Skip to main content

Posts

Showing posts from May 9, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Biteko Ashiriki Tulia Marathon Mbeya

📌 Ampongeza Dkt. Tulia kwa ubunifu na kusaidia wahitaji 📌 Wananchi 9,000 wapata bima za afya kupitia Tulia Marathon 📌 Awashukuru wadau na wasanii kwa kushiriki Tulia Marathon Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amempongeza  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson kwa mchango wake katika sekta za afya na elimu sambamba na kusaidia wahitaji jijini Mbeya. Dkt. Biteko ametoa pongezi hizo leo Mei 10, 2025 jijini Mbeya mara baada ya kukimbia mbio fupi za Tulia (Tulia Marathon) katika Uwanja wa Sokoine. “ Dkt. Tulia anafanya kazi kubwa kwenye sekta ya afya na elimu pamoja na kuwajengea nyumba watu wenye uhitaji. Zile nyumba tunazoziona anawakabidhi watu kumbe tayari kuna nyingine zimejengwa Uyole,” amesema Dkt. Biteko. Amesisitiza “ Nataka niwaambie hakuna  sadaka kubwa kama kusaidia wahitaji na sisi wengine tunajifunza kupitia wewe Dkt...

Kapinga Azindua Kituo Mama Cha Gesi Asilia Iliyoshindiliwa (Cng) Jijini Dar Es Salaam

📌 *Ni cha Pili kwa ukubwa barani Afrika; Cha Kwanza kwa ukubwa EAC* 📌 *Kujaza Gesi Asilia kwenye magari 1200 kwa siku* 📌 *Ampongeza Dkt. Samia kutatua changamoto za wananchi kwa vitendo* 📌 *Aipongeza TPDC; Ataka Vituo vya CNG kuendelea kujengwa* Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amezindua Kituo Mama cha Gesi Asilia iliyoshindiliwa (CNG) ambacho kina uwezo wa kujaza Gesi Asilia kwenye magari 1200 kwa siku huku kikifanya kazi kwa muda wa saa 24.  Kapinga amezindua kituo hicho tarehe 9 Mei, 2025 jijini Dar es Salaam akimwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ambapo uzinduzi huo ulienda sambamba na uzinduzi wa basi la mfano la Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) ambalo litaendeshwa kwa kutumia nishati ya Gesi Asilia. Akizungumza na halaiki iliyohudhuria hafla hiyo, Kapinga amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono, mtazamo na maelekezo yake kwa Wizara ya Nishati ambayo yanaleta matokeo chanya kielelezo mojawapo kikiwa ni ...

Wananchi Tarime Wamtaja Kembaki Kama Mbunge Wa Pekee Wakipokea Madawati

Na Shomari Binda-Tarime WANANCHI wa jimbo la Tarime mjini wamemtaja mbunge wa jimbo hilo Michael Kembaki kama mbunge wa pekee katika maendeleo ya elimu. Licha ya wananchi kumtaja mbunge huyo kama wa pekee Chama cha Mapinduzi ( CCM) Wilaya ya Tarime haikuwa mbali na wananchi hao kwa kudai ametekeleza ilani pasipo shaka. Hayo wameyasema kwa nyakati tofauti wakati wakipokea madawati yaliyotolewa na mbunge huyo kwaajili ya shule za msingi. Mmoja wa wananchi hao aliyeshuhudia upokeaji wa madawati hayo Mwita Mniko amesema wamepita wabunge kwenye jimbo la Tarime mjini kwenye sekta ya elimu Kembaki amekuwa suruhisho. Amesema madawati aliyoyatoa yanakwenda kuwafanya wanafunzi kukaa mahala sahihi pa kuwawezesha kusoma pasipo kukaa chini. Mwita amesema mbunge huyo ni mdau mkubwa wa elimu na mchango wake unaonekana kwa macho namna anavyosaidia kuinua elimu. " Tunamshukuru sana mheshimiwa mbunge kwa mchango wake wa kutoa madawati kwaajili ya shule zetu za msingi kwa lengo la kufanya kila mtoto...

Rais Samia, hili la msamaha wa faini za ankara za maji, umekonga nyoyo za wananchi

Na: Dk. Reubeni Lumbagala, Tanga Jamani eeeh! Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ni mtu bingwa wa huduma za maji nchini. Pamoja na kwamba, serikali yake inafanya kazi usiku na mchana kuboresha maisha ya wananchi katika sekta zote, lakini kwenye maji nako kazi zinafanyika haswa. Yaliyofanyika ni mengi kwenye maji, lakini makala hii inaangazia msamaha uliotolewa na Rais Dk. Samia kwa wadaiwa wa faini za ankara za maji ambao wamesitishiwa huduma ya maji kutokana na deni la faini. Msamaha huo wa faini za maji umetangazwa Mei 08, 2025 bungeni na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, kwa niaba ya Rais Dk. Samia wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2025/2026  ambapo Shilingi Trilioni 1.01 zinatarajiwa kutumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na matumizi mengine ya ofisi. "Ninapenda kutoa salamu za Wizara kwa wananchi wote wenye faini kuwa Mama Samia Suluhu Hassan amesamehe faini hizo. Wafike katika Mamlaka z...

