Skip to main content

Posts

Showing posts from August 7, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MULEBA: UJENZI WA KITUO CHA KUSUKUMA MAFUTA EACOP WAFIKIA 88%

   Na Angela Sebastian ;Muleba Kituo cha Kusukuma Mafuta Ghafi namba Tatu (PS3) kinachojengwa katika Kijiji cha Kikagate, Kata ya Mubunda, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, kimefikia asilimia 88 ya ujenzi na kinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Agosti au mwanzoni mwa Septemba mwaka huu. Kituo hicho ni sehemu ya Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), unaounganisha maeneo ya uzalishaji mafuta nchini Uganda na Tanzania. Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Derick Moshi, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, amesema kukamilika kwa asilimia 88 ya ujenzi wa PS3 ni hatua kubwa katika utekelezaji wa mradi huo. Moshi amesema ziara ya wabia na wadau wa mradi huo katika kituo hicho imelenga kujionea maendeleo ya ujenzi na hatua zilizofikiwa pia kuweka msisitizo wa kuhakikisha vituo vyote vya kusukuma mafuta vya mradi huo vikikamilika ifikapo Desemba mwaka hatua itakayosaidia katika kukamilisha maandalizi ya uendeshaj...

TRA NA WYFI WAMPONGEZA RAIS SAMIA KUWA KINARA WA NISHATI SAFI AFRIKA

 NA: MWANDISHI WETU Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Taasisi ya Women and Youth Future Initiative (WYFI) wamepongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa Kinara wa Nishati Safi Barani Afrika. Pongezi hizo zimetolewa Agosti 7, 2026, Jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya WYFI. Taasisi ya WYFI inaongozwa na Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Asha Baraka, ambapo imejikita kuwawezesha wanawake na vijana kiuchumi kupitia fursa mbalimbali za maendeleo.  "Kutokana na jitihada alizoonyesha Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan katika kupigania matumizi ya nishati safi ya kupikia, tumeona tumpongeze na kumtia moyo kwa kazi kubwa na nzuri anazofanya," amesema Baraka. Katika tukio hilo, Mkurugenzi wa Nishati Safi ya Kupikia, Nolasco Mlay, alimwakilisha Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba. Akizungumza katika uzinduzi huo, Mlay aliwahimiza vijana na wanawake kutokuwa tegemezi wa ajira pekee, bali kutumia ubunifu, teknolojia na mitandao ya kij...

CHONGOLO AITAKA NIRC KUKAMILISHA UGAWAJI WA PAMPU KABLA YA AGOSTI 30

 📍Nzuguni : Dodoma Waziri wa Kilimo, Mh.Daniel Chongolo, ameipongeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) na kuitaka kuhakikisha pampu za Umwagiliaji  zilizotengwa kwa ajili ya wakulima zinagaiwa kuanzia Agosti 30 kwa wanufaika katika mikoa husika ili ziweze kutumika kuongeza uzalishaji wa mazao. Mheshimiwa Chongolo ametoa maelekezo hayo leo alipotembelea banda la Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika Maonesho ya Wakulima (Nane Nane) yanayoendelea katika viwanja vya John Malechela, Nzuguni, mkoani Dodoma. Amesema Serikali imeendelea kuwekeza katika upatikanaji wa teknolojia za Umwagiliaji kwa lengo la kuongeza tija ya uzalishaji, hivyo ni muhimu vifaa hivyo viwafikie wakulima kwa wakati ili viweze kutoa matokeo yaliyokusudiwa. Waziri Chongolo amepongeza jitihada za Tume katika kuratibu na kusimamia utekelezaji wa programu mbalimbali za Umwagiliaji nchini, zikiwemo usambazaji wa pampu na utekelezaji wa miradi ya Umwagiliaji  inayolenga kuwawezesha wakulima kuzalisha kwa ufan...

KAMBARAGE WASIRA AIKABIDHI BUNDA KOMPYUTA 10 ILI KUONGEZA UJUZI WA TEHAMA SHULENI

 Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Mhe.Kambarage Masato Wasira, ametoa Kompyuta 10 za Kisasa kwa ajili ya kusaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuongeza matumizi ya teknolojia katika shule zilizopo katika Kata 10 za Halmashauri ya Mji wa Bunda. Kompyuta hizo zimekabidhiwa kwa uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda kupitia mwakilishi wa Mbunge huyo, Elly Mwabe, ambaye ameeleza kuwa msaada huo ni sehemu ya mpango wa Mhe.Wasira wa kuendelea kushirikiana na jamii katika kuboresha elimu, hususan katika Mkoa wa Mara. Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkuu wa Wilaya ya  Bunda Mhe.Aswege Kaminyoge amesema kompyuta hizo zitakabidhiwa kwa Halmashauri ya Mji wa Bunda ili wataalamu na viongozi wa halmashauri wabaini maeneo yenye uhitaji mkubwa na kuzisambaza kwa shule husika. Amesema dunia ya sasa inahitaji wanafunzi kuwa na uelewa wa teknolojia, hivyo upatikanaji wa kompyuta mashuleni ni muhimu katika kuwaandaa wanafunzi kukabiliana na mahitaji ya elimu ya kisasa. “Wato...

RC SENDIGA AHIMIZA WANANCHI KUTEMBELEA MAONESHO YA NANENANE, KUJIFUNZA TEKNOLOJIA MPYA ZA KILIMO

 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Cuthbert Sendiga, leo Agosti 7, 2026, akiwa mgeni rasmi wa zamu, ametembelea mabanda mbalimbali katika Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya Themi-Njiro, jijini Arusha. Katika ziara hiyo, Mhe. Sendiga ametoa wito kwa wananchi wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini kujitokeza kwa wingi kutembelea maonesho hayo ili kujifunza teknolojia mbalimbali za kisasa za kilimo, mifugo na uvuvi zitakazochochea ongezeko la uzalishaji na maendeleo ya kiuchumi. Amesema maonesho hayo yamekusanya wafanyabiashara, wabunifu na wajasiriamali kutoka ndani na nje ya nchi, jambo linalotoa fursa kwa wananchi kupata maarifa, kujifunza ubunifu na kuanzisha ushirikiano wa kibiashara. Maonesho ya Nanenane ya mwaka 2026 yanaongozwa na kaulimbiu isemayo: "Tambua Soko, Ongeza Tija kwa Kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050."

