Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali imeendelea kuimarisha tahadhari na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Ebola ili kuzuia hatari ya ugonjwa huo kuingia na kusambaa nchini. Akijibu maswali ya Papo kwa Papo Bungeni jijini Dodoma leo Juni 4, 2026, Dkt. Mwigulu alisema Tanzania inaendelea kuwa na mahusiano ya karibu na mataifa jirani kupitia shughuli za kijamii, kiuchumi na kiutamaduni, hali inayochochea mwingiliano wa watu kuvuka mipaka na hivyo kuhitaji umakini mkubwa katika kudhibiti magonjwa ya mlipuko. Amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali za kinga ikiwemo kuendelea kutoa elimu kwa umma kupitia majukwaa tofauti, kuhamasisha wananchi kuzingatia tahadhari za kiafya na kuimarisha ufuatiliaji katika maeneo ya mipakani na sehemu nyingine muhimu. “Tanzania si kisiwa. Kila mwananchi ana wajibu wa kushiriki katika mapambano dhidi ya Ebola kwa kuzingatia tahadhari na kutoa taarifa mapema pale anapoona dalili zinazoweza kuashiria ugonjwa huo,” ame...
Marato tv - Sauti ya Jamii