Skip to main content

Posts

Showing posts from July 8, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

NEST YANG'ARA DUNIANI, YATWAA TUZO YA MIFUMO 20 BORA YA SERIKALI MTANDAO

   Mfumo wa Usimamizi wa Ununuzi wa Umma Kielektroniki (NeST) umeendelea kuiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia baada ya kutunukiwa tuzo ya kimataifa na kutambuliwa kuwa miongoni mwa mifumo 20 bora ya Serikali Mtandao duniani katika Tuzo za World Summit on the Information Society (WSIS) Prizes 2026, zilizofanyika Julai 8, 2026 jijini Geneva, Uswisi. Tuzo hiyo ilikabidhiwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Dennis Simba, na Mratibu Mkuu wa Tuzo za WSIS, Bi. Gitanjali Sah, aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Mawasiliano (ITU). Kwa mujibu wa ITU, NeST ilishinda katika kategoria ya Serikali Mtandao (e-Government), iliyoshirikisha zaidi ya mifumo 1,500 kutoka nchi 122 duniani. Mifumo hiyo ilitathminiwa kwa mchango wake katika kuimarisha uchumi shirikishi, ustawi wa jamii na maendeleo endelevu kupitia matumizi ya teknolojia. Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Bw. Dennis Simba amesema mafanikio hayo yametokana na maono n...

NEST YANG'ARA DUNIANI, YATWAA TUZO YA MIFUMO 20 BORA YA SERIKALI MTANDAO

 Mfumo wa Usimamizi wa Ununuzi wa Umma Kielektroniki (NeST) umeendelea kuiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia baada ya kutunukiwa tuzo ya kimataifa na kutambuliwa kuwa miongoni mwa mifumo 20 bora ya Serikali Mtandao duniani katika Tuzo za World Summit on the Information Society (WSIS) Prizes 2026, zilizofanyika Julai 8, 2026 jijini Geneva, Uswisi. Tuzo hiyo ilikabidhiwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Dennis Simba, na Mratibu Mkuu wa Tuzo za WSIS, Bi. Gitanjali Sah, aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Mawasiliano (ITU). Kwa mujibu wa ITU, NeST ilishinda katika kategoria ya Serikali Mtandao (e-Government), iliyoshirikisha zaidi ya mifumo 1,500 kutoka nchi 122 duniani. Mifumo hiyo ilitathminiwa kwa mchango wake katika kuimarisha uchumi shirikishi, ustawi wa jamii na maendeleo endelevu kupitia matumizi ya teknolojia. Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Bw. Dennis Simba amesema mafanikio hayo yametokana na maono na uongo...

WAKAGUZI WA MAHESABU WAYATUMIE MAFUNZO YA MABADILIKO SHERIA ZA KODI KULETA UFANISI UKUSANYAJI KODI

 NA: DK. REUBENI LUMBAGALA  Julai 1, 2026, serikali imeanza utekelezaji wa bajeti mpya kwa mwaka wa fedha 2026/2027. Yale yaliyopangwa na serikali na kujadiliwa na wabunge na hatimaye yakaafikiwa katika bajeti hiyo, yameanza kufanyiwa kazi ili kufanikisha mipango ya maendeleo. Wizara ya Fedha kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekuja na mabadiliko mbalimbali ya kodi. Mabadiliko haya yamelenga kuleta mageuzi, ufanisi na hatimaye kuongeza mapato bila kumuumiza mlipakodi ambaye ni mdau muhimu katika mipango ya maendeleo.  Kwahiyo, kutokana na mabadiliko hayo, TRA pamoja na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), wameratibu mafunzo kwa wahasibu, wakaguzi, wataalamu wa fedha na washauri wa kodi ili kuwajengea uwezo wa mabadiliko hayo ili ukusanyaji kodi ufanyike kwa ufanisi. Hivyo basi, baada ya kupata mafunzo hayo, watakuwa na jukumu la kwenda kwa walipakodi na wananchi kuwaelimisha juu ya mabadiliko hayo ili kujenga uelewa wa pamoja ili yale yaliyopang...

