Skip to main content

Posts

Showing posts from May 26, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

ZIARA YA MADIWANI KIBAHA YAFUNGUA FURSA MPYA ZA KUONGEZA MAPATO

MADIWANI wa Manispaa ya Kibaha wameeleza kuwa ziara yao ya mafunzo katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya na Halmashauri ya Mji Tunduma italeta manufaa makubwa katika kuongeza mapato na kuimarisha miradi ya maendeleo ya Manispaa hiyo. Akizungumza baada ya ziara hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha, Dkt. Mawazo Nicas amesema madiwani pamoja na wataalamu wa halmashauri wamepata uzoefu mkubwa kuhusu usimamizi wa mapato na uendeshaji wa vitega uchumi vinavyochangia maendeleo ya wananchi. Amesema katika Jiji la Mbeya wamejifunza namna miradi ya ujenzi wa maduka, ukumbi pamoja na maeneo ya mapumziko inavyoongeza mapato ya halmashauri na kutoa huduma bora kwa wananchi na wafanyabiashara. Kwa upande wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Dkt. Nicas amesema wamevutiwa na mfumo wa parking za malori unaochangia mapato makubwa ya Halmashauri hiyo kutokana na shughuli za biashara mpakani mwa Tanzania na Zambia. “Tumepata mambo mengi ya kujifunza. Tumeona namna parking za malori zinavyoongeza mapato Tundu...

KAMPUNI YA AMBONI YABOMOA NYUMBA ZA KAYA 67, MWANAFA ALAANI

📍Wananchi waachwa wakilala nje kwenye baridi, mwekezaji adaiwa kugomea wito wa Mkuu wa Mkoa Na Mwandishi Wetu, Muheza KAMPUNI ya Amboni Plantation imewabomolea nyumba na kuwaacha wakilala nje kwenye baridi wananchi wa kaya 67, katika kitongoji cha Maisha Plus kilichopo kata ya Kigombe, wilayani Muheza mkoani Tanga. Uharibifu huo wa dharura umefanyika Ijumaa iliyopita katika Kijiji cha Mshakangoto, ambapo kampuni hiyo inayolima mkonge imetumia uamuzi wa mahakama kuondoa familia hizo, ambazo nyingi ni za vibarua na wastaafu wa shamba hilo. Mbunge wa Muheza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma (MwanaFA), alitembelea eneo hilo Leo Mei 26 kushuhudia uharibifu huo na kulaani kitendo hicho akikitaja kuwa ni unyama uliokosa utu. Mhe. Mwinjuma alifichua kuwa, baada ya mwekezaji huyo kushinda kesi, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batlida Burihan alimwita mwekezaji ili kuweka utaratibu wa kiungwana wa kuwahamisha wananchi lakini hakupatikana kwa simu zake ...

JMAT:TANZANIA IMEBAKI KISIWA CHA AMANI NA UMOJA WA KIDINI

Katibu wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Askofu Israel Maasa, amesema Tanzania imeendelea kudumisha amani, mshikamano na uhuru wa kuabudu kwa zaidi ya nusu karne, hali iliyowafanya wananchi wa dini mbalimbali kuishi kwa upendo na ushirikiano mkubwa. Askofu Maasa amesema Watanzania wamekuwa wakishirikiana katika shughuli za maendeleo, kufanya biashara pamoja, kujenga urafiki na hata kuoana kati ya familia za dini tofauti bila kuwepo migogoro ya kidini. Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 26, 2026 jijini Dodoma, amesema hali hiyo imeifanya Tanzania kuwa miongoni mwa mataifa yenye utulivu mkubwa barani Afrika. “Tuhuma na shutuma dhidi ya uwepo wa ubaguzi wa kidini nchini Tanzania zimetusikitisha, kutukasirisha na kutufedhehesha,” amesema Askofu Maasa. Amesema hata raia wa Marekani wanaoishi Tanzania ni mashahidi wa namna uhuru wa kuabudu unavyoheshimiwa na kuimarika nchini. “Hatutaki kuamini kwamba Marekani, taifa ambalo tuliungana nalo katika majonzi wakati wa mas...

