Na Angela Sebastian,Kyerwa MKUU wa Wilaya ya Kyerwa, Zaitun Msofe, amewataka madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kuongeza nguvu katika kudhibiti magendo ya kahawa na mianya yote inayosababisha Halmashauri kukosa mapato, akisema vitendo hivyo vinadhoofisha uchumi wa Wilaya na Taifa kwa ujumla. Msofe alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, kilichojadili utekelezaji wa shughuli za robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026. Alisema Kyerwa ipo katika msimu wa biashara ya kahawa, zao ambalo ni tegemeo kubwa kwa wakazi wa Wilaya hiyo na chanzo muhimu cha mapato ya Halmashauri, hivyo madiwani wanapaswa kufuatilia kwa karibu biashara zinazoendelea katika kata zao na kuhakikisha wafanyabiashara wanatimiza wajibu wa kulipa ushuru. “Tuko katika kipindi cha msimu wa biashara hii ambayo tunaitegemea sana Kyerwa katika kukusanya mapato,Kahawa ndiyo zao kubwa tunalolitegemea hapa kwetu hivyo madiwani nawakumbusha kuwa wapo...
Marato tv - Sauti ya Jamii