▪️Waziri Mavunde azindua mabweni ya Wanafunzi na jengo la mionzi ▪️ Ni matokeo ya marekebisho ya Sheria ya Madini kupitia miradi ya CSR ▪️Asisitiza kuimarishwa mahusiano kati ya Migodi na Jamii ninazozunguka migodi ▪️Rais Samia apongezwa kwa maboresho ya sekta ya Afya ▪️RC Shigela aahidi kusimamia kikamilifu utekelezaji wa miradi Geita Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa bweni katika Shule ya Sekondari Nyamwilolelwa na Mtakuja, mradi unaotekelezwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Geita kupitia Mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), kwa gharama ya zaidi ya Shilingi milioni 291,mradi unaotarajiwa kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuongeza fursa za elimu kwa wanafunzi wa kike. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mavunde amesema utekelezaji wa miradi hiyo ni matokeo ya maboresho ya Sheria ya Madini yaliyoweka wajibu kwa wamiliki wa leseni za madini kurejesha sehemu ya fai...
Marato tv - Sauti ya Jamii