Skip to main content

Posts

Showing posts from February 18, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Majaliwa Kuzindua Kampeni Ya Kitaifa Ya Msaada Wa Kisheria Ya Mama Samia, Mkoa Wa Lindi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Februari 19, 2025 atazindua kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia katika mkoa wa Lindi, kwenye viwanja vya Madini, Ruangwa Mkoani humo. Lengo la Kampeni hiyo ni kuwafikia wananchi  wenye uhitaji na wasio na uwezo wa kumudu gharama za huduma za kisheria. Pia kampeni hiyo itawezesha kupata utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala, kuongeza uwajibikaji kwa watendaji na kuimarisha umoja na mtangamano miongoni mwa jamii. Mpaka sasa kampeni hiyo imefika katika mikoa  16 na kuhudumia wananchi zaidi ya milioni 1 Kaulimbiu ya kampeni hiyo ni “Msaada wa Kisheria kwa Haki, Usawa Amani na Maendeleo”.

Nitakuwa Mkali Sana Kwa Wala Rushwa na Wanaotumia Vibaya Madaraka yao-Rc Tabora

Mkuu wa Mkoa wa Tabora  Paul Chacha amemsimamisha kazi Meneja wa Wakala wa huduma ya ununuzi serikalini(GPSA) wa Mkoa huo Mayala Ambuli pamoja na Watumishi Wawili wa Wakala wa Barabara(Tanroads)kwa ajili ya kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazowakabili.  Chacha amechukua hatua hiyo baada ya kupokea Malalamiko kutoka kwa Wateja wa GPSA Mkoani Tabora  pamoja na viongozi akiwemo yeye binafsi kuwa Muhanga wa Lugha ambazo hazina staha kutoka Ndugu Mayala. "Leo asubuhi nimefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi ya Wakala wa huduma ya ununuzi Serikalini (GPSA)- Mkoa wa Tabora, nikiwa Katika ziara hiyo na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tabora nimemsimamisha Kazi kupisha Uchunguzi Ndugu Mayala Ambuli ambaye alikuwa ni Meneja wa GPSA mkoa wa Tabora kwa tuhuma za Kutumia Madaraka yake vibaya, Kutoa Lugha Zisizo na Staha kwa Wateja wa GPSA na Viongozi wa Serikali na kuwa na Utovu wa nidhamu Kazini"Alisema Chacha Wakati wa kikao hicho.  Pia, Mkuu wa Mkoa Tabora Pa...

Rais Mwinyi Aishukuru WB Kwa Msaada Wa Sekta Ya Afya Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi ameishukuru Benki ya Dunia kwa Msaada wa kiasi cha Dola Milioni 100 kwa ajili kuimarisha Miundombinu ya Sekta ya Afya  hapa nchini. Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Mkurugenzi Muendeshaji wa Benki hiyo Kanda ya Kusini Mwa Afrika  Milena Stefanova na ujumbe wake, Ikulu Zanzibar tarehe 18 Februari 2025. Aidha Rais Dkt.Mwinyi ameuelezea Ujumbe huo kuwa Serikali ina Malengo Mahsusi ya kuifanya Zanzibar kuwa kituo Bora cha Matibabu kwa Nchi za Afrika Mashariki na Afrika  kwa  Ujumla na kuipongeza Benki ya Dunia kwa kuendelea kuunga mkono juhudi hizo. Naye Mkurugenzi Muendeshaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Kusini Mwa Afrika Milena Stefanova ameeleza kuwa Benki hiyo inaridhika na juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya  Zanzibar za kuimarisha huduma za Afya na kuahidi kuendelea na misaada kwa ustawi wa watu wake. Kwa upande mwingine Waziri wa Afya Nassor Ahmed Mazroui ame...

Kamati Ya Pic Yaona Tija Uwekezaji Kiwanda Cha Uzalishaji Bidhaa Za Ngozi

*Waziri Ridhiwani Kikwete aihakikishia uwekezaji endelevu.  Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na mitaji ya Umma (PIC) imepongeza serikali ya Awamu ya sita chini  Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uwekezaji wenye tija na manufaa kwa  maendeleo ya nchi  katika kiwanda cha uzalishaji wa bidhaa za ngozi Kilimanjaro International Leather Industries Co Ltd. Akiongea mara baada ya kutembelea kiwanda hicho  mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe.  Agustine Holle amesema kuwa kutokana na uwekezaji wenye tija waliouona utaiwezesha  serikali kuongeza  mapato. Vile vile kiwanda hicho kitaunufaisha mkoa wa Kilimanjaro pamoja na mikoa ya jirani kwa kuboresha mfumo wa maisha na kuongeza kipato kwa wakazi hao. Mwenyekiti amebainisha kuwa wameridhika na uendeshaji wa Kiwanda hicho ambapo kitakapokamilika kwa asilimia 100 kinakwenda kutoa ajira 3,000 kwa ajira za moja kwa moja na ajira nyingine zisizo za moja kwa moja ni 4,000. Kwa upande wake...

Wananchi Waendelea Kukumbushwa Kuchangia Nguvu Kazi Ujenzi Wa Shule Za Sekondari Musoma Vijijini

Na Shomari Binda-Musoma WANANCHI wa jimbo la Musoma Vijijini wamekumbushwa kuendelea kuchangia nguvu kazi katika ujenzi wa shule za sekondari unaoendelea kwenye maeneo yao. Ukumbusho huo umetolewa na mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo aliotoa leo februari 18 kwenda kwa wananchi. Amesema jimbo la Musoma Vijijini lenye jumla ya Kata 21 lina sekondari 26 za Kata zikiwa za serikali na 2 za binafsi.  Muhongo amesema sekondari 3 zinazojengwa na serikali kuu ambapo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika februari 28 katika Kijiji cha Butata Kata ya Bukima,Kijijini Kasoma Kata ya Nyamrandirira na Kijiji cha Kurwaki Kata ya Mugango  Amesema wanavijiji kwenye maeneo hayo wamekubali kuchangia nguvukazi zao kwenye ujenzi wa sekondari hizo na wengine wameendelea kukumbushwa. " Elimu bado ni kipaumbele chetu na tunaendelea kuwakumbusha wanavijiji kwenye maeneo ya ujenzi kuendelea kuchangia nguvu kazi. " Tunaishukuru sana serikali kuu kwa kuendelea kutuletea fedha nyingi...

Rais Mwinyi:Smz Itaendelea Kuwaunga Mkono Uwawaza

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea Kuunga mkono Harakati za Jumuiya ya Wawakilishi Wanawake  (UWAWAZA) za kuwajengea Uwezo Wanawake katika Maendeleo yao kisiasa,Kiuchumi na Kijamii. Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Wajumbe wa Jumuiya hiyo waliofika Ikulu kujitambulisha  na Kumpongeza Dkt, Mwinyi. Aidha Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Jumuiya hiyo ni sauti muhimu katika kupigania haki za Wanawake ndani na Nje ya Baraza la Wawakilishi na kuahidi kuendelea  kuiunga Mkono  kuyafikia Malengo  yao. Ameeleza kufarijika na kazi zinazofanywa na Jumuiya hiyo za  kuimarisha  Ushiriki na kuongeza Idadi ya Wajumbe Wanawake katika Baraza la Wawakilishi  kwani Uzoefu unaonesha  Wanawake wanafanya Vizuri katika Uongozi. Rais Dkt, Mwinyi ametumia fursa hiyo kuwahamasisha Wanawake Kutosita kugombea nafasi za Uongozi katika  Uchaguzi Ujao ili kuongeza Idadi yao katika Baraza la ...

Wasira Azungumza Na Balozi Wa Jamhuri Ya Korea Nchini

 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara)Ndg. Stephen M. Wasira amefanya mazungumzo na Mhe. Eunju Ahn, Balozi wa Jamhuri wa Korea Nchini,  Leo tarehe 18/2/2025 katika Ofisi  ndogo ya  makao makuu ya CCM Lumumba, Dar es Salaam.  Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamebadilishana mawazo katika namna mbalimbali yanayohusu ushirikiano wa nchi ya Tanzania na Korea.

Waziri Mkuu Akutana Na Balozi Wa Umoja Wa Ulaya Nchini

_▪️Pia ateta na Balozi wa Jamhuri ya  Korea_ _▪️Awaahidi kuendeleza ushirikiano_ WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Februari 18, 2025 amefanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Christine Grau, Ofisini ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es salaam. Katika mazungumzo hayo Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Tanzania itaendelea kukuza na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji na nchi za Umoja wa Ulaya. “Inatia faraja sana kuona kuna ukuaji wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na nchi za Umoja wa Ulaya, Umoja wa Ulaya umewekeza takriban euro bilioni tatu nchini, hii kwa kiasi kikubwa imechangia kutengeneza ajira na makusanyo ya kodi. ” Amesema kuwa Tanzania itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji ili kuzivutia sekta binafsi kushiriki katika shughuli za maendeleo. Kadhalika Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Tanzania inathamini msaada mkubwa ambao unatolewa na Umoja wa Ulaya katika kuchangia shughuli za maendeleo nchini.  “Katika kipindi cha 2021-...

Mkuu Wa Mkoa Wa Mara Kanali Mtambi Ampokea Na Kuteta Na Meja Jenerali Gaguti km

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 18/2/2025 amempokea na kuzungumza na Mkuu wa Utumishi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Jenerali Marco Gaguti na ujumbe wake waliopo katika ziara ya kikazi katika Mkoa wa Mara.  Akizungumza katika mapokezi hayo yaliyofanyika ofisini kwake, Mhe. Mtambi amesema hali ya usalama ya Mkoa wa Mara ni shwari na wananchi wanaendelea kufanya shughuli zao za kawaida za maendeleo.  Mhe. Mtambi amelipongeza Jeshi la Ulinzi laWananchi wa Tanzania kwa kazi nzuri wanayoifanya kulinda amani na usalama wa nchi na hususan katika maeneo ya mipaka ya Tanzania.  Mhe. Mtambi amelishukuru JWTZ kwa ushirikiano wanaoutoa kwa Serikali ya Mkoa na kuahidi kuwa viongozi na Kamati ya Usalama ya Mkoa itaendelea kutoa ushirikiano kwa JWTZ katika utekelezaji wa majukumu yao katika Mkoa wa Mara.   Kwa upande wake, Meja Jenerali Gaguti akizungumza katika mapokezi hayo amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Mara na Kamati ya...