Na Mwandishi Wetu, Mafinga SHULE ya Sekondari Ndolezi iliyopo Halmashauri ya Mji Mafinga, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, imeandika historia mpya baada ya kuanza rasmi kupokea wanafunzi wa Kidato cha Tano kwa mara ya kwanza. Hatua hii inatajwa kuwa ukombozi mkubwa utakaopanua fursa za elimu ya sekondari ya juu (A-Level) katika eneo hilo. Akizungumza na wanafunzi wa kwanza waliowasili shuleni hapo, Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Mji Mafinga, Mwalimu Stephen Shemdoe, amesema lengo kuu la Halmashauri ni kuhakikisha wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali nchini wanapata elimu bora itakayowezesha kupata matokeo mazuri na kuchangia maendeleo ya Taifa. Mwalimu Shemdoe amebainisha kuwa Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika ujenzi wa miundombinu na kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia. Kutokana na uwekezaji huo, amewataka wanafunzi kutumia fursa hiyo adhimu kusoma kwa bidii, kutunza mali za shule, na kuzingatia nidhamu ya hali ya juu. "Matamanio ya Serikali ni kuona...
Marato tv - Sauti ya Jamii