Skip to main content

Posts

Showing posts from November 14, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

WANAFUNZI WATAKIWA KUWA MABALOZI WA USALAMA BARABARANI

Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma kupitia Dawati la Elimu kwa Umma limewataka wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Dodoma kuzingatia usalama barabarani wakati wa likizo ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. Akizungumza na wanafunzi hao Novemba 13, wakati shule hiyo ikifunga muhula Sajenti Ester Makali kutoka Ofisi ya Kamanda wa Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma (RTO) alisema likizo si sababu ya wanafunzi kusahau sheria na kanuni za barabarani. “Barabara ni eneo la kuwafikisha kwenye ndoto zenu, endeleeni kuzingatia kanuni na sheria za usalama barabarani,” alisema. Kuhusu usalama wakati wa mvua, Sajenti Makali aliwataka wazazi kuwavalisha watoto mavazi yanayoonekana kwa urahisi pale wanapotumwa dukani au sehemu nyingine hasa kukiwa na mawingu na mwanga hafifu ili madereva waweze kuwaona kwa urahisi wanapovuka barabara. Aidha, aliwasisitiza wanafunzi kuvuka barabara kwenye vivuko salama na pale wanapotumia vivuko vya kujitegemea visivyo na zebra wawe makini za...

WANANCHI MBULU KUNUFAIKA NA MITUNGI 3,255 YA GESI KWA BEI NAFUU

📌 *Nishati safi ya kupikia kwa kila Mtanzania* 📍 *Mbulu, Manyara* Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndugu Abubakar Kuuli kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo na wananchi, amepokea rasmi Mradi wa Usambazaji na Uuzaji wa Mitungi ya Gesi ya kilo sita kwa Bei ya Ruzuku, unaolenga kuongeza upatikanaji na matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wananchi wa wilaya hiyo. Mradi huo ni sehemu ya mwendelezo wa utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia, ambao unalenga kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia, hatua inayolenga kupunguza utegemezi wa nishati zisizo safi na kulinda afya za wananchi pamoja na mazingira. Mradi huo unatekelezwa na kusimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kupitia kampuni ya Manjis Logistics Limited, ambayo imepewa jukumu la kusambaza na kuuza jumla ya mitungi 3,255 ya gesi kwa bei ya ruzuku katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Mbulu. Aidha, katika mradi huu mwana...
  NaMwanamkuu Mwandoro, Tanga. WANANCHI mkoani Tanga na mikoa jirani wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika uchunguzi wa awali na matibabu ya upasuaji kwa atakaebainika na  changamoto ya Busha/Ngirimaji bila malipo kuanzia Novemba 16 hadi 30,2026. Akizungumza na waandshi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi. Dkt. Batilda Burian amesema  serikali imeandaa Kambi maalimu kwajili ya kuwafikia wananchi wengi wenye changamoto hiyo ili kuweza kupatiwa matibabu kwa urahisi,pia matibabu hayo yanatarajiwa kutolewa katika wilaya tatu za mkoa huu ambazo ni Handeni, Muheza na Korogwe. Aidha Dkt. Batilda amesema ugonjwa wa ngirimaji husababishwa na vimelea vinavyoenezwa kwa binadamu kupitia kung'atwa na mbu waliobeba vimelea vya maambukizi, hali inayoweza kusababisha kuvimba kwa sehemu mbalimbali za mwili kutokana na kuziba kwa mfumo wa limfu. Ameongeza kuwa madhara ya ugonjwa huo yanaweza kuathiri afya za waathirika, shughuli zao za kiuchumi, ustawi wa familia na maisha ya kijamii,...

BODABODA WALIOPATA LESENI WAMETAKIWA KUWA MABALOZI WAZURI WA USALAMA BARABARANI.

  Na Mwanamkuu Mwandoro,Tanga VIJANA wa bodaboda waliohitimu mafunzo ya udereva na kupata leseni wametakiwa kuwa mabalozi wazuri wa usalama barabarani kwa kuwahamasisha wenzao ambao bado hawajapata mafunzo ya elimu ya usalama barabarani na ambao hawana leseni kwenda kupata elimu na kufuata sheria za barabarani. Wito huo umetolewa  na kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga Almachius Mchunguzi wakati wa hafla fupi ya kukabidhi leseni za udereva kwa vijana 42 waliofanikiwa kukamilisha mafunzo katika Chuo cha Udereva cha Bandiwe, yaliyofadhiliwa na Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Tanga. Akizungumza katika hafla hiyo, Kamanda Mchunguzi amesema vijana hao wana nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko katika sekta ya usafiri wa bodaboda kwa kuwa mfano bora kwa wenzao, hususan wale ambao bado wanaendesha vyombo vya moto bila kuwa na leseni. Aidha mchunguzi ameongeza kuwa kuendesha pikipiki bila kuwa na leseni ni hatari kwa dereva mwenyewe na watumiaji wengine wa barabara, hivyo ni muhimu mader...