Wananchi wa Kata ya Zuzu, Jijini Dodoma, wameibuka na malalamiko makali yenye hisia nzito na machungu makubwa, wakimlenga Diwani wa kata hiyo kwa kumtuhumu kuhusika katika kufungwa kwa eneo la uchimbaji wa kokoto na mchanga ambalo lilikuwa mkombozi wao wa maisha kwa zaidi ya wananchi 300. Kwa sauti zilizotawaliwa na huzuni, hasira na wakati mwingine machozi yakibubujika, wananchi hao wamesimulia jinsi maisha yao yalivyoporomoka ghafla kufuatia kufungwa kwa eneo hilo, wakisema walikuwa wakitegemea uchimbaji huo kama chanzo kikuu cha kipato cha kila siku. Wamesema kupitia shughuli hizo walikuwa wakigharamia mahitaji ya familia, ada za shule za watoto na matumizi ya msingi ya nyumbani, lakini sasa wamebaki wakikabiliwa na hali ngumu ya maisha isiyo na uhakika wala matumaini. Kwa hisia kali na maumivu ya wazi, wananchi hao wamedai kuwa uamuzi wa kufungwa kwa eneo hilo ulifanyika bila kushirikishwa wala kufanyika mkutano wa pamoja wa wananchi, jambo ambalo wamesema limeongeza hasira, m...
Marato tv - Sauti ya Jamii