Skip to main content

Posts

Showing posts from July 22, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

TANZANIA TO GRACE AFRICA BEE EXPO IN ALGERIA

Tanzania has accepted an invitation to be the guest of honour at the opening of the Africa Bee Expo 2026 to be held in Algiers, Algeria, from 3-6 September, 2026. Speaking to Algerian television journalists at the Tanzanian Embassy in Algiers, Ambassador Mobhare Matinyi said the Minister of Natural Resources and Tourism, Hon. Dr. Ashatu Kijaji, will open the exhibition on behalf of the Government of the United Republic of Tanzania. Ambassador Matinyi said Hon. Minister Dr. Kijaji will pay an official visit to Algeria leading a delegation of senior government officials and experts as well as stakeholders from the private sector who are involved in the whole industry of beekeeping in the country. Ambassador Matinyi said the government attaches special importance to the beekeeping sector as it employs about two million people in the country and generates US$77.5 million (205 Tanzania billion shillings) per year from the export of honey and beeswax to various countries around the world. Ci...

TANZANIA MGENI RASMI MAONESHO YA UFUGAJI NYUKI AFRIKA NCHINI ALGERIA

 Tanzania imekubali mwaliko wa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Maonesho ya Ufugaji wa Nyuki barani Afrika yatakayofanyika jijini Algiers, Algeria, tarehe 3-6 Septemba, 2026. Akizunngumza na waandishi wa habari wa televisheni za Algeria kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini Algiers, Balozi Mobhare Matinyi alisema Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, ndiye atakayefungua maonesho hayo kwa niaba ya serikali. Balozi Matinyi alisema Mhe. Waziri Dkt. Kijaji atakuja Algeria akiongoza ujumbe wa maafisa waandamizi na wataalamu wa serikali pamoja na wadau kutoka sekta binafsi ya ufugaji wa nyuki na utengenezaji wa bidhaa za nyuki nchini. Balozi Matinyi alisema serikali inaipa sekta ya ufugaji wa nyuki umuhimu wa kipekee kwani inaajiri watu wapatao milioni mbili nchini na huingiza dola za Marekani milioni 77.5 (shilingi bilioni 205) kwa mwaka kutokana na mauzo ya asali katika nchi mbalimbali duniani. Akinukuu takwimu za serikali, Balozi Matinyi alisema Tanzania hivi sasa ni ...

MUNDE KUONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA PAMOJA WA MAWAZIRI WA UMOJA WA AFRIKA NCHINI CÔTE D’IVOIRE

 Na.Mwandishi weu CÔTE D’IVOIRE:Naibu Waziri wa Fedha, Mshamu Ali Munde, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar, ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano wa Pamoja wa 9 wa Kamati Maalum ya Mawaziri (STC) ya Umoja wa Afrika inayosimamia masuala ya Fedha, Uchumi, Mipango na Mtangamano pamoja na Mkutano wa 5 wa Kamati Maalum ya Mawaziri inayosimamia masuala ya Biashara, Utalii, Viwanda na Madini, jijini Abidjan, nchini Côte d’Ivoire kuanzia tarehe 23 hadi 24 Julai, 2026. Mkutano huo utawakutanisha Mawaziri wa Fedha, Madini, Biashara, Viwanda, Mipango ya Uchumi, Magavana wa Benki Kuu pamoja na viongozi wa taasisi mbalimbali za Umoja wa Afrika na mashirika ya kifedha ya kikanda kujadili mikakati ya kuharakisha maendeleo ya viwanda barani Afrika kupitia upatikanaji wa rasilimali fedha, biashara, uwekezaji na ushirikiano wa kiuchumi. Miongoni mwa masuala ya sekta ya fedha yatakayojadiliwa ni namna ya kuongeza wigo wa fedha za maendeleo ya viwanda, usimamizi wa deni l...

RUSHWA YATAJWA KIKWAZO CHA UTEKEKEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

 Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga  Viongozi wa halmashauri zote mkoani Tanga wakiwememo watumishi wa umma,watendaji wa taasisi pamoja na wakurugenzi wametakiwa kuwa waadilifu katika kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa na inayotarajiwa kutekelezwa mkoani humu. Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Handeni Salum Nyamwese Kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi  Dkt. Batilda Burian katika warsha ya wadau wa usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoa wa Tanga iliyoandaliwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU  iliyofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa, amewataka kuonyesha uzalendo uwajibikaji pamoja na kutokuwa sababu ya kuzuia maendeleo kupitia miradi inayotekelezwa mkoani humu. "Rushwa ni adui mkubwa wa maendeleo ya Taifa lolote, kuhujumu matumizi sahihi ya rasilimali za umma, kudhoofisha ubora wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo  na kupunguza ufanisi wa utoaji wa huduma kwa wananchi  na  kuondoa...

RAIS SAMIA NA MAHAMA WAAFIKIANA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA AFYA, MADINI NA BIASHARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Ghana, Mhe. John Dramani Mahama, katika Ikulu ya nchi hiyo Jubilee House, jijini Accra, Ghana, tarehe 22 Julai, 2026. Pamoja na mambo mengine, Rais Mhe. Dkt. Samia na Mwenyeji wake Rais Mhe. Mahama walikubaliana kuimarisha ushirikiano kwa kutekeleza kwa pamoja masuala mbalimbali ya afya.  Pia, walizungumzia ushirikiano na kubadilishana uzoefu kwenye sekta ya madini ambapo kwa upande wa Ghana asilimia 60 ya uzalishaji unafanywa na wachimbaji wadogo na asilimia 40 unafanywa na wachimbaji wakubwa, hali inayowanufaisha wananchi wa kawaida.  Kuhusu Biashara baina ya nchi mbili kuwa na muamko mdogo, waligusia kuendelea kuipa msukumo mkubwa na hasa baada ya Shirikia la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) kuanzisha safari katika ukanda huo wa Magharibi ambapo kumeanza kuchochea fursa mbalimbali za kiuchumi tofauti na awali.

