Wakati maonesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa, mjini Sumbawanga, mkoani Rukwa yakiwa katika siku ya pili, leo tarehe 9 Oktoba 2026, banda la VETA limekuwa na mvuto wa kipekee likikusanya wadau na wananchi kwa ujumla kushuhudia umahiri wa vijana wahitimu wa ufundi stadi, hususani wenye ulemavu kutoka vyuo mbalimbali vya VETA. Katika maonesho hayo yanayofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi, Nduwa chini ya kaulimbiu, _Mazingira Tofauti, Fursa Sawa kwa Vijana_, VETA inawakilishwa na vijana wahitimu na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya VETA, wengi wao wakiwa ni wenye ulemavu, hivyo kutafsiri kaulimbiu hiyo kwa vitendo zaidi. Miongoni mwa wahitimu hao ambao wameonesha umahiri mkubwa na kuwa kivutio kikubwa cha wadau na wananchi katika maonesho hayo ni pamoja na wanafunzi wenye ulemavu wa viungo Francis Madanganya, mhitimu wa stadi ya TEHAMA kutoka Chuo cha TEHAMA cha VETA Kipawa na Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi Morogoro ambaye ana ubunifu wa Power Bank ya kompyuta mpakato (laptop); G...
Marato tv - Sauti ya Jamii