JMAT:YATOA ONYO KWA MAREKANI KWA KAULI ZA UDINI TANZANIA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Sheikh Alhad Mussa Salum, ameibuka na kulaani vikali kauli za baadhi ya maseneta wa Bunge la Marekani waliodai kuwa Tanzania si salama na kwamba kuna ubaguzi wa kidini dhidi ya baadhi ya waumini nchini. Akizungumza leo Mei 26, 2026 jijini Dodoma katika mkutano wa waandishi wa habari ulioandaliwa na JMAT, Sheikh Alhad amesema madai hayo ni ya uongo, uchochezi na hayana uhalisia wowote ndani ya Tanzania. JMAT ni jumuiya inayounganisha madhehebu mbalimbali ya dini za Kiislamu, Kikristo pamoja na dini nyingine nchini kwa lengo la kuimarisha amani, maridhiano na mshikamano wa Taifa. “Uwepo wetu hapa leo ni ushahidi wa wazi kwamba Tanzania hakuna udini. Tunaitaka Serikali ya Marekani iwakemee maseneta hao mara moja na kueleza wazi kuwa kauli hizo ni maoni yao binafsi,” amesema Sheikh Alhad. Amesema Watanzania wamejenga maisha ya upendo, umoja na kuheshimiana kwa miaka mingi bila kujali tofauti za dini, jambo ambalo limeendelea kui...

WIZARA YA MAMBO YA NJE YAOMBA BILLIONI 358.36 KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2027

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeomba kuidhinishiwa jumla ya shilingi bilioni 358.36 kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake katika mwaka wa fedha 2026/2027. Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amesema wizara hiyo pia inatarajia kukusanya maduhuli ya Serikali yenye thamani ya shilingi bilioni 1.511 kutoka katika vyanzo mbalimbali vinavyosimamiwa na makao makuu ya wizara pamoja na balozi za Tanzania zilizopo nje ya nchi. Amefafanua kuwa vyanzo hivyo vya mapato ni pamoja na upangishaji wa nyumba za Serikali zilizopo nje ya nchi, upangishaji wa kumbi za mikutano pamoja na huduma za uthibitishaji wa nyaraka mbalimbali kama vyeti vya elimu, vyeti vya ndoa, hati za talaka na nyaraka nyingine rasmi. Kwa mujibu wa makadirio hayo, wizara imepanga kutumia jumla ya shilingi bilioni 358.36, ambapo kati ya hizo shilingi bilioni 312 zitaelekezwa katika ...

BULAYA:TANZANIA NI NCHI HURU ISIINGILIWE NA MATAIFA MENGINE

Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini mkoani Mara, Esther Bulaya amesema Tanzania ni nchi huru na haiwezi kuingiliwa na mataifa mengine, huku akisisitiza kuwa ushirikiano wa kimataifa lazima uzingatie maslahi ya Taifa. Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki bungeni jijini Dodoma, Bulaya amesema Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuimarisha diplomasia ya kimataifa na kuimarisha mahusiano na mataifa mbalimbali duniani. Amesema hatua hiyo imeongeza heshima na ushawishi wa Tanzania katika jukwaa la kimataifa, pamoja na kuleta manufaa katika sekta za uchumi, ulinzi na maendeleo ya kijamii. Aidha, Bulaya amesisitiza kuwa licha ya Tanzania kunufaika na ushirikiano wa kimataifa, Serikali ina wajibu wa kulinda haki na maslahi ya Watanzania wakati wote. Ameeleza kuwa  kuwa Tanzania itaendelea kuwa mshirika mwema wa mataifa mengine, lakini itaweka mbele maslahi ya Taifa katika kila hatua ya ushirikiano wa kimataifa. Bulaya amesema kuwa ...

Diaspora Waongeza Uwekezaji Hadi Billion 11.7 Nchini

Serikali imefanikiwa kuimarisha ushiriki wa Watanzania wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) katika uchumi wa taifa, baada ya kuwekeza zaidi ya shilingi bilioni 11.7 kupitia Mfuko wa Uwekezaji wa UTT AMIS hadi Februari 2026, kutoka shilingi bilioni 7.5 zilizowekezwa mwaka uliopita. Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi Leo Mei 26,2026 Bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo ametoa Takwimu hizo kwa mwaka wa fedha 2026/2027, zikionesha ongezeko la imani ya diaspora katika mifumo rasmi ya uwekezaji nchini. Balozi Kombo ameeleza kuwa ongezeko hilo linatokana na jitihada za kimkakati za kuhamasisha taasisi za kifedha kutoa huduma mahsusi kwa Watanzania wa diaspora, lengo likiwa ni kuongeza ushiriki wao katika maendeleo endelevu ya taifa. Katika hatua hiyo, akaunti maalum za diaspora zimeanzishwa katika benki sita ambazo ni TCB, CRDB, NBC, NMB, Azania na Absa, hatua inayorahisisha uwekezaji, utunzaji wa fedha na uhawilis...