TUME YA TAIFA YA UNESCO YAJADILI USHIRIKIANO WA KUENDELEZA JUKWAA LA AMANI KWA VIJANA

 Dar es Salaam, Agosti 7, 2026  Tume ya Taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekutana na ujumbe kutoka African Leadership Initiative for Impact (ALI) kwa lengo la kujadili fursa za ushirikiano katika maandalizi ya Jukwaa la Amani kwa Vijana, linalotarajiwa kufanyika mwezi Septemba 2026 jijini Dar es Salaam. Majadiliano hayo yalilenga kubaini namna pande hizo mbili zitakavyoshirikiana katika kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika kujenga amani, kukuza uongozi wenye maadili na kuimarisha mshikamano wa kijamii kupitia Elimu ya Uraia wa Dunia (Global Citizenship Education - GCED), ambayo ni moja ya maeneo ya kipaumbele ya UNESCO katika kujenga jamii zenye amani, uvumilivu na maendeleo endelevu. Akizungumza wakati wa kikao hicho, Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Profesa Hamisi Malebo, alisema Tume imepokea kwa furaha wazo hilo na kuliona kuwa linaendana na dhamira ya UNESCO ya kujenga amani katika fikra za watu kupitia elimu, sayansi, utamaduni, ma...

Vi AGROFORESTRY YASEMA KILIMO MISITU NI SULUHISHO UHABA WA CHAKULA

 Na Mwandishi Wetu, Dodoma SHIRIKA la Vi Agroforestry Tanzania, kwa kushirikiana na wadau wake akiwemo Tanzania Alliance for Biodiversity (TABIO), limeendelea kutumia Maonesho ya Nanenane kuhamasisha matumizi ya kilimo misitu kama suluhisho la kuongeza uzalishaji wa chakula, kuboresha lishe, kuhifadhi mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Akizungumza katika maonesho hayo yanayofanyika katika viwanja vya John Malecelea jijini Dodoma, Mkurugenzi Mkaazi wa  Vi Agroforestry Tanzania, Martha Olotu, alisema shirika hilo linaendelea kuhamasisha mfumo wa kilimo unaounganisha mazao, miti na mifugo katika eneo moja ili kuongeza tija ya uzalishaji, kuboresha rutuba ya ardhi na kuongeza kipato cha wakulima. Alisema banda la Vi Agroforestry limepokea idadi kubwa ya wakulima, wataalamu na wananchi waliotembelea kujifunza mbinu mbalimbali za kilimo misitu pamoja na kuona bidhaa zinazotokana na mfumo huo, zikiwemo mbegu za asili, unga wa ubuyu, vyakula vya lishe na ma...

BWAWA LA FARKWA TUMAINI JIPYA LA MAJI MKOANI DODOMA

  ▪️Ujenzi Wake Kuanza Oktoba 2026 ▪️Fidia Shilingi bil 8.5 Imeshalipwa kwa Wananchi Waliopisha Mradi *Na Adelina Johnbosco – MAELEZO* Tatizo la uhaba wa maji katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Dodoma linaelekea kupata ufumbuzi wa kudumu kufuatia ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Farkwa utakaoanza kujengwa Oktoba mwaka huu. Bwawa hilo litakalojengwa wilayani Chemba, kata ya Farkwa mkoani Dodoma litakuwa na uwezo wa kuzalisha lita milioni 128 kwa siku na kuhifadhi lita bilioni 390 na linatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 22. Bwawa hili litahudumia hasa wilaya za Chemba, Bahi, Chamwino na maeneo mengine ndani na maeneo ya karibu na mkoa wa Dodoma, lengo ni kutokomeza kabisa upungufu wa maji ndani ya mkoa huo. Ujenzi wa bwawa la Farkwa utatekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa gharama ya Shilingi bilioni 163.43 hadi kukamilika kwake. Aidha, jumla ya Shilingi bilioni 8.5 zimelipwa kama fidia kwa wananchi kutoka katika vijiji viwili vya Mombose na B...

FURSA ZA BIASHARA ZA MABILIONI KATIKA MIGODI ZAWAFUNGUKIA WATANZANIA

 Vijana na wanawake wapewa kipaumbele kunufaika na mnyororo wa thamani wa madini 📍DODOMA Serikali kupitia Tume ya Madini imefungua fursa za biashara zenye thamani ya mabilioni ya fedha katika migodi kwa Watanzania, huku vijana na wanawake wakipewa kipaumbele ili kuongeza ushiriki wao katika Sekta ya Madini na kuchochea utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Hatua hiyo inalenga kujenga uchumi shindani na jumuishi unaowezesha Watanzania kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji, kuongeza thamani ya rasilimali za madini na kunufaika zaidi na fursa zinazotokana na sekta hiyo. Akizungumza katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, Dodoma, Mjiolojia kutoka Kurugenzi ya Ukaguzi na  Biashara ya Madini ya Tume ya Madini, Hassan Mkumba, amesema Tume imeainisha bidhaa na huduma 20 zitakazotolewa mahsusi na Watanzania ili kuongeza ushiriki wao katika shughuli za migodi. Amezitaja baadhi ya huduma hizo kuwa ni usambazaji wa vilainishi migodini...