ili wanafunzi wapate maarifa na stadi zinazowaweze...

WAZIRI MKENDA ATAJA MIKAKATI YA SERIKALI KATIKA UBORESHAJI SEKTA YA ELIMU NCHINI

 Serikali imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha sekta ya elimu kwa kuongeza miaka ya elimu ya lazima, kupanua fursa za elimu ya sekondari na kuimarisha mafunzo ya ufundi ili kuwapa vijana uwezo wa kushiriki kikamilifu katika soko la ajira.   Akizungumza Septemba 02, 2026 jijini Dodoma na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema maandalizi ya utekelezaji wa miaka 10 ya elimu ya lazima kuanzia mwaka 2028 yanaendelea, hatua itakayohitaji miundombinu, walimu na nafasi za kutosha katika shule za sekondari.   Prof. Mkenda amebainisha kuwa mpango huo utasababisha ongezeko kubwa la wanafunzi watakaoingia sekondari, hivyo Serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha wanafunzi wote wanaostahili wanapata nafasi ya kuendelea na masomo.   Aidha, ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuimarisha mfumo wa elimu wenye mikondo ya elimu ya jumla na elimu ya amali, ili wanafunzi wapate maarifa na stadi zinazowawez...

RIDHIWANI KIKWETE APOKEA TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA TRAMPA, ATARAJIA MKUTANO WENYE MATOKEO CHANYA

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, amepongeza maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Chama cha Watunza Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA), akieleza kuwa mkutano huo unatarajiwa kuwa chachu ya kuimarisha chama hicho na kuendeleza tasnia ya kumbukumbu na nyaraka nchini. Kikwete ameyasema hayo baada ya kupokea taarifa ya maandalizi ya Mkutano Mkuu huo kutoka kwa Mwenyekiti wa TRAMPA, Devotha Mrope, aliyefika ofisini kwake Mtumba, Dodoma pamoja na Kamati Tendaji ya chama hicho. Amesema ameridhishwa na maandalizi yaliyofanyika, huku akiwapongeza viongozi wa TRAMPA kwa kazi nzuri waliyoifanya na kuwatakia maandalizi mema kuelekea mkutano huo. “Tumewapongeza kwa kazi nzuri ya maandalizi na tunatarajia mkutano mzuri unaolenga kuimarisha chama chao na tasnia yao,” amesema Kikwete. Mkutano huo unatarajiwa kujadili na kuweka mikakati mbalimbali ya kuimarisha TRAMPA pamoja na kuendeleza taaluma na tasnia ya utunzaji wa kumbukumbu na ...

WAZAZI WAHIMIZWA KUFUATILIA ELIMU NA TABIA ZA WATOTO NYUMBANI

Na Mwandishi Wetu - Dodoma. Wazazi wamehimizwa kuwa na ushirikiano wa karibu na walimu katika kufuatilia maendeleo ya watoto wao wanapokuwa nyumbani, ili kusaidia kukuza uwezo wao kitaaluma na kujenga msingi bora wa elimu, badala ya kutegemea walimu pekee katika jukumu hilo. Wito huo umetolewa na Mkuu wa shule ya Shekinah Pre & Primary School Obadia Mwambapa wakati wa siku maalumu ya kufunga shule, ambapo amesema ushirikiano kati ya wazazi na walimu ni muhimu katika kuhakikisha watoto wanapata malezi na elimu bora.  Amesema wazazi wanapaswa kutenga muda wa kufuatilia masomo ya watoto wao, kujua changamoto wanazokutana nazo na kushirikiana na walimu katika kutafuta suluhisho. Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Shule hiyo Juliana Sabrere amesema ulinzi na usalama wa watoto ni jukumu la pamoja kati ya walimu na wazazi, akisisitiza umuhimu wa kushirikiana katika kulinda maadili mema ya watoto na kuhakikisha wanakua katika mazingira salama na yenye malezi yanayozingatia misingi ya hesh...

HII HAPA MIKOA 14 NCHINI ITAKAYOKUMBANA NA EL NIÑO

 WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Prof. Palamagamba Kabudi, ameitaka mikoa 13 iliyopewa tahadhari kujiandaa mapema kukabiliana na madhara yanayoweza kusababishwa na mvua za El Niño. Akizungumza kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Dharura wa Kukabiliana na Madhara ya El Niño, Prof. Kabudi amesema mikoa hiyo inapaswa kuhakikisha maandalizi yanafanyika kwa wakati ili kupunguza madhara kwa wananchi na mali zao. Mikoa iliyotajwa ni Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu,Morogoro, Kigoma, Tanga, Pwani, Ruvuma, Mara, Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Dar es Salaam. Prof. Kabudi pia amesisitiza umuhimu wa wananchi kupata na kuzingatia taarifa za tahadhari zinazotolewa na mamlaka husika, huku akivitaka vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa maandalizi na hatua za kuchukua. Amesema Serikali, kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, inaendelea kuratibu maandalizi kwa kushirikisha serikali za mikoa, serikali za mitaa na jamii ili kuhak...

SERIKALI YAFAFANUA SHILINGI BILIONI 730 ZA MPANGO WA KUKABILI EL-NIÑO

 SERIKALI imefafanua kuwa makadirio ya Shilingi bilioni 730 yanayotajwa katika Mpango wa Taifa wa Dharura wa Kukabiliana na Madhara ya El-Niño si fedha zilizotengwa na Serikali kwa matumizi ya moja kwa moja, bali ni makadirio ya rasilimali zinazohitajika kutekeleza mpango huo kwa kushirikisha Serikali, taasisi, sekta binafsi, mashirika ya kitaifa na kimataifa pamoja na wadau wengine.  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Prof. Palamagamba Kabudi, amesema mpango huo umeandaliwa kufuatia utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wa Agosti 18, 2026, uliotabiri uwepo wa El-Niño yenye nguvu inayoweza kusababisha mvua kubwa, mafuriko, maporomoko ya ardhi, magonjwa ya mlipuko kwa binadamu na wanyama pamoja na madhara kwa miundombinu, makazi na shughuli za kiuchumi.  Amesema mpango huo umeandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikisha Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, Mikoa na Halmashauri, mashirika ya kitaifa na kimataifa, ...