NA: MWANDISHI WETU, DODOMA Maridhiano baina ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Alliance For Change and Transparency (ACT-Wazalendo) kuelekea uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Zanzibar, umepongezwa kwani umezingatia maslahi ya nchi ambayo ni muhimu kuliko maslahi binafsi ya wanasiasa. Hayo yameelezwa na Mbunge wa Viti Maalum CCM na Mwenyekiti Taifa wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda, Julai 9, 2026, Jijini Dodoma. Akitoa maoni yake baada ya kumalizika hafla hiyo ya Tamko la Pamoja la Maridhiano ya Kisiasa baina ya vyama hivyo, Chatanda amesema, Wazanzibar wameshasahau siasa za chuki, kipaumbele chao sasa ni umoja, mshikamano na maendeleo. "Wazanzibar ni watu rahimu sana, wao wanataka amani, mshikamano na maendeleo na kitendo cha vyama hivi viwili kufikia muafaka, ni ishara ya ukomavu wa kisiasa na kuzingatia maslahi ya nchi," amesema Chatanda. Aidha, amesema maridhiano hayo yana maana kubwa katika kuhakikisha SUK inaundwa kwa ukamilifu wake kwani SUK ...
Marato tv - Sauti ya Jamii