Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga Mfumo wa maktaba mtandao umekuwa na matokeo chanya kwa bodi ya huduma za maktaba kwani utarahisisha kusomana na mifumo mingine kama anavyosisitiza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan kuhusu mifumo kusomana na tayari ndani yake kuna mifumo kadhaa ya kiserikali kama mfumo wa malipo ya serikali,madeni ya serikali na mingineyo,pia mifumo ya elimu kama mfumo wa takwimu ambao upo chini ya wizara ya elimu. Hayo yamebainishwa na Mkurungenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB) Dkt. Mboni Ruzegea alipokuwa akitolea ufafanuzi juu ya kuanzishwa Kwa Maktaba mtandao na kuanza kufanya kazi kwake alipokuwa katika viwanja vya usagara yalipouwa yakifanyika maonesho ya kitaifa ya wiki ya elimu ujuzi na ubunifu. Ruzegea pia amewataka watunzi wa vitabu au majarida kuhakikisha wanafika katika Maktaba kuu ya taifa na kuatiwa namba ya utambulisho,na katika machapisho hayo atatakiwa kuacha kopi mbili ila kwakuwa sasa tupo katika ...
Marato tv - Sauti ya Jamii