…..Itafantika katika hospitali ya JKCI-ALMC kuanzia tarehe 21 Na Mwandishi Wetu, Arusha Hospitali ya JKCI–ALMC Arusha (Selian ya Mjini) imeandaa Kambi Maalum ya Matibabu ya Kibingwa itakayofanyika kuanzia Septemba 21 hadi 24, 2026, ikiwakutanisha madaktari bingwa na wabobezi kutoka Tanzania na India. Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Dkt. Tatizo Waane, alisema jana kuwa kambi hiyo itawakutanisha wataalamu kutoka Apollo Hospitals–India, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) pamoja na madaktari bingwa wa JKCI–ALMC Arusha (Selian ya Mjini). Alisema kambi hiyo imelenga kuwafikishia wananchi huduma za kibingwa katika maeneo ya magonjwa ya mfumo wa fahamu, upasuaji wa ubongo na uti wa mgongo, magonjwa na upasuaji wa mfumo wa mkojo, pamoja na magonjwa, upasuaji wa mifupa, viungo na majeraha. “Tunatarajia kuona wagonjwa kati ya 100 hadi 200 kwa siku. Watapata nafasi ya kuonana na madaktari bingwa, kufanyiwa tathmini, kupata us...
Marato tv - Sauti ya Jamii