BUTIAMA WALIA TAA ZA BARABARANI, SERIKALI YATOA MAJIBU

MBUNGE wa Jimbo la Butiama, Mhe. Dkt. Charles Mahera, ameiiomba Serikali kuharakisha uwekaji wa taa za barabarani katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo yanayopitiwa na barabara ya Mkutano,Natta kupitia Nyamwisuwa. Akizungumza bungeni jijini Dodoma Mei 26, 2026 wakati akiuliza swali la nyongeza, Dkt. Mahera amesema barabara hiyo ilianza kujengwa muda mrefu huku kipande cha Mkutano hadi Nyamwisuwa kikikamilika tangu mwaka 2007, lakini wananchi bado hawajanufaika na huduma ya taa za barabarani. “Barabara hii inapitia maeneo mengi sana ya Jimbo la Butiama lakini maeneo hayo hayana taa kuanzia Nyambange, Nyakanga, Butuguri, Mbusegwe, Kiguri, Kiarano hadi Bisale. Wananchi wa Butiama wanasubiri taa hizi kwa muda mrefu tangu mwaka 2023,” amesema Dkt. Mahera. Dkt. Mahera  ameiomba Serikali kuhakikisha wananchi wa Butiama wanapatiwa huduma hiyo muhimu ili kuongeza usalama pamoja na kuchochea shughuli za kijamii na kiuchumi katika maeneo hayo. Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhan...

MBUNGE MARY AENDELEA KUWAPA TABASAMU WANANCHI WA SERENGETI

 Mbunge wa Jimbo la Serengeti, Mary Daniel Surati, ameendelea kuweka historia ya maendeleo katika jimbo hilo baada ya kutoa na kugawa shilingi milioni 88 kwa ajili ya miradi ya huduma za kijamii. Mary alitoa fedha hizo kupitia Mfuko wake wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo, katika hafla maalum iliyofanyika Mei 20, 2026 wilayani Serengeti na kuhudhuriwa na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, viongozi wa serikali na wananchi. Mbunge huyo alisisitiza dhamira yake ya kuhakikisha wananchi wa Serengeti wanapata huduma bora za afya, elimu na maendeleo ya kijamii kwa ujumla. Katika mgao huo wa fedha, kiasi cha shilingi milioni 25 kimetengwa kwa ajili ya kugharimia ukamilishaji wa Zahanati ya Kisaka, mradi unaotarajiwa kuongeza upatikanaji wa huduma za afya kwa wakazi wa eneo hilo na kupunguza adha ya wananchi kusafiri umbali mrefu kufuata matibabu. Mbunge Mary akikabidhi hundi ya mfano ya milioni 25/- Mbali na fedha hizo, Mbunge Mary pia alikabidhi madawati kadhaa yenye thamani ya shilingi...

TRA Mkoa wa Kagera Yakusanya Billions 55

Mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa Kagera kwa kipindi cha miezi mitatu Januari hadi Machi mwaka huu wamevuka lengo la ukusanyaji mapato na kukusanya shilingi bilioni 55. Meneja wa TRA mkoa wa Kagera CPA Joseph Mutalemwa ametoa takwimu hizo Mei 26,2026 katika maonyesho ya elimu ya juu kupitia bodi ya mikopo (HESLB) yanayoendelea katika viwanja vya soko kuu mjini Bukoba. Amesema kuwa, Mamlaka hiyo katika kipindi cha miezi mitatu Januari hadi Machi mwaka huu walipanga kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 51 lakini wamevuka lengo hilo na kukusanya shilingi  bilioni 55. Ameeleza kuwa, kupanda kwa lengo hilo kumetokana na elimu ambayo wamekuwa wakitoa maeneo mbalimbali mkoani humo ambayo imesaidia wafanyabiashara kulipa kodi yao bila shuruti. Mutalemwa amewashauri wafanyabiashara kuwasirisha ritani zao kwa maana ya hesabu za biashara ili kuangalia kiasi cha kodi wanachokilipa kwa mwaka husika kama kinalingana na kiasi cha kodi wanachopaswa kulipa. “Sheria imeweka uhuru kwamba kabla y...