Ccm Yatoa Pongeza Kwa Kardinali Robert Francis Prevost Kuwachaguwa Kuwa Papa na Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani

 

Ushindi wa Rigathi Gachagua Kotini

  ALIYEKUWA Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua amepata ushindi Ijumaa baada ya Mahakama ya Rufaa kuamua kwamba, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu hakuwa na mamlaka ya kuteua jopo la majaji kusikiliza kesi zilizopinga kuondolewa kwake madarakani. Majaji Daniel Musinga, Mumbi Ngugi na Francis Tuiyott walisema jukumu la kuteua jopo la majaji limetwikwa Jaji Mkuu na Katiba, na kwamba kuwapangia majaji kazi si mojawapo ya majukumu ya kiutawala ambayo Jaji Mkuu anaweza kumpa Naibu Jaji Mkuu. “Inapaswa kukumbukwa kuwa jukumu la kuteua jopo la majaji limetwikwa Jaji Mkuu kwa mujibu wa Katiba, na hatuoni kuwa ni mojawapo ya kazi za kiutawala ambazo Jaji Mkuu anaweza kumpa au kuhamishia kwa Naibu Jaji Mkuu kwa mujibu wa kifungu cha 5(2) cha Sheria ya Huduma za Mahakama (JSA),” walisema majaji hao. Majaji hao walisema kifungu cha 5(4) cha JSA kinaweka wazi hali tatu pekee ambazo zinaruhusu Naibu Jaji Mkuu kuchukua nafasi ya Jaji Mkuu — ikiwa ni kuondolewa, kujiuzulu au kifo cha Jaji Mkuu. Uam...

Rais Samia Aagana na Mgeni Wake Rais wa Nchi ya Msumbiji

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Daniel Francisco Chapo mara baada ya kuhitimisha Ziara yake ya Kiserikali, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2025.

Wajumbe na Mabalozi 2,200 Wanufaika Songea na Mafunzo ya Utatuzi wa Migogoro Songea

Na Mwandishi Wetu WIZARA ya Katiba na Sheria, imeanzisha program ya kutoa mafunzo ya utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala ambapo wajumbe na mabalozi 2,200 kutoka kata 11 za jimbo la Songea mkoani Ruvuma wamenufaika. Mafunzo hayo yalifunguliwa jana wilayani hapa na Waziri wa  Sheria na Katiba, Dk Damas Ndumbaro na yanatarajiwa kuwanufaika mabalozi na wajumbe wa maeneo mengi. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Dk Ndumbaro alisema Wizara imeanza kutoa mafunzo hayo kwa lengo la kumaliza migogoro ili elimu wanayo pata viongozi hao wakaitumie kutatua migogoro kwa njia mbadala. “Kipekee tumshukuru sana Rais wetu mpendwa Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia mpatiwe mafunzo haya muhimu ya utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala na zaidi mtapatiwa elimu ya utawala bora na ukatili wa kijinsia”, alisema Dk Ndumbaro  Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo kama hayo Wilaya ya Madaba mkoani hapa, Dk Ndumbaro alisema yanalenga kumaliza migogoro mbalimbali ya kisheria inayoibuka na il...

Wazazi,Walimu Shule ya Msingi Bukoba B Wamshukuru Mbunge Mathayo Kuchangia Chakula

Na Shomari Binda-Musoma  WAZAZI na walimu wa shule ya msingi Bukoba B wamemshukuru mbunge wa jimbo la Musoma mjini kwa kuwachangia magunia mawili ya mahindi ili wanafunzi wapate chakula shuleni. Shukrani hizo wamezitoa leo mei 9,2025 kwenye kikao cha wazazi kilichofanyika shuleni hapo wakati wa kujadili maendeleo ya shule hiyo. Wakizungumza baada ya mbunge huyo kuzungumza kwa njia ya simu kwenye kikao hicho kutoka bungeni jijini Dodoma wamesema moyo wa upendo alionao katika kusaidia masuala ya kijamii unapaswa kushukuliwa. Mwalimu Mkuu wa shule hiyo James Makanya licha ya kumshukuru mbunge huyo amesema mtoto anapopata chakula shuleni walau mlo mmoja unamuongezea uwezo wa kufatilia masomo darasani. Amesema suala la chakula lina umuhimu mkubwa na kuwaomba wazazi kumuunga mkono mbunge kwa kuhakikisha wanachangia chakula na kuwa suala endelevu. Makanya amesema chakula ambacho wazazi watakichangia kwaajili ya wanafunzi kitatumika kwa malengo kusudiwa. " Tunamshukuru sana mbunge kwa moy...

Kibano Cha Takukuru Mkoani Kagera Chaokoa Mamilioni ya Fedha

 Na Angela Sebastian; Bukoba  Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoani Kagera imeokoa zaidi ya shilingi milioni 52.6 kwa kipindi cha miezi mitatu ambazo zilitolewa na Serikali kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa hospitali sambamba na  za wananchi waliokuwa wametapeliwa fedha kwa ajili ya kuunganishiwa umeme. Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali jana mjini Bukoba katika ofisi za taasisi hiyo kaimu mkuu wa Takukuru mkoa Hajinas Onesphory alisema kwa kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu Takukuru, walifanikiwa kurejesha vigae vyenye thamani ya shl.mil 50,368,000 kutoka kwa mzabuni aliyepewa kazi ya kujenga hospitali ya Wilaya ya Missenyi. "Katika ufuatiliaji huo tulibaini kutokuwepo na kutotumika  vigae vya zaidi ya thamani ya mil 50.3 ambavyo vilinunuliwa na Serikali ambapo havikuwasilishwa kwenye mradi huku nyaraka zote za mapokezi na manunuzi zikionyesha kuwepo na kupokelewa kwenye mradi"alisema Onesphory Alisema baada ya kubai...