Na Jovina Massano Musoma. Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Musoma mkoani Mara yahamasisha mashirika yasiyo ya kiserikali ( NGO) kuelimisha jamii dhidi ya tahadhali ya mvua za el nino kama ilivyotolewa na Mamlaka ya hali ya hewa hapa nchini. Hayo yamesemwa wakati wa kongamano la Mwaka la mashirika yasiyo ya kiserikali lililohisisha mashirika zaidi ya 50 yaliyopo katika Manispaa hiyo. Kongamano hilo lenye lengo la kujenga fikra mpya katika upatikanaji wa rasilimali fedha kupitia vyanzo vya ndani limeweza kufanya majadiliano mbalimbali yanayohusu jamii ikiwemo uwasilishaji wa taarifa kwa NGO za mwaka 2025/2026. Aidha mashirika yametakiwa kushirikiana na kuhakikisha yanaboresha taarifa zao kupitia mfumo uliopo kuwezesha taarifa kupatikana kwa urahisi ikiwemo uwasilishaji. Akitoa hamasa hiyo Loserian Mollel Saning'o afisa mradi kutoka shirika la Victory Hope Foundation Tanzania (VIHOFOTA) kwa niaba ya Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa hiyo amesema mashirika yashiriki kikamil...
Marato tv - Sauti ya Jamii