MBUNGE wa Jimbo la Bunda Mjini, Mhe. Ester Bulaya, amewapeleka Madiwani wa Jimbo hilo katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ziara maalum ya kujifunza shughuli za utalii, uhifadhi na fursa za kiuchumi zinazotokana na sekta hiyo. Ziara hiyo imelenga kuwawezesha Madiwani hao kujionea kwa vitendo utajiri wa wanyamapori na vivutio mbalimbali vilivyopo Serengeti, pamoja na kupata uelewa mpana kuhusu namna sekta ya utalii inavyoweza kuchangia maendeleo ya wananchi. Kupitia ziara hiyo, Madiwani wamepata fursa ya kujifunza umuhimu wa uhifadhi wa rasilimali za nchi na namna fursa za utalii zinavyoweza kuibuliwa, kuendelezwa na kutumiwa kama kichocheo cha shughuli za kiuchumi katika maeneo yao. Mhe. Bulaya amesisitiza umuhimu wa kuitangaza Bunda Mjini na maeneo jirani kama sehemu yenye fursa za utalii, akieleza kuwa hatua hiyo inaweza kusaidia kuongeza shughuli za kiuchumi, ajira na kipato kwa wananchi. Amesema viongozi wanapaswa kuwa na uelewa mpana kuhusu fursa zilizopo katika maeneo ya...
Marato tv - Sauti ya Jamii