……. Ni cha Kairuki Pharmaceuticals Industry Limited Na Mwandishi Wetu Waziri wa Afya, Jenista Mhagama, amekipongeza kiwanda cha kutengeneza maji tiba cha Kairuki Pharmaceuticals Industry Limited kilichoko Mkoa wa Pwani. Alitoa pongezi hizo jana alipotembelea kiwanda hicho kwa lengo la kujionea uzalishaji wa maji tiba na kuzungumza na mwekezaji wa kiwanda hicho. Waziri Mhagama aliongozana na viongozi mbalimbali kutoka taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Afya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Pwani. Waziri Mhagama alisema amefurahi kufanya ziara katika kiwanda hicho ambapo ameona namna uzalishaji maji tiba unaotumia teknolojia ya kisasa unavyofanyika. Waziri Mhagama alisema serikali inajivunia uwekezaji unaofanywa na taasisi binafsi ikiwemo Kairuki Pharmaceuticals Industry Limited. Alisema utengenezaji wa maji tiba hayo hapahapa nchini unapunguza gharama za usafirishaji pamoja na kupunguza muda wa kusubiri dawa kutoka nje ya nchi. Waziri Mhagama alisema uwekezaji uliofanywa n...
Marato tv - Sauti ya Jamii