Msalala, Kahama Kamati ya Kitaifa ya Ufungaji Migodi imepitia na kujadili Mpango wa Ufungaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu uliopo Halmashauri ya Msalala, Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, ili kujiridhisha kama unakidhi matakwa ya sheria, kanuni na miongozo inayosimamia shughuli za ufungaji migodi nchini. Kikao hicho kilichofanyika mapema jana kililenga kutathmini iwapo mpango huo unazingatia matakwa ya Sheria ya Madini, Sura ya 123, Kanuni za Uchimbaji Madini (Usalama, Afya na Utunzaji wa Mazingira) za mwaka 2010 pamoja na Mwongozo wa Ufungaji Migodi wa mwaka 2019. Akiongoza kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Ufungaji Migodi, Mhandisi Hamisi Kamando, alisema migodi ya kati na mikubwa inalazimika kisheria kuandaa na kuwasilisha mipango ya ufungaji migodi kwa Mkaguzi Mkuu wa Migodi kwa ajili ya mapitio na uidhinishaji. Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Madini, Sura ya 123 na Kanuni ya 206 ya Kanuni za Uchimbaji Madini (Usalama, Afya na Utunzaji wa Mazingira) za mwak...
Marato tv - Sauti ya Jamii