Skip to main content

Posts

Showing posts from August 28, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

RAIS SAMIA ATOA KAULI NZITO KUHUSU ULINZI WA MIPAKA

Amri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Rais Dr Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali yake itatumia kila uwezo katika kuimarisha jeshi la ulinzi wa wananchi Tanzania. Rais Samia ametoa kauli hiyo Agosti 28-2024 jijini Dar es Salaam,wakati akikabidhi mabasi ya kisasa na ndege kwa ajili ya mafunzo kwa marubani kwa mkuu wa majeshi ya ulinzi jenerali JACOBO JOHN MKUNDA. Rais Samia pamoja na kulipongeza JWTZ kwa kazi kubwa inayofanya katika mipaka ya Tanzania, amesema lazima serikali iendelea kuliimarisha kwa kulipatia zana na vifaa vya kisasa ili liwe tayari kukabiliana na matishio yoyote ya kiusalama. Kwa sababu hiyo Rais Samia, amesema pamoja na serikali kuendelea kuimarisha hilo,amewataka Watanzania kutambua kuwa suala la ulinzi wa mipaka ni jukumu la kila Mtanzania. Kwa upande wake waziri wa ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa Mh Dtk Stergomena Tax,amempongeza Rais Samia kwa uongozi wake imara ambao umeimarisha diplomasia ya ulinzi na mataifa mengine.  Kwa upande wake mkuu...

Daraja la Mwadobana Kuchochea Uchumi Bariadi

Na Mwandishi Wetu Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA)  wilayani Bariadi imejenga Daraja la Mwadobana lenye urefu wa mita 36 na upana mita 9.9 ambalo litachochea ukuaji wa uchumi wilayani humo. Kaimu Meneja wa TARURA wa Wilaya ya Bariadi, Mhandisi Khalid Mang’ola amesema hayo wakati wa mahojiano kuhusu miradi iliyotekelezwa na TARURA wilayani humo. “Tumekamilisha ujenzi wa daraja la  Mwadobana, lenye urefu wa mita 36 na upana wa mita 9.9. Daraja hili pamoja na maingilio ya barabara limegharimu shilingi bilioni 1.1, ambapo linaunganisha Kata za Mwaubingi, Nkololo, Banemhi na Mwadobana,” amesema Mhandisi Mang’ola. Amesema  kuwa, uwepo wa daraja la Mwadobana utaongeza uchumi wilayani humo, kutokana na biashara za madini ya dhahabu katika Kata ya Mwaubingi, ambapo kwa sasa wafanyabiashara wa madini watakuwa na uhakika na biashara yao kutokana na njia kupitika kwa mwaka mzima bila changamoto yoyote hasa katika kipindi cha masika. Kwa upande wake Mariam Ma...