WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Jumapili, Oktoba 4, 2026, amesimikwa rasmi kuwa Kanoni Mlei (Lay Canon) wa Kanisa Anglikana Tanzania katika ibada iliyofanyika katika Kanisa Kuu Anglikana la Kristo Mfalme Chanika, Dayosisi ya Handeni, mkoani Tanga. Dkt. Mwigulu amesimikwa katika wadhifa huo katika Ibada ya Misa Takatifu ya kuwekwa wakfu kwa Kasisi Canon Charles Mika Lundu kuwa Askofu wa Dayosisi ya Handeni. Dkt. Mwigulu alishiriki ibada hiyo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Waziri Mkuu alitunukiwa cheo cha Kanoni Mlei na Kanisa Anglikana Tanzania, chini ya Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Dkt. Maimbo Mndolwa, Juni 21, 2026, katika Harambee ya kukamilisha mradi wa jengo la Kitega Uchumi cha Kanisa Anglikana Tanzania iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu, Jimbo la Dodoma. Kanisa Anglikana Tanzania lilimtunuku Waziri Mkuu cheo hicho kwa kutambua mchango wake katika kuhamasisha na kufanikisha uchangishaji wa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo na vitega...
Marato tv - Sauti ya Jamii