TUNALIPA JANA YA PSSSF, IMEFUTA MACHOZI KWA WASTAAFU

 NA: DK. REUBENI LUMBAGALA Miongoni mwa haki za msingi za mfanyakazi serikalini au sekta binafsi ni pamoja na kulipwa mafao yake kwa wakati pindi anapostaafu utumishi wake. Mafao hayo yanatokana na michango aliyochangia katika mifuko ya hifadhi ya jamii kutoka kwenye makato ya mshahara wake pamoja na michango ya mwajiri wake. Kwahiyo, mfanyakazi anapomaliza muda wa utumishi wake eidha kwa kustaafu kwa hiari au kwa lazima, mifuko ya hifadhi ya jamii inapaswa kumlipa mafao yake ili kuendeleza maisha mengine, kwani maisha lazima yaendelee hata baada ya kustaafu. Kwa muda mrefu, kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya wastaafu kucheleweshewa kulipwa mafao yao, ambayo kama nilivyoeleza awali ni haki yao ya msingi na si hisani. Kwa ufupi, wanastahili kulipwa bila usumbufu wowote. Kucheleweshewa mafao ya wastaafu kumesababisha usumbufu mkubwa kwa wastaafu, na hata kuwasababishia msongo wa mawazo kwa kujiuliza kwani kustaafu ni kosa la jinai hadi kusumbuka kiasi hicho?  Ni faraja kuona k...

RC MHITA AITAKA MSALALA KUFUNGA HOJA ZA CAG KWA WAKATI

MSALALA, SHINYANGA  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, ameielekeza Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kuhakikisha inatekeleza kwa wakati mapendekezo yote yaliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), akisisitiza kuwa hatua hiyo itaimarisha uwajibikaji, uwazi na matumizi sahihi ya rasilimali za umma. Mhe. Mhita ametoa maelekezo hayo leo, Julai 8, 2026, wakati akifungua Baraza Maalumu la kujadili na kupitia hoja za ukaguzi wa CAG kwa mwaka wa fedha ulioshia Juni 30, 2026, lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala. Amesema utekelezaji wa hoja za CAG si suala la hiari, bali ni wajibu wa kila taasisi ya umma kuhakikisha dosari zilizobainishwa zinarekebishwa kwa wakati ili kuongeza ufanisi wa usimamizi wa fedha za Serikali na kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi. "Hoja za CAG zinapaswa kutazamwa kama fursa ya kuboresha utendaji wetu. Hakikisheni kila hoja inafanyiwa kazi kwa wakati na kufungwa kwa mujibu wa taratibu," amesis...

BALOZI WA AMANI ASIFIA UTULIVU ULIOJITOKEZA MWANZA

 Balozi wa Amani Tanzania na Katibu wa Mahusiano wa Jumuiya ya Wachimbaji Tanzania (FEMATA), Mess Chengula, amepongeza hali ya amani na utulivu iliyoendelea kutawala jijini Mwanza, akisema ndiyo msingi wa maendeleo na ustawi wa wananchi. Akizungumza leo baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ya jiji hilo, Chengula alisema ameridhishwa kuona shughuli za kijamii na kiuchumi zikiendelea, huku baadhi ya maduka yaliyokuwa yamefungwa yakifunguliwa tena na kuanza kutoa huduma. "Ninawapongeza Watanzania kwa kuchagua amani siku hii ya leo. Furaha kubwa kwa binadamu ni kuona amani ikitawala mioyoni mwa watu," amesema. Aidha, aliiomba Serikali kuendelea kusikiliza makundi mbalimbali yenye malalamiko ili kutatua changamoto kwa njia ya mazungumzo na kuimarisha utulivu nchini. Chengula amesema amani huwezesha wananchi kujishughulisha kwa uhuru katika shughuli za uzalishaji mali, huku akisisitiza kuwa maridhiano yanayotarajiwa kufanywa kati ya Serikali, vyama vya siasa na makundi mbalimbali ...

AKIMWAKILISHA DKT.POSSI KATIKA MKUTANO WA WIPO,BALOZI TEMU ASISITIZA MAREKEBISHO YA MIFUMO YA MALI MILIKI

Na Mwandishi Wetu Geneva – Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Geneva ametoa wito wa kuwa na mifumo ya mali miliki (Intellectual Property)inayojumuisha wote, yenye usawa na inayolenga mustakabali ili kuchochea ubunifu na maendeleo endelevu. Akizungumza katika Mkutano wa 68 wa Mabaraza ya Nchi Wanachama wa Shirika la Kimataifa la Mali Miliki WIPO, Balozi Temu aliwashukuru Mwenyekiti na Makamishna wenzake kwa uongozi wao. Pia alimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa WIPO, Bw. Daren Tang, kwa kuteuliwa tena na kuipongeza Sekretarieti kwa maandalizi bora ya mkutano huo. Tanzania iliungana na tamko lililosomwa na Afrika Kusini kwa niaba ya Nchi za Afrika na Nepal kwa niaba ya Nchi Zinazoendelea. Balozi Temu, ambaye alikuwa anamwakilisha Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa na Mashirika mengine ya Kimataifa Geneva, Mhe. Dkt. Abdallah S. Possi, alisema Tanzania inatambua mali miliki kama kichocheo muhimu cha ubunifu, viwanda na maend...

