SENGEREMA YAFIKIA ASILIMIA 97 YA UTOAJI WA CHAKULA KWA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI ZAFIKIA ASILIMIA 75
Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema imefikia asilimia 97 ya utekelezaji wa mpango wa utoaji wa chakula kwa shule za msingi 123, huku shule za sekondari 59 zikifikia asilimia 75 katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2026, hatua inayolenga kuimarisha afya, lishe na mazingira bora ya kujifunzia kwa wanafunzi. Mafanikio hayo yamebainishwa katika kikao cha Kamati ya Lishe ya Wilaya ya Sengerema kilichofanyika kwa lengo la kupitia na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za lishe katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027. Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli hizo, Afisa Lishe wa Halmashauri hiyo, Bi. Neema Sappy, amesema mpango wa utoaji wa chakula shuleni unaendelea vizuri, huku mwitikio wa wazazi katika kuchangia chakula kwa ajili ya watoto wao ukiendelea kuridhisha. Amesema ushiriki wa wazazi ni muhimu katika kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula wanapokuwa shuleni, hivyo amewahimiza kuendelea kutimiza makubaliano yaliyofikiwa katika vikao vya kamati za shul...