Skip to main content

Posts

Showing posts from November 16, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MBUNGE MNZAVA AWAFURAHISHA WANANCHI NANYOGIE.

  📍Wamasai wampongeza kwa Kasi ya miradi ya maendeleo  Na Mashaka Mhando, Korogwe WANANCHI wa Kijiji cha Nanyogie, kilichopo Kata ya Mkomamazi wilayani hapa, wamempokea kwa shangwe na heshima kubwa Mbunge wao, Mhe. Timotheo Mnzava, kufuatia kimbunga cha maendeleo alichokiwasilisha kijijini hapo kinacholenga kugusa sekta mbalimbali za maisha yao ya kila siku. Kijiji cha Nanyogie ambacho idadi kubwa ya wananchi wake ni wafugaji wa kabila la Kimasai, kipo Kusini, Mashariki pembezoni mwa mto Pangani. Katika ziara hiyo iliyoacha alama kubwa, Mbunge huyo amewasihi wananchi wa jamii ya Kimasai kuhakikisha wanawapeleka shuleni watoto wao wote 13 waliofaulu mitihani ya darasa la saba ili kujiunga na kidato cha kwanza mwakani, akisisitiza kuwa elimu ndiyo urithi pekee wa kuaminika kwa vizazi vijavyo. "Serikali imejenga shule za sekondari karibu katika kila kata ili kuwawezesha watoto wetu kupata elimu bora. Hivyo, niwaombe kuhakikisha watoto wenu wote wanakwenda shule, na ikitokea cha...

SERIKALI YAENDELEA KUIMARISHA URATIBU WA MAANDALIZI YA AFCON 2027

  Na, Mwandishi wetu - Dar es Salaam Serikali imeendelea kuimarisha uratibu wa maandalizi ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027), yanayotarajiwa kufanyika kuanzia Juni 19 hadi Julai 17, 2027, kwa kuzikutanisha Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali ili kutathmini maendeleo ya maandalizi na kuweka mikakati ya kukamilisha utekelezaji wa majukumu yaliyobaki kwa wakati. Hayo yamebainishwa leo (16 Novemba, 2026), jijini Dar es Salaam katika kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Serikali, kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Dkt. Jim Yonazi. Kikao hicho kililenga kupitia na kutathmini hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya mashindano hayo, hususan utekelezaji wa miradi ya miundombinu, upatikanaji na matumizi ya bajeti, uratibu wa shughuli za kisekta pamoja. AFCON 2027 itaandaliwa kwa pamoja na nchi za Tanzania, Kenya na Uganda. Kwa upande wa Tanzania, mashindano hayo yatafanyika ka...

TIBA HEALTHCARE WAFANYA MATEMBEZI YA MAPAMBANO DHIDI YA KISUKARI, WANANCHI WAASWA KUBADILISHA MTINDO WA MAISHA ILI KUDHIBITI MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA (NCDs)

  Na Mwandishi Wetu, Dar. Kampuni ya Tiba Healthcare imefanya matembezi ya kupambana na Kisukari (Diabetes) 'TIBA TWENDE' katika kuadhimisha Wiki ya Magonjwa Yasiyoambukiza inayofanyika wiki ya pili ya Novemba kila mwaka. Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Projesh Mtasingwa, ameitaka jamii kufanya mazoezi, kula mlo kamili na kupima afya mara kwa mara ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza, ikiwemo kisukari. Amesema kampeni ya mwaka huu ni chini ya kauli mbiu, "Zijue Namba Zako, Chukua Hatua, Okoa Maisha," na kwamba watu wengi huishi na magonjwa hayo bila kujua hadi matatizo yanapotokea, hivyo vipimo vya mara kwa mara ni muhimu. Ametaja kutofanya mazoezi, ulaji mbaya, pombe kupita kiasi na tumbaku kama sababu kuu za hatari. Amewashauri wananchi kufanya mazoezi angalau dakika 30 kwa siku, siku tano kwa wiki, kula matunda na mboga za majani, kupunguza chumvi, sukari, pombe na tumbaku, na kupata usingizi wa kutosha. Ametaja kisukari, saratani, magonjwa ya ...

KUELEKEA SAFARI YA MARIDHIANO: RAIS SAMIA ATETA NA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA

  Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo, tarehe 16 Novemba, 2026, amekutana na kuzungumza na wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa Ikulu, Dar es Salaam. Kikao hicho kimejadili maoni ya wadau wa Baraza, uwakilishi wa vyama vya siasa na ushiriki wa wananchi kuelekea kuunda Tume ya Taifa ya Maridhiano.  Sambamba na hayo, Wajumbe hao pia wametoa maoni yao kuhusu mwelekeo wa mchakato wa Marekebisho ya Katiba, utakaotanguliwa na hatua ya Maridhiano. Rais Dkt. Samia amesema vyama vya siasa vinatarajiwa kuwasilisha majina ya watu wawili kwa kuzingatia jinsia kwa kila chama, kwa ajili ya uteuzi wa Wajumbe wa Tume hiyo.  Ameongeza kuwa, baadhi ya majina ya wajumbe wanaopendekezwa tayari yamepokelewa, yakiwemo yaliyowasilishwa kutoka Zanzibar. Kama sehemu ya uwakilishi, Rais Dkt. Samia amesema viongozi wa dini watapata nafasi ya kukutana na kutoa maoni yao kuhusu mchakato huo wa Maridhiano, akibainisha kuwa mashauriano hayo yataendelea waka...

NCHI ZA EAC ZATAKIWA KUUNGANA DHIDI YA VITISHO VYA USALAMA MIPAKANI

  Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimetakiwa kuimarisha ushirikiano wa kikanda ili kukabiliana kwa pamoja na vitisho vya kiusalama vinavyovuka mipaka, ikiwemo ugaidi, makundi yenye silaha, uhalifu wa kimataifa, ukosefu wa usalama mipakani, milipuko ya magonjwa na uhalifu wa mtandaoni. Wito huo umetolewa na Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Uganda, Luteni Jenerali Jack Ngorza Okasumba, wakati akifungua Mkutano wa Wataalamu wa Ulinzi wa EAC, uliofanyika jijini Kampala, Uganda Novemba16, 2026. Mkutano huo ulianza kwa ngazi ya Wataalamu wa Ulinzi, huku ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Mkurugenzi wa Mafunzo na Elimu Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Brigedia Jenerali Benno M. Nzowa, utahitimishwa kwa mkutano wa ngazi ya Mawaziri wa Ulinzi utakaofanyika Novemba 20, 2026 jijini Kampala. Luteni Jenerali Okasumba amesema kuwa vitisho vya kiuslama vinavyovuka mipaka haviwezi kutatuliwa na nchi moja moja, bali zinahitaji hatua za pamoja, mshikamano na ushir...

President Samia Pushes Ahead With National Reconciliation

  By Prosper Makene  President Samia Suluhu Hassan has stepped up efforts to forge national reconciliation, meeting members of the Council of Political Parties at State House in Dar es Salaam to shape the formation of the National Reconciliation Commission and chart the way forward for constitutional review. The meeting, held today, 16 November 2026, discussed the views of Council stakeholders, representation of political parties and citizen participation towards forming the Commission. President Dr Samia said political parties are expected to submit two names each, taking gender into consideration, for appointment as members of the Commission. She added that some proposed names have already been received, including those submitted from Zanzibar. As part of representation, she said religious leaders will be given an opportunity to meet and give their views on the Reconciliation process, noting that consultations will continue while preparations for forming the Commission conti...