REPRESENTING DR.POSSI, AMBASSADOR TEMU CHAMPIONS INTELLECTUAL PROPERTY SYSTEMS REFORM

  By Prosper Makene  Geneva- Deputy Permanent Representative of the United Republic of Tanzania to the United Nations in Geneva has called for inclusive, balanced, and future-oriented intellectual property systems to drive innovation and sustainable development. Addressing the 68th Series of Meetings of the Assemblies of Member States of WIPO, Ambassador Temu thanked the Chairperson and Vice-Chairs for their leadership. She also congratulated WIPO Director General Mr. Daren Tang on his re-appointment and commended the Secretariat for excellent preparations. Tanzania aligned itself with statements delivered by South Africa on behalf of the African Group and Nepal on behalf of the Least Developed Countries. Ambassador Temu, who represented the Permanent Representative of Tanzania to the United Nations and other international organizations in Geneva, H.E. Dr. Abdallah S. Possi, said Tanzania recognizes intellectual property as a strategic driver of innovation, creativity, industr...

DKT. KIRUSWA: MAGEUZI SEKTA YA MADINI YAIFANYA TANZANIA KUWA KITOVU CHA UWEKEZAJI AFRIKA*

🔶_Tume ya Madini yaeleza usimamizi wa leseni za madini na Local Content unavyowanufaisha Watanzania_ 🔶_Fursa za uwekezaji zatangazwa kuanzia utafiti, uchimbaji hadi uongezaji thamani wa madini_ 📍Dar es Salaam Serikali imesema mageuzi yanayoendelea kutekelezwa katika sekta ya madini chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yameifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye mazingira bora ya uwekezaji barani Afrika, huku ikiwakaribisha wawekezaji kuwekeza katika utafiti, uchimbaji, uchenjuaji, uchakataji na uongezaji thamani wa madini. Kauli hiyo imetolewa leo, Julai 8, 2026, na Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Steven Kiruswa, wakati akifungua Kongamano la Madini lililofanyika katika Ukumbi wa Dome, ndani ya Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), maarufu Sabasaba. Dkt. Kiruswa amesema maboresho ya sera, sheria na mifumo ya usimamizi wa sekta ya madini yameongeza uwazi, uwajibikaji na ushiriki wa sekta binafsi, hatua zilizochochea ongezeko la uwekezaji...

BARABARA YA MZUNGUKO DODOMA MWAROBAINI MSONGAMANO WA MAGARI

▪️ Madereva Waeleza Inavyorahisisha Safari ▪️Wafanyabiashara Washerehekea *Na Adelina Johnbosco – MAELEZO* Barabara za Mzunguko Jijini Dodoma imechangia kwa kiasi kikubwa kuondoa msongamano wa magari katikati ya jiji, hususan magari makubwa ya mizigo ya ndani na yanayokwenda nchi za nje. Mradi huu wa barabara ya njia nne kwa kiwango cha lami una urefu wa jumla ya kilometa 112.3 huku sehemu ya kwanza (lot 1) yenye kilometa 52.3 ikiwa imekamilika kwa asilimia 93.3. Barabara hii imeunganisha barabara kuu za mikoa minne, bandari kavu Ihumwa - Morogoro, Veyula - Arusha, Nala - Singida na Matumbulu – Iringa ambako sehemu ya pili ya ujenzi (lot 2) inaanzia. Shughuli za usafiri na usafirishaji tayari zimeanza katika barabra hiyo, watumiaji wanashuhudia urahisi wa safari kutokana na kutokuwepo foleni.  “Imeturahisishia sana, inafanya safari iwe fupi kutokana na ukweli kwamba njia hii haina foleni hata kidogo kama kule mjini kati, mwanzoni kutoka Ihumwa hadi Nala ilikuwa tunatumia takribani ...

WAZIRI MKUU AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA KAMPUNI YA ALSTOM.

_▪️Yaonesha nia ya kushirikiana na Serikali katika usafiri ya Mijini._ _▪️Dkt. Mwigulu awahakikishia mazingira bora ya uwekezaji_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amekutana na Makamu wa Rais wa Kampuni ya ALSTOM ya nchini Ufaransa, Philippe Deller ambapo wamejadiliana kuhusu fursa za uwekezaji katika sekta ya miundombinu ya usafiri nchini Tanzania. Katika mazungumzo hayo, Dkt. Mwigulu Nchemba aliikaribisha ALSTOM kuwekeza nchini, akieleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji na kutekeleza mageuzi yanayolenga kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara, usafiri na uwekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki. Kwa Upande wake Bw. Phillepe alieleza nia ya kampuni hiyo kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya usafiri wa mijini. Kampuni hiyo imeonesha utayari wa kuwekeza katika ujenzi wa mifumo ya usafiri wa haraka na miundombinu ya kisasa yenye leng...