MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo mpya za petroli, dizeli na mafuta ya taa zitakazoanza kutumika kuanzia Jumatano, Oktoba 7, 2026, saa 6:01 usiku. EWURA imesema ongezeko hilo limechangiwa na kupanda kwa bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia kutokana na kuibuka upya kwa mgogoro wa kisiasa katika Mashariki ya Kati. Kwa bei za rejareja katika bandari, Dar es Salaam petroli itauzwa hadi Sh4,057 kwa lita, dizeli Sh4,086 na mafuta ya taa Sh4,067. Tanga, petroli itauzwa hadi Sh4,123, dizeli Sh4,152 na mafuta ya taa Sh4,133 kwa lita, huku Mtwara petroli ikiwa Sh4,170, dizeli Sh4,199 na mafuta ya taa Sh4,180 kwa lita. Kwa baadhi ya maeneo ya ndani, bei ya juu zaidi ya petroli iliyotajwa katika jedwali la EWURA ni Sh4,370 kwa lita Kyerwa (Ruberwa), Kagera, huku dizeli ikiwa Sh4,399 na mafuta ya taa Sh4,380. EWURA imewataka wafanyabiashara kuzingatia bei kikomo zilizotangazwa na imeonya kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wa...
Na Ssgt Mawazo Mtondo - DODOMA. Kanda ya Magereza imeonesha uwezo mkubwa katika Mashindano ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) 2026, baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu kati ya Kanda saba zilizoshiriki mashindano hayo yaliyofanyika jijini Mwanza kuanzia Septemba 21 hadi Oktoba 3, 2026. Kwa mujibu wa matokeo ya jumla yaliyotolewa leo, Oktoba 6, 2026, Kanda ya Magereza imefanya vizuri katika Mashindano ya BAMMATA 2026, baada ya kutwaa vikombe viwili vya mshindi wa kwanza kupitia michezo ya wavu kwa wanaume na wanawake, pamoja na vikombe vinne vya mshindi wa pili, vikiwemo mpira wa pete na kurusha vishale. Aidha, Katika riadha, Kanda ya Magereza ilipata kikombe cha mshindi wa pili kupitia Inspekta Catherine Lange, aliyeshika nafasi ya pili katika mbio za Half Marathon. Mafanikio hayo yanaonesha ushindani wa Kanda ya Magereza katika mashindano yaliyowakutanisha wanamichezo kutoka vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama nchini, kwa lengo la kuimarisha umoja, mshikama...