Waziri wa Uchukuzi Mheshimiwa Profesa Makame Mbarawa leo tarehe 12 Juni, 2026 amezindua majaribio ya kuruka na kutua ndege katika Uwanja wa Ndege Musoma na kuahidi kuwa ndege za abiria kuanza kufanya kutua katika uwanja huo mwezi Julai, 2026. Akizungumza katika hafla, Mhe. Mbarawa ambaye alikuwa mgeni rasmi ameliagiza Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kuharakisha utaratibu wa kuupanga Uwanja wa Ndege Musoma katika ratiba za ndege za abiria ili wananchi wa Mkoa wa Mara waweze kuanza kutumia usafiri huo. “Ninaiagiza ATCL kuhakikisha kuwa inauingiza Uwanja wa Ndege Musoma katika ratiba za ndege haraka iwezekanavyo ili huduma za usafiri ziweze kutolewa kwa wananchi” amesema Mhe. Mbarawa. Mhe. Mbarawa amesema majaribio ya utayari katika viwanja vya ndege vya Musoma na Shinyanga yanaashiria kukamilika kwa sehemu muhimu za miradi ya ukarabati na upanuzi wa viwanja hivyo na kuwa tayari kuanza kutoa huduma kwa wananchi. Mhe. Mbarawa amezielekeza taasisi zinazohusika na mra...
Marato tv - Sauti ya Jamii