Skip to main content

Posts

Showing posts from August 20, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKUU WA MAJESHI WA MALAWI

 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb), tarehe 20 Agosti 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Malawi, Jenerali George Jaffu, ambaye yupo nchini kwa ziara rasmi ya kikazi. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Upanga, jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu ushirikiano wa kiulinzi na kijeshi kati ya Tanzania na Malawi. Katika mazungumzo hayo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ameeleza kuridhishwa na uhusiano mzuri na wa muda mrefu uliopo kati ya Majeshi ya Tanzania na Malawi. Amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha na kudumisha uhusiano huo wa kihistoria kwa manufaa ya nchi na wananchi wa mataifa hayo mawili. Kwa upande wake, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Malawi, Jenerali George Jaffu, ametoa shukrani kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa msaada mbalimbali ambao umekuwa ukitolewa kwa Malawi k...

TAASISI YA SANJEEV MANSOTRA NA MBUNGE MAVUNDE WAKABIDHI MADARASA 10 NA MAABARA 3 ZA SAYANSI JIJINI DODOMA

Taasisi ya Sanjeev Mansotra Foundation kwa ushirikiano na Mbunge wa Jimbo la Mtumba Mh. Anthony Mavunde wamekabidhi madarasa 10 na maabara 3 za sayansi zenye jumla ya thamani ya Tsh 444,700,000 kwa shule ya Sekondari Anthony Mavunde-Mkoyo,Hombolo na Shule ya Msingi Makutupora. Akizungumza katika hafla hiyo,Mbunge Mavunde amewashukuru wananchi wa Mkoyo kwa kumuunga mkono wakati anaanzisha ujenzi wa shule hiyo ili kuwanusuru watoto waliokuwa wakitembea kilomita 18 kufuata Shule. Aidha, Mavunde ameishukuru serikali chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa kuunga mkono juhudi hizo na kuchangia ujenzi wa madarasa ambayo inawafanya wanafunzi wasome katika mazingira ya utulivu. Aidha,Mbunge Mavunde ameishukuru Taasisi ya Sanjeev Mansotra kwa ujenzi wa madarasa na maabara ambazo zitasaidia wanafunzi kuwa na mazingira mazuri ya ufundishwaji na kupunguza msongamano wa wanafunzi hasa kwa Shule ya Msingi Makutupora. Akitoa salamu zake,Mwakilishi wa Taasisi ya Sanjeev Mansotra Ndg. Da...

SAGINI AWAFUNDA VIONGOZI NA WATENDAJI DIRA 2050 MKOA WA SONGWE*

 Imeelezwa kuwa namna ya kufikisha na kufanikisha *Utekelezaji wa Dira 2050* ni kuwepo na uundaji wa Kamati za Usimamizi, Ufuatiliaji na Utekelezaji kwenye ngazi zote pamoja na mkakati mawasiliano utumiwe ipasavyo kufikisha ujumbe kwa viongozi na wananchi. Hayo yameelezwa na *Mhe. Jumanne Abdallah Sagini* Agosti 20, 2026 wakati alipokuwa akitoa *Mafunzo ya Kujenga Uwezo wa Viongozi na Watendaji wa Mkoa wa Songwe kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050* katika Jukwaa la Dira yenye mada ya "Uongozi wa Kimkakati na Mabadiliko ya Fikra Kiuongozi na Kiutendaji katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa kuwezesha Utekelezaji wa Dira 2050"  *Sagini* ameeleza kuwa kufanikisha kwa *Dira 2050* hakutegemei fedha tu bali watu wakiwemo viongozi, Watendaji katika Sekta binafsi ambapo viongozi watendaji watasaidia kutafsiri Dira katika mipango mikakati inayotekelezeka. "Mabadiliko ya fikra kwetu sote ni injini ya kutufikisha kwenye matokeo tarajiwa na ajenda ya utekelezaji wa *Dira 2050* iwe y...

TACAIDS YAWEKA MIKAKATI MADHUBUTI KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

  Na, Mwandishi Wetu – Dodoma Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) inaendelea kuimarisha mikakati madhubuti ya kupambana na VVU na UKIMWI kupitia ushirikiano wa kisekta, kuhamasisha vyanzo vya fedha vya ndani, kusogeza huduma karibu na jamii ikiwemo Vituo vya Maarifa kwa madereva wa malori na kuwajengea uwezo vijana na wanawake ili kufikia lengo la kutokomeza kabisa janga hili ifikapo mwaka 2030. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI ilipokutana kwa lengo la kupokea taarifa ya wasilisho la hali ya Maambukizi ya VVU na UKIMWI kwa Vijana na Mkakati wa Kupunguza Maambukizi Mapya kwa Vijana, kilichofanyika tarehe 20 Agosti, 2026 Bungeni Jijini Dodoma. Waziri Kabudi ameipongeza Kamati kwa namna ilivyoshauri na kupendekeza  uboreshwaji wa masuala  mbalimbali ikiwemo matumizi ya teknolojia katika utoaji wa h...

JOWUTA NA OJA KUIBUA FURSA ZA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI KUPITIA HABARI

     Mwandishi Wetu Jovina Massano Chama Cha wafanyakazi katika vyombo vya habari Tanzania (JOWUTA)na Chama Cha waandishi wa habari wa Ufalme wa Oman(OJA) kushirikiana katika kuibua fursa za kiuchumi kupitia habari. Maamuzi hayo yametolewa mara baada ya ujumbe maalum kufika hapa nchini Agosti 19,2026 ukiongozwa na makamu Mwenyekiti wa OJA Salem Hamad Al-Jahwari.  Ujumbe huo umefanya mazungumzo na Chama cha wafanyakazi katika vyombo vya habari (JOWUTA) pamoja na Serikali na kukubaliana kuandaa kongamano la kimataifa ambalo litahusisha wanahabari wa nchi hizo na sekta nyingine. Makubaliano hayo yamefikiwa katika ziara ya kikazi yenye lengo la kuimarisha uhusiano wa kitaalamu na kindugu, baina ya Oman na Tanzania, mazungumzo ambayo yamehudhuriwa na maafisa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Idara ya Habari - Maelezo Jijini Dar es Salaam. Ujumbe huo wa OJA, upo nchini kwa mwaliko wa JOWUTA, unaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa OJA. Katika kikao hicho,...

JOWUTA NA OJA KUIBUA FURSA ZA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI KUPITIA HABARI

   Mwandishi Wetu Jovina Massano Chama Cha wafanyakazi katika vyombo vya habari Tanzania (JOWUTA)na Chama Cha waandishi wa habari wa Ufalme wa Oman(OJA) kushirikiana katika kuibua fursa za kiuchumi kupitia habari. Maamuzi hayo yametolewa mara baada ya ujumbe maalum kufika hapa nchini Agosti 19,2026 ukiongozwa na makamu Mwenyekiti wa OJA Salem Hamad Al-Jahwari.  Ujumbe huo umefanya mazungumzo na Chama cha wafanyakazi katika vyombo vya habari (JOWUTA) pamoja na Serikali na kukubaliana kuandaa kongamano la kimataifa ambalo litahusisha wanahabari wa nchi hizo na sekta nyingine. Makubaliano hayo yamefikiwa katika ziara ya kikazi yenye lengo la kuimarisha uhusiano wa kitaalamu na kindugu, baina ya Oman na Tanzania, mazungumzo ambayo yamehudhuriwa na maafisa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Idara ya Habari - Maelezo Jijini Dar es Salaam. Ujumbe huo wa OJA, upo nchini kwa mwaliko wa JOWUTA, unaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa OJA. Katika kikao hicho, Al-Jah...

TCRA YAKUMBUSHA BLOGU ZISIZOSAJILIWA, YASHUSHA LESENI HADI ELFU 50

 Na MASHAKA MHANDO, Tanga Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa onyo kali kwa wamiliki wa blogu, tovuti (websites), na mawakala wa habari mtandaoni wanaosambaza habari bila kusajiliwa na kupata leseni, ikieleza kuwa wanafanya makosa ya jinai na watachukuliwa hatua kali za kisheria. Hata hivyo, ili kuweka mazingira rafiki, TCRA imetangaza kushusha gharama za usajili na kupata leseni kutoka Shilingi 500,000 za awali hadi Shilingi 50,000 pekee, ili kutoa fursa kwa kila mwandishi wa mtandaoni kutambulika kisheria. Onyo hilo limetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa TCRA, Rolf Kibaja, wakati akizungumza kwenye Maonesho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika jijini Tanga. Kibaja aliwataka wamiliki hao kutojidanganya kuwa hawajulikani, akisisitiza kuwa TCRA ina mfumo thabiti wa kufuatilia anga mtandao (Cyberspace) ambao kila baada ya saa sita hutoa taarifa za kile kinachorushwa, ambapo hadi sasa wanaona utendaji wa runinga za mtanda...

TACAIDS YAWEKA MIKAKATI MADHUBUTI KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

 Na, Mwandishi Wetu – Dodoma Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) inaendelea kuimarisha mikakati madhubuti ya kupambana na VVU na UKIMWI kupitia ushirikiano wa kisekta, kuhamasisha vyanzo vya fedha vya ndani, kusogeza huduma karibu na jamii ikiwemo Vituo vya Maarifa kwa madereva wa malori na kuwajengea uwezo vijana na wanawake ili kufikia lengo la kutokomeza kabisa janga hili ifikapo mwaka 2030. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI ilipokutana kwa lengo la kupokea taarifa ya wasilisho la hali ya Maambukizi ya VVU na UKIMWI kwa Vijana na Mkakati wa Kupunguza Maambukizi Mapya kwa Vijana, kilichofanyika tarehe 20 Agosti, 2026 Bungeni Jijini Dodoma. Waziri Kabudi ameipongeza Kamati kwa namna ilivyoshauri na kupendekeza  uboreshwaji wa masuala  mbalimbali ikiwemo matumizi ya teknolojia katika utoaji wa hu...