DKT. MUNISI AKUTANA NA KUFANYA KIKAO KAZI CHA KIMKAKATI NA WAKURUGENZI WA IDARA YA AJIRA NA UKUZAJI UJUZI
Na. OWM (KAM) Dodoma Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Dkt. Evaline Munisi amekutana na kufanya kikao kazi na Wakurugenzi pamoja na wataalamu wa Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi hiyo kwa lengo la kuimarisha utekelezaji wa majukumu, kuongeza ufanisi wa kazi na kuimarisha ushirikiano katika utoaji wa huduma kwa wananchi. Katika kikao hicho kilichofanyika ofisini kwake Dodoma Juni 04,2026 , Dkt. Munisi ameitaka idara hiyo kuongeza juhudi katika kutangaza fursa mbalimbali za ajira na programu za ukuzaji ujuzi zinazotolewa na Serikali ili kuwafikia Watanzania wengi zaidi na kuwawezesha kunufaika na fursa hizo kwa wakati. Aidha, amesisitiza umuhimu wa ubunifu, uwajibikaji na ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya idara hiyo ili kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakuwa na tija, zinawafikia walengwa ipasavyo na kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini. Dkt. Munisi ameelekeza idara hiyo kuweka mkazo katika uboreshaji w...