Skip to main content

Posts

Showing posts from February 14, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Biteko Aikaribisha India Kuwekeza Miradi Ya Umeme Jua Nchini

📌 Asema suala la Tanzania kuwa na nishati ya uhakika si la kusubiri 📌 Taasisi ya Kimataifa ya Umeme Jua (ISA) yaonesha nia ya kuwekeza 📌 Kituo cha umahiri wa umeme jua kuzinduliwa Arusha Juni mwaka huu Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kimataifa ya Kuendeleza Nishati ya Jua (ISA), Dkt. Ajay Mathur yenye Makao Makuu yake nchini India ambaye ameeleza nia ya ISA kuwekeza katika miradi ya umeme jua nchini. Mazungumzo  kati ya Dkt. Biteko na Dkt. Mathur yamefanyika jijini New Delhi nchini India ambapo Dkt. Biteko alishiriki Wiki ya Nishati India ambayo ilienda sambamba na mikutano mbalimbali kuhusu nishati.  “ Tunawaalika mje kuwekeza Tanzania kwani tunahitaji kuwa na miradi mingi ya umeme kutoka vyanzo tofauti ili kuweza kutosheleza mahitaji ya watu wetu na kinachotupa msukumo zaidi kwa sasa ni mpango mahsusi wa misheni 300 tuliousaini mwezi Januari 2025 ambapo Tanzania tunapaswa kup...

Majaliwa Mgeni Rasmi Mkutano Mkuu Jimbo la Itilima

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Waziri Mkuu Ndugu Kassim Majaliwa leo Februari 15, 2025 ni mgeni rasmi kwenye Mkutano Mkuu Maalum Chama cha Mapinduzi Jimbo la Itilima, mkoani Simiyu. Mkutano huo maalum mbali na kuhudhuriwa maelfu ya wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa jimbo la Itilima lakini pia umehudhuriwa na mamia ya wana CCM,wapenzi na wakeleketwa wa chama hicho wakiwemo viongozi mbalimbali wa chama, Serikali  na viongozi wa dini.

Rc Chongolo atoa maagizo mazito kwa Tanroads Mkoa wa Songwe

  Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo, amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Songwe, Mhandisi Suleiman Bishanga, kuhakikisha mkandarasi wa barabara ya Isongole-Isoko anaanza ujenzi mara moja. Tayari serikali imetangaza zabuni kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Isongole II – Ibungu – Isoko (km 52.419) kwa kiwango cha lami, ambapo waathiriwa wa mradi wapatao 312 wamelipwa jumla ya TZS milioni 850.269 kama fidia ya mali, nyumba, na mazao yao. Barabara hiyo ni muhimu kwani itasaidia kuunganisha mikoa ya Mbeya na Songwe, hivyo kurahisisha usafiri na biashara mipakani, kati ya mpaka wa Kasumulu wilayani Kyela, Mkoa wa Mbeya, na Isongole wilayani Ileje na Tunduma wilayani Momba, Mkoa wa Songwe, ambazo zinapakana na nchi za Malawi na Zambia.

Serikali kuendelea kuwezesha Wanawake Kiuchumi-Rc Mtambi

 Na Ghati Msamba, Mara. Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, amesema Serikali mkoani hapo itaendelea kuunga mkono shughuli za maendeleo ya wanawake. Amesema hayo wakati alipokuwa akifungua Mkutano wa Chemba ya Wanawake Wafanyabiashara (TWCC) katika Ukumbi wa Uwekezaji, ulio Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara. “Serikali inazo fursa nyingi kwa ajili ya wanawake, ikiwemo mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa hapa nchini kwa ajili ya makundi maalum ya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu,” amesema Kanali Mtambi. Kanali Mtambi ameongeza kuwa Serikali imeweka mazingira mazuri, ikiwemo sera, sheria, kanuni, na taratibu zinazowawezesha wanawake kufanya shughuli zao, hususan shughuli za uzalishaji mali, bila kubaguliwa. Aidha, amewataka wanawake kutumia fursa mbalimbali zilizopo katika Mkoa wa Mara, ikiwa ni pamoja na kilimo, ufugaji, uvuvi, utalii, na uchimbaji wa madini ili kujikwamua kiuchumi. Amewataka wanawake wa Mkoa wa Mara kujitokeza kwa wingi kushiri...

Rais Samia Ashiriki Mkutano Wa Baraza La Amani Na Usalama Umoja Wa Afrika Nchini Ethiopia

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AUPSC) pamoja na viongozi kutoka nchi mbalimbali katika Makao Makuu wa Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 14 Februari, 2025.

Rais Samia Awasili Nchini Ethiopia Kushiriki Mkutano wa Wakuu Wa Nchi na Serikali

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole, Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 14 Aprili, 2025 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU). Pamoja na mambo mengine pia Mhe. Rais Dkt. Samia atashiriki mkutano wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika

Mbunge Mathayo akumbushia Bungeni eneo la jeshini kuhusu ujenzi wa shule

  Na Shomari Binda MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo ameendelea kuwasemea wananchi bungeni kuhusiana na masuala mbalimbali. Leo hii februari 14 bungeni katika bunge la 12 mkutano wa 18 mbunge huyo katika swali la nyongeza alilouliza kwrnye Wizara ya Ulinzi alitaka kujua ni nini kinaendelea katika eneo la jeshi Makoko kuhusu ujenzi wa shule. Mbunge Mathayo amesema katika siku za nyuma alishaulizia kuhusu eneo hilo na timu ya Wizara kufika eneo la tukio lakini bado majibu hayajapatikana. Amesema wananchi wa eneo la Makoko manispaa ya Musoma wanao uhitaji mkubwa wa shule ili watoto wa eneo hilo waweze kupata elimu. " Mheshimiwa Naibu Spika nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza,katika siku za nyuma niliuliza hapa bungeni kuhusu eneo la jeshi Makoko pale Musoma kuhusu maombi ya wananchi na ujenzi wa shule. " Nashukuru timu ilishafika pale na kuangalia eneo hilo sasa nini kinaendelea ili wananchi waelewe kuhusu maombi yao"ameulizia. Akimjibu ...