MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo mpya za petroli, dizeli na mafuta ya taa zitakazoanza kutumika kuanzia Jumatano, Oktoba 7, 2026, saa 6:01 usiku. EWURA imesema ongezeko hilo limechangiwa na kupanda kwa bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia kutokana na kuibuka upya kwa mgogoro wa kisiasa katika Mashariki ya Kati. Kwa bei za rejareja katika bandari, Dar es Salaam petroli itauzwa hadi Sh4,057 kwa lita, dizeli Sh4,086 na mafuta ya taa Sh4,067. Tanga, petroli itauzwa hadi Sh4,123, dizeli Sh4,152 na mafuta ya taa Sh4,133 kwa lita, huku Mtwara petroli ikiwa Sh4,170, dizeli Sh4,199 na mafuta ya taa Sh4,180 kwa lita. Kwa baadhi ya maeneo ya ndani, bei ya juu zaidi ya petroli iliyotajwa katika jedwali la EWURA ni Sh4,370 kwa lita Kyerwa (Ruberwa), Kagera, huku dizeli ikiwa Sh4,399 na mafuta ya taa Sh4,380. EWURA imewataka wafanyabiashara kuzingatia bei kikomo zilizotangazwa na imeonya kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wa...
Marato tv - Sauti ya Jamii