MKUU WA MAJESHI NCHINI AMESEMA JWTZ LITAENDELEA KULINDA AMANI NA MIPAKA YA NCHI

 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda amelitaka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuendelea kutekeleza jukumu lake la msingi la kulinda amani na mipaka ya Taifa, ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa salama na yenye utulivu. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha Mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF CUP 2026), Jenerali Mkunda alisema michezo ni sehemu muhimu ya kujenga afya, mshikamano na utayari wa wanajeshi katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku. Mashindano hayo yalihitimishwa kwa mchezo wa fainali uliowakutanisha DFHQ na JKT, ambapo timu ya JKT iliibuka bingwa baada ya kuifunga DFHQ kwa mabao 3-1 katika mchezo ulioshuhudiwa na viongozi mbalimbali wa jeshi pamoja na wadau wa michezo. Aidha, Jenerali Mkunda amewaasa wanamichezo hao kuendelea kujitunza, kujiweka katika kiwango bora cha utimamu wa mwili na kuzingatia nidhamu pamoja na sheria za michezo wanaposhiriki mashindano ya ndani na yale ya kimataifa. K...

RAIS SAMIA AHIMIZA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA AFYA, BARANI AFRIKA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa wito kwa nchi za Afrika kuongeza uwekezaji wa ndani katika sekta ya afya ili kujenga mifumo imara, endelevu na inayojitegemea katika usimamizi wa sekta hiyo. Rais Dkt. Samia ametoa wito huo leo, tarehe 22 Julai, 2026 alipohutubia Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Afya, uliofanyika jijini Accra, nchini Ghana. Mkutano huo umejadili namna ya kuharakisha utekelezaji wa Ajenda ya Afya ya Afrika kupitia usawa katika upatikanaji wa huduma, afya kwa wote, kutokomeza UKIMWI, kuboresha afya ya mama na mtoto, pamoja na kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza na yasiyopewa kipaumbele. Amesema Tanzania tayari imeanza kutekeleza Ramani ya Afya ya Umoja wa Afrika 2030 kwa kuiingiza katika Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa 2026/2027-2030/2031, huku ikijielekeza kwenye uwekezaji katika uzalishaji wa dawa, kuimarisha mifumo ya afya na kuongeza uwezo wa nchi kujitegem...

KAMATI YA KITAIFA YA USIMAMIZI WA MAAFA YAIDHINISHA MPANGO WA DHARURA WA TAIFA WA KUKABILIANA NA MADHARA YA EL NIÑO

 Na.Mwandishi wetu - Dar es Salaam Kamati ya Kitaifa ya Wataalamu ya Usimamizi wa Maafa imeidhinisha Mpango wa Taifa wa Dharura wa Kukabiliana na Madhara ya El Niño na kuzielekeza Wizara, Idara, Taasisi, Mikoa na Halmashauri kuongeza kasi ya maandalizi ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua za El Niño zinazotabiriwa kudumu hadi mwisho wa mwaka 2026. Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Dkt. Jim Yonazi, ameelekeza kila sekta kutenga rasilimali zitakazowezesha hatua za kuzuia, kujiandaa, kukabili na kurejesha hali katika eneo lake na pia kuandaa mipango ya dharura ya manunuzi. Pia amesisitiza umuhimu wa kutambua mapema maeneo hatarishi, kufanya tathmini za vihatarishi na kuwahamasisha wananchi wanaoishi katika maeneo hayo kuhamia maeneo salama. Aidha, Dkt. Yonazi ameelekeza wananchi kupewa elimu kuhusu namna ya kupunguza madhara ya mvua hizo kwa kuweka ...

AGIZO LA RC LATEKELEZWA: FAMILIA YA RUHUMBIKA KASANJE YALIPWA FIDIA

Familia ya Ndugu Ruhumbika Machumu Kasanje, mkazi wa Kijiji cha Chirorwe aliyekuwa anaidai fidia Kampuni ya Wakazi Mining Limited imelipwa kufuatia maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi aliyoyatoa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji hicho jana tarehe 21 Julai, 2026.  Akizungumza leo tarehe 22 Julai, 2025 baada ya familia hiyo kulipwa fidia na kuhama katika eneo hilo, Mhe. Mtambi amepongeza hatua hiyo kwa kuwa inamaliza mgogoro uliodumu kwa muda mrefu na kuyaondoa maisha ya familia hiyo katika hatari za kiusalama baada ya baadhi ya watu waliokuwa wamepata ajira kwenye mgodi huo kuifanyia vurugu za kuharibu mazao ya familia hiyo baada ya mgodi huo kufungwa.  “Kulipwa kwa fidia hiyo kunatuwezesha kuufungua tena mgodi huo uendelee na shughuli zake za kawaida za uchimbaji wa madini ambapo watu zaidi ya 400 wamepata ajira na maisha yao yanategemea mgodi huo” amesema Mhe. Mtambi.  Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Mhe. Mtambi alit...