Skip to main content

Posts

Showing posts from July 23, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

WADAU WA SEKTA YA MADINI WATOA ELIMU KUPITIA MAONESHO LCCF 2026

 📍 MWANZA Wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini wameendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu fursa na huduma zinazopatikana katika Sekta ya Madini kupitia maonesho yanayoendelea sambamba na Jukwaa la Tano la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini (LCCF 2026) jijini Mwanza. Jukwaa hilo limewakutanisha wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini, wakiwemo makampuni ya uchimbaji wa madini, watoa huduma migodini, wafanyabiashara wa madini, wawekezaji, taasisi za umma na binafsi, pamoja na vyama vya wachimbaji wa madini kutoka maeneo mbalimbali nchini. LCCF 2026 linafanyika chini ya kaulimbiu: “Kutoka Majadiliano hadi Utekelezaji: Kujenga Sekta Imara ya Madini kupitia Ushirikishwaji wa Watanzania na Uanzishwaji wa Viwanda.”

WAZIRI WA FEDHA ANADI FURSA ZA UWEKEZAJI UINGEREZA

Na Benny Mwaipaja, London LONDON  Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amewakaribisha wawekezaji kutoka jumuiya ya kimataifa, kuchangamia fursa za uwekezaji nchini Tanzania katika sekta mbalimbali zikiwemo miundombinu, nishati, viwanda, kilimo, madini na huduma za kifedha. Mhe. Balozi Omar ametoa wito huo jijini London nchini Uingereza alipoongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Kimkakati wa Uwekezaji na Ushirikiano wa Tanzania (Tanzania Strategic Investment and Partnership Forum) ukiwakutanisha viongozi wakuu wa taasisi kubwa za kifedha duniani, sekta ya bima na vihatarishi ulioandaliwa na Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Standard Bank ya nchini humo. Alisema kuwa Serikali imeweka mazingira bora ya uwekezaji pamoja na vivutio vya kikodi ili kuvutia mitaji kutoka nje itakayochangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayoelekeza nchi ifikie uchumi wa dola za Marekani trilioni 1 ifikapo mwaka 2050 ambapo asilimia 70 ya fedha hizo zinatarajiwa ku...

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA AMWAKILISHA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KATIKA MAHAFALI YA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI

 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb), tarehe 23 Julai 2026, amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mahafali ya 14 ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi yaliyofanyika Kunduchi, jijini Dar es Salaam. Mahafali hayo yalihitimisha mafunzo ya ngazi ya juu ya Mkakati wa Ulinzi na Usalama, ambapo jumla ya wanafunzi 72 kutoka Tanzania na nchi mbalimbali walihitimu baada ya kukamilisha mafunzo hayo. Akizungumza kwa niaba ya Rais katika hafla hiyo, Dkt. Nyansaho alisisitiza kuwa ulinzi na usalama wa Taifa ni jukumu la kila Mtanzania, bila kujali nafasi au wajibu alionao. Alibainisha kuwa amani, utulivu na usalama wa nchi vinategemea ushirikiano wa wananchi wote katika kulinda mipaka, rasilimali na maslahi ya Taifa. Aidha, aliwataka wahitimu wa kozi hiyo kutumia maarifa, ujuzi na uzoefu walioupata katika kuimarisha mifumo ya ulinzi na usalama katika maeneo yao ya kazi, huku wakisi...

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI NA MEGA WE CARE WAANDAA KAMBI YA KUPIMA HOMA YA INI KUELEKEA JULAI 28

 Na: Mwandishi Wetu,DAR ES SALAAM. HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Kampuni ya Dawa ya Mega We Care inaendelea na maandalizi ya kambi ya Uchunguzi wa homa ya Ini kuelekea maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani, Julai 28, 2026. Kambi hiyo inatarajiwa kufanyika katika Kituo cha Kliniki ya Muhimbili Sokoine Drive Medical Centre (MNHSDMC) kilichopo mkabala na SGR jijini Dar es Salaam.  Ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwafikia Wananchi na kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa kupima homa ya Ini mapema pamoja na kupata matibabu. Katika ushirikiano huo, Mega We Care imetoa mchango wa Dawa na Vifaa Tiba vingine vya kitabibu vitakavyotumika kutoa huduma wakati wa kambi hiyo.  Mchango huo ni sehemu ya jukumu la sekta binafsi katika kuunga mkono jitihada za kuboresha afya kwa jamii. Akizungumzia ushiriki huo, Afisa Habari wa Mega We Care, Bw. Mengi Ntasimba amesema kampuni hiyo imeamua kushiriki kama sehemu ya kurudisha kwa jamii na kuhakikisha wananchi wanapata ...

UWT YAMUHIMIZA MKANDARASI KUKAMILISHA MRADI WA MARIA NYERERE SHOPPING MALL

 NA: MWANDISHI WETU, DAR Mkandarasi anayetekeleza mradi wa Maduka ya Biashara ya Maria Nyerere (Maria Nyerere Shopping Mall) ulio chini Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), amehimizwa kuongeza kasi ya ujenzi ili mradi huo ukamilike kwa wakati. Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda, Julai 22, 2026, Jijini Dar es Salaam, katika ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UWT Taifa, kukagua uhai wa Chama na miradi ya Jumuiya hiyo. Chatanda amesema, ipo haja ya mkandarasi huyo kuongeza kasi ya ujenzi, huku akimshauri kuongeza wakandarasi wengine ili kumsaidia baadhi ya kazi na kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi huo. "Mradi unakwenda vizuri, isipokuwa kwa mwenendo unavyokwenda na kwa muda tuliokubaliana huenda asikamilishe kwa wakati. Mkandarasi tunachomuhitaji aukamilishe mradi kwa mujibu wa tulivyokubaliana na kama kuna maeneo yeye hana uwezo wa kufanya, akabidhi kwa wakandarasi wengine (sub contractors) ili kazi ikamilike kwa...

KAMATI YA UTEKELEZAJI UWT TAIFA YAFANYA ZIARA YA MAFUNZO STAMICO

 NA: MWANDISHI WETU, KISARAWE Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), imefaya ziara ya mafunzo katika Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Julai 21, 2026, wilayani Kisarawe mkoani Pwani. Ujumbe huo uliongozwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda. Katika ziara hiyo, Wajumbe wa Kamati hiyo, walitembelea kiwanda cha Rafiki Briquettes, kinachochakata makaa ya mawe kuwa nishati safi ya kupikia ambayo ni rafiki wa afya na utunzaji mazingira. Katika ziara hiyo, Chatanda amesema, wanawake wana mchango mkubwa katika kufanikisha kampeni ya nishati safi ya kupikia kutokana na ukweli kuwa kazi hiyo inafanywa kwa kiwango kikubwa na wanawake. "Tunamuunga mkono Rais wetu, Dk. Samia Suluhu Hassan, katika kampeni ya kuhimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kutunza afya na mazingira. Sisi UWT tunahimiza jamii itumie nishati safi," amesema Chatanda. Aidha, amesema UWT wapo tayari kuwa mabalozi na kushirikiana na STAMICO katika kutoa elimu kwa wanaw...

WIZARA YAJIPANGA KIKAMILIFU KUELEKEA TAMASHA LA NNE LA UTAMADUNI LA KITAIFA 2026.

 Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imefanya kikao cha maandalizi kwa lengo la kupitia na kuratibu hatua mbalimbali za utekelezaji kuelekea Tamasha la Nne la Utamaduni la Kitaifa, litakalofanyika kuanzia tarehe 25 hadi 29 Agosti 2026. Kikao hicho kimefanyika leo, Julai 23, 2026, katika Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika, jijini Dar es Salaam, kikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Methusela Ntonda. Akiongoza kikao hicho, Bw. Ntonda amesisitiza umuhimu wa ushirikiano na maandalizi madhubuti ili kuhakikisha Tamasha la Nne la Utamaduni la Kitaifa linafanyika kwa mafanikio na kufikia malengo yaliyokusudiwa ya kuenzi utamaduni wa Tanzania. Kikao hicho kimewakutanisha viongozi na watendaji wa Wizara kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji, ikiwemo uratibu wa shughuli za tamasha, maandalizi, pamoja na mikakati ya kuhakikisha tamasha hilo linafanyika kwa ufanisi.