RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemtaka Makamu wa Rais, Mheshimiwa Deogratius John Ndejembi, kutambua kuwa cheo alichokabidhiwa si ufalme bali ni dhamana ya kuwatumikia Watanzania kwa uzalendo, uadilifu, bidii na uwajibikaji. Rais Dkt. Samia ametoa kauli hiyo leo, Agosti 29, 2026, katika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, wakati akizungumza katika hafla ya kumuapisha Mheshimiwa Ndejembi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. “Cheo si ufalme, ni dhamana. Dhamana uliyopewa ni ya kuwatumikia Watanzania,” amesema Rais Dkt. Samia. Amesema nafasi ya Makamu wa Rais inahitaji kiongozi mwenye uwezo wa kuwaunganisha wananchi, kusimamia utekelezaji wa shughuli za Serikali na kuhakikisha maslahi ya Taifa yanapewa kipaumbele katika kila hatua. Rais Dkt. Samia amesema uzoefu wa Mheshimiwa Ndejembi katika nafasi mbalimbali za uongozi alizowahi kushika Serikalini, pamoja na uwezo wake wa kujifunza, kufuatilia na kusimamia majukumu aliyope...
Marato tv - Sauti ya Jamii