Serikali imeendelea kuimarisha Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ili kiweze kuzalisha wataalamu wenye ujuzi wa kukidhi mahitaji ya sekta ya uchukuzi, sambamba na uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanyika katika miundombinu ya usafirishaji nchini. Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Mhandisi Dkt. Prosper Mgaya. amesema chuo hicho kilianzishwa mwaka 1975 kama kitengo cha Shirika la Usafirishaji la Taifa, kabla ya kupandishwa hadhi mwaka 1982 kuwa taasisi ya elimu ya juu yenye jukumu la kutoa mafunzo, kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu katika sekta ya uchukuzi. Amesema baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977, Tanzania ilikabiliwa na uhaba wa wataalamu wa sekta ya usafirishaji, hali iliyoifanya Serikali kuimarisha chuo hicho ili kiweze kuzalisha wataalamu wa usafiri wa barabara, reli, anga na majini. Aidha, ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa unaoendelea ku...
Marato tv - Sauti ya Jamii