Skip to main content

Posts

Showing posts from September 10, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Vyama Vya siasa vyaagizwa kufuata Sheria ya uchaguzi

Na MASHAKA MHANDO, Tanga VYAMA vya siasa mkoani Tanga, vimetakiwa kufuata kanunu, taratibu na Sheria ya uchaguzi kuchagua wanaendesha kampeni zenye na upendo ili uchaguzi wa Oktoba 29 mwaka huu ufanyike kwa amani. Akizungumza katika semina ya siku moja iliyofanyika katika ukumbi wa Jiji la Tanga Leo Septemba 11, Ofisa Mwandamizi wa ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa nchini, Edna Assey alisema vyama vinapaswa kufuata Sheria na waepuke kampeni zenye viashiria vya uvunjigu wa amani nchini. Alisema kuwa wajibu wa vyama vya siasa ni uchaguzi na kushinda baada ya wananchi kuridhika na sera za vyama vyao wanazofanya mikutano ya kampeni. Ofisa huyo alisema viongozi hao wafuate taratibu za uchaguzi ambazo ni mbili za Vyama vya siasa Sheria namba 257 na Sheria namba 278 za gharama za uchaguzi. "Najua viongozi mnajua Sheria hizi, mtazifuata lakini mtafanya kampeni za kistaarabu ambazo zitasababisha uchaguzi wetu unafanyika kwa Amani na haki," alisema. Pia aliwataka kuhakikisha kuwa end...

Majaliwa Afungua Kongamano la Nne la Kitaifa la Ufuatiliaji na Tathmini

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Septemba 11, 2025 amemuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa kongamano la Nne la Kitaifa  la Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza linalofanyika katika ukumbi wa hotel ya Malaika Beach jijini Mwanza. Washiriki wa kongamano hilo ni wadau wa maendeleo, wakurugenzi wa halmashauri, wataalam kutoka nje na ndani ya Serikali pamoja na viongozi kutoka Mataifa mbalimbali ya Afrika na nje ya Afrika. kaulimbiu  ya Kongamano ni “Kuimarisha uwezo wa Ufuatiliaji na Tathmini kwa Jamii ili kuwezesha utendaji bora na maendeleo endelevu”.

Viongozi Ccm Tuhimize Wananchi Kupiga Kura - Dkt. Biteko

Mgombea Ubunge Jimbo la Bukombe, Ndugu Doto Mashaka Biteko amewahimiza viongozi wa Chama cha Mapinduzi ngazi Vitongoji, Vijiji na Kata kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu ujao utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu. Dkt. Biteko amesema hayo Septemba 10, 2025 katika Kata ya Ng’anzo wilayani Bukombe ambapo amesema Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan anastahili kura zote za Ndiyo ili aweze kuongoza nchi kwa kipindi kingine na kukamilisha utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ya maji, umeme na miundombinu. “ Viongozi hamasisheni wananchi tarehe 29 Oktoba wamchague Dkt.  Samia Suluhu Hassan ambaye ametuletea maendeleo na kwa kumchagua yeye tutaendelea kupata maendeleo mengine mengi. Nawaomba pia mnichague mimi Dkt. Doto Biteko ili tukamilishe yale tuliyokwisha yaanzisha lakini pia mtuchagulie Diwani wa CCM, Ndugu Mashaka na kuchagua viongozi wa CCM ni kuchagua maendeleo ya nchi hii”

Rais Samia Kuziunganisha Monduli na Ngorongoro Kwa Barabara ya Lami

 _Usanifu wakamilika, yatarajiwa kukuza utalii na uchumi wa Arusha_ Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeanza rasmi utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami ya Mto wa Mbu- Engaruka, Engaruka- Ngaresero ili kukuza shughuli za kiuchumi na kijamii ikiwemo Utalii na Uwekezaji, barabara itakayoziunganisha Wilaya za Monduli na Ngorongoro. Akizungumza na Viongozi wa dini, Mila na Serikali pamoja na Watendaji kuanzia ngazi ya Kitongoji Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, leo Jumatano Septemba 10, 2025 wakati akihitimisha ziara yake Wilayani humo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla amesema usanifu wa barabara hiyo ya Mto wa Mbu- Engaruka- Ngaresero yenye urefu wa Kilomita 74 umekamilika na hatua za kumpata Mkandarasi zimeshaanza. "Lengo la Mhe. Rais na serikali yake ya awamu ya sita ni kutatua hili tatizo la muda mrefu na kuunganisha Wilaya za Monduli na Ngorongoro suala ambalo litavutia zaidi uwekezaji unaofanywa kw...

Wasira Awapa Ujumbe Mzito Walioongoza Ubunge, Udiwani

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira wanachama walioongoza kura za maoni na kupewa dhamana ya kupeperusha bendera ya Chama katikabuchaguzi mkuu wa mwaka wana dhima ya kuwaunganisha wana CCM na na sio kuwafarakanisha. Amesema CCM ni kama mtumbwi unaosafiriwa na wengine, hivyo haitavumiliwa kuona watu wachache wanataka kuutoboa kwa utazamisha watu wote. Wasira alieleza hayo kilosa mkoani Morogoro alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya wilaya hiyo, akiwa katika ziara ya kutafuta kura za mgombea urais wa CCM, wagombea ubunge na udiwani. Alisema anatambua kuna msuguano, kwenye baadhi ya kata ambapo walioshindwa wanasema hawajashindwa vizuri, hivyo kusababisha misuguano na walioshinda. "Sisemi hapa mna matatizo makubwa, wala sikweli, yako majimbo yana matatizo nimepitapita huko nimekutana na matatizo makubwa, kuna mahali imenibidi nifanye maamuzi magumu, lakini hapa ninaambiwa matatizo hayo yapo lakini yanaweza kumalizwa. ...

Vitongoji vinne katika kijiji cha Mtukula kunufaika na mradi wa maji wa Bilioni 1.4

  Na Angela Sebastian  Missenyi Wananchi wa vitongoji nane wapatao 7,562 katika kijiji cha Mutukula Wilayani Missenyi mkoani Kagera wanatarajiwa kunufaika na mradi wa maji wa kijiji hicho, unaohudumiwa na mamlaka ya Maji safi maji taka na usafi wa Mazingira (BUWASA) ambao umefikia asilimia 70.   Mradi huo ambao unatagharimu shilingi Bilioni 1.4 utakapokamilika utaongeza upatikanaji wa maji katika eneo linalohudimiwa na BUWASA kwa wilaya hiyo kutoka asilimia 86 ya sasa hadi 100. Kiongzi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2025 Ismail Ali Ussi umetembelea mradi huo na kulidhishwa na maendeleo ya utekelezaji ambapo amesema hayo ni maono ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi hawatembei mwendo mrefu kufuata huduma ya maji . "Tumelidhishwa na utekelezaji wa mradi huu ambapo unahudumiwa na Buwasa tunawaomba wanachi wa vitongoji vitano ambavyo bado havijapata maji tuwe wavumilivu mradi unakamilika muda si mrefu tunapata maji safi na salama kwasababu nia...

Mwenge wa Uhuru Wazindua Shule ya Sekondari ya Wasichana Kyaka

 Na Angela Sebastian ;Missenyi  Mwenge wa uhuru umezindua bweni la wasichana wa kidato cha tano na sita lenye vyumba viwili katika shule ya sekondari Kyaka iliyoko Wilayani Missenyi mkoani Kagera. Bweni hilo ambalo limegharimu shillingi milioni 260 ambapo ni chachu kuwajengea uwezo wanafunzi wa kike wanaotarajiwa kujiunga na shule hiyo mwaka kesho, kufanya vizuri katika masomo yao,kujiamini na kuepuka adha za kiusalama ambazo watoto wa kike hukumbana nazo wanapotafuta elimu. Akisoma taarifa ya mradi kwa kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Ismail Ali Ussi leo,mkuu wa shule hiyo Fadhir Nnko amesema fedha ya ujenzi huo ilitoka Serikali kuu ambapo mradi huo ulianza kutekelezwa Machi 15,2025 na kukamilika Agosti 20 mwaka huu kwa asilimia 100. "Bweni hilo linaouwezo wa kulaza wanafunzi 160 wa kidato cha tano na sita kwa wakati mmoja ambao wanatarajiwa kudahiliwa mwaka ujao wa masomo kutoka maeneo mbalimbali ya nchi na itasaidia kuondoa adha za watoto wa kike kutembea umbali